Greatest Of All Time
JF-Expert Member
- Jan 1, 2017
- 23,620
- 52,790
Mkataba wake wa Sasa ukiisha atapewa mkono wa kwaheriKinachomuweka mpaka sasa Mkude Simba labda ni kwasababu anapendwa tuu na Mkuu MO na wanasimba kwa ujumla, na pia ni mtoto wa nyumbani, nje ya hapo huyu hakutakiwa kuwepo. Mchezaji kila siku kesi mara injury, Tadeo kwasababu sio mtoto wa nyumbani ndomana msimu mmoja tuu wa injury umetosha kumfukuzisha.
Kabla ya Thadeo lwanga alikuwepo James kotei na kisha akaja FragaKufatia tetesi za kuondoka kwa Tadeo Lwanga na kutua kwa Mnigeria Akpan klabuni Simba, ni muendelezo wa ujio na kuondoka kwa viungo wakabaji Simba lakini wote hao wamekuwa wakimkuta na kumuacha Jonas Gerald Mkude.
Jonas Mkude sio wa kawaida ana kitu cha ziada inaonekana ambacho Viungo wengine hasa wa kigeni hawana.
Haya mimi naanza na Tadeo Lwanga ambaye anaondoka Simba kwa sababu ya majareha yasiyoisha...endelea na wewe
Fraga aliondoka kama anavyoondoka Lwanga...majerahaKabla ya Thadeo lwanga alikuwepo James kotei na kisha akaja Fraga
mama yako ndo alimfundisha hizo tabia za gizaMkude kubaki Simba ni Nguvu za Giza tu, maana Hana tabia yoyote Ya kiungo wa ulinzi au kiungo wa ushambuliaji.
Haruki mipira ya kichwa, Hana uwezo wa kunyang'anya mipira, Hana uwezo katika mipira ya 50/50 , Hana uwezo wa kucheza Kwa Kasi.
Kitu kimoja alichonacho ni kuweza kukaa na mpira na nguvu ya miguu ila mzito wa maamuzi.
Hapana Si mama yangu ila uwezo wake unatia shaka, makocha wengi wakija awamtumii na mbaya zaidi anatatizo la kinidhamu Cha kushangaza wamekuja wachezaji wengi wanaondoka tena wengi wamemzidi ki uchezaji.mama yako ndo alimfundisha hizo tabia za giza
Mimi ni Yanga ila nashangaa yule Abdul swamadu alikosaje kucheza pale Simba na anauwezo mkubwa ki uchezaji hasa kama namba sita. Ana Kaba, ana pora mipira, anacheza mipira ya juu, ana utulivu ila alitolewa Kwa mkopo aka achwa Mkude.Kahata aliachwa kimakosa,Abdull Swamadu akupewa nafasi.
Mkuu nilifikiri mimi peke yangu ndio nauona ubora wa Abdulswamadu. Uwezo wa Abdulswamadu Mkude haiingii hata nusu yake. Jamaa anakaba kwa nguvu, anapora mipira, ana piga pasi vizuri zenye macho, anaingia mwilini, ana kasi nzuri na kazi chafu pale kati anaziweza lakini maajabu anatolewa kwa mkopo/sijui kavunjiwa mkataba halafu Mkude anabaki. Kwa mpira wa kisasa kiungo mkabaji lazima awe anakaba kwa nguvu na kucheza faulu za akili ili mabeki wa kati wawe na kazi rahisi. Ukitaka kujua hayo mwangalie Lwanga kabla ya majeraha mabeki wa kati wakina Wawa na Onyango walikuwa hawana kazi kubwa na hata Yanga chini ya Bangala sasa hivi Mwamnyeto na Job hawana kazi kubwa.Mimi ni Yanga ila nashangaa yule Abdul swamadu alikosaje kucheza pale Simba na anauwezo mkubwa ki uchezaji hasa kama namba sita. Ana Kaba, ana pora mipira, anacheza mipira ya juu, ana utulivu ila alitolewa Kwa mkopo aka achwa Mkude.
Mpira wa Tanzania una mambo ya ajabu sana.
Ata Mzamiru ni mchezaji mzuri japo ana matatizo ya pasi za mwisho ila si waku Kaa bench.
Mzamiru anajituma sana ila anadharaulika sana.
Kwasasa yuko wapi?Mkuu nilifikiri mimi peke yangu ndio nauona ubora wa Abdulswamadu. Uwezo wa Abdulswamadu Mkude haiingii hata nusu yake. Jamaa anakaba kwa nguvu, anapora mipira, ana piga pasi vizuri zenye macho, anaingia mwilini, ana kasi nzuri na kazi chafu pale kati anaziweza lakini maajabu anatolewa kwa mkopo/sijui kavunjiwa mkataba halafu Mkude anabaki. Kwa mpira wa kisasa kiungo mkabaji lazima awe anakaba kwa nguvu na kucheza faulu za akili ili mabeki wa kati wawe na kazi rahisi. Ukitaka kujua hayo mwangalie Lwanga kabla ya majeraha mabeki wa kati wakina Wawa na Onyango walikuwa hawana kazi kubwa na hata Yanga chini ya Bangala sasa hivi Mwamnyeto na Job hawana kazi kubwa.
Leo Simba wanashangaa eti Yanga kachukuaje ubingwa wakati wachezaji wa maana kama Abdulswamadu wanatolewa kwa mkopo/wanavunjiwa mikataba kirahisi tu. Lakini wachezaji wa hovyo kama wakina Yusuph Mhilu ambaye amepewa mechi nyingi mpaka za kimataifa na bado kachemsha lakini unashangaa bado yupo mpaka leo. Nina hakika Abdulswamadu angeendela kubaki Simba miaka miwili ijayo wala wasingehangaika na hawa viungo wakabaji wanaotoka nje kwa mamilioni ya pesa halafu wanasepa baada ya muda mfupi.
Mara ya mwisho nimemuona kama sikosei Ruvu ya Mkwasa.Kwasasa yuko wapi?