Tujikumbushe Wachezaji walioletwa mjini na Mnyama wakaishia Jangwani

mmteule

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
5,883
Reaction score
14,600
Miongoni mwa visa wa watani wa Jadi ni kuchuana kunasa saini za wachezaji wanaotamba kwenye vilabu mbalimbali nje na ndani ya Tanzania. Kuna wachezaji kadhaa ambao walilipiwa ticket za Ndege, Basi, Taxi, nk nk na Timu ya Msimbazi lkn walipotua tu Jijini walinaswa na watani zao Yanga na hivyo Simba kuishia kunawa, Tujikumbushe Visa hivyo;

1. Pius Buswita kutoka Mbao FC ........ "yanga ni kuzuri"
2. Malimi Busungu kutoka Mgambo JKT........ "simba ni wababaishaji"
3. Deus Kaseke Kutoka Mbeya City ............... "simba hawaeleweki"
4. Mbuyu Twite kutoka Congo .............. "naangalia maslahi"
5. Paul Nonga .................. "Yanga ndio saizi yangu"

Mdogo wangu Ngosha Buswita ukitaka kujua laana ya usaliti watafute hao wenzio uwaulize kilichowakuta! Ongezeeeni waliomtema Mnyama wakaja kujuta kama Malimi Busungu anavyolialia kule Lipuli, ukikaa naye unaweza kumwombea poo kwa Hanspope kwa kosa alilofanya.
 
Kauli zao zilikuwa thabiti ..... Ukiwa na akili zako timamu huwezi kucheza na MBUMBUMBU.
 
Chuji ............. "bora niuze ndimu kuliko kucheza Simba" .......... baadae alirud simba
Victor Costa .......... "Niko tayari kustaafu kuliko kurudi simba" ............ baadae alirud msimbaz
Messi ................. "Simba ni matapeli"
Ajib ................. "sina raha nikiwa simba" (Zamalek huendi Ng'ooooo wenzio hawaachiagi wachezaji kutafuta maisha)
Yondani ........... ''simba wana dharau"
Kaseja ............ "nafuata Pesa"............ baadae alirud msimbaz
Okwi ............... 'nafuata Pesa"............ baadae alirud msimbaz
Simba haijawah kumwacha mtu salama ni historia haisemi uongo Ipo siku watarudi tu!
 
Wote ulio wataja wamebeba "Ndoo ya VPL" wakiwa jangwani, sasa sijui Buswita na Mkude ni nani wa kujutia na pahala alipo!
 


Mkuu kunakitu kimoja ambacho hujakielewa, kitu ambacho kinawavutia wachezaji wengi sana kuja kucheza soka Jangwani. Hakuna jambo lingine ambalo Yanga inawavutia wachezaji wengi ndani na nje ya nchi kama si "MATAJI".

Kati ya hao ulio wataja wengi walikuja huko simba wakiwa wamekwisha twaa Mataji pale jangwani. Pia wengi wao walikuja Simba wakiwa wanakaribia kutunika daluga lao. Eg (Kiiza Hamisi Diedo).

Asilimia 80% ya wachezaji hao wote ulio wataja wameonja medali za Ubingwa wa VPL.
 
Kauli zao zilikuwa thabiti ..... Ukiwa na akili zako timamu huwezi kucheza na MBUMBUMBU.


Ni kweli, Mchezaji yeyote mwenye ndoto ya kutwaa Ubingwa wa VPL na kushiriki michuano nje ya Bongo ni lazima jicho lake lielekee Jangwani.
 
katika hao uliiwataja ni mbuyu twite pekee alitamba wengine.wote waliishia kutupiwa virago mwisho.wa msimu

nakuongezea mwingine feitoto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…