Tujikumbushe watangazaji maarufu Radio one enzi hizo

masare

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Posts
1,791
Reaction score
1,830
Mwaka 1994 Radio One FM Stereo ilikua radio station binafsi ya pili kuanzishwa baada ya Radio Tumaini iliyoanzishwa kwa majaribio mwaka 1993.
Ni dhahiri ilitokea kuteka Dar Es Salaam yote pamoja na mikoa mingine mitano ambayo ilianza nao kusikika yaani Dodoma, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza na Tanga.

Ubunifu pamoja na Watangazaji machachari uliibeba sana Radio One Stereo enzi za 1994 hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 ambapo ilikua haina mshindani licha ya kuongezeka kwa idadi ya radio station za binafsi apa DarEsSalaam na mikoani pia.

Kwa sasa watangazaji "wakongwe" waliobakia Radio One ni watatu tu, Aboubakar Sadiq-alitokea East Africa FM(Sikuhz yaitwa East Africa Radio),Deo Rweyunga pamoja na Abdallah Mwaipaya -alitokea PRT(Sikuhz inaitwa TBC FM)

Wafuatao ni baadhi ya watangazaji wa Radio One wa enzihizo waliotengeneza njia ya kizazi kipya cha utangazaji Tanzania;

-Mike Mhagama
-Taji Liundi
-Master Voice
-DJ Ommy
-DJ JD
-Aboubakar Liongo
-Abdallah Majura
-Rose Chitala
-Asia Mohammed
-Flora Nducha
-Leila Muhaji
-Janet Sostheness
-Sos B
-Basil Mbakile
-Masoud Masoud
-Mikidadi Mahmoud
-Amina Saleh
-Misanya Bingi

Ongezea na wengine.
 
Daaah,hivi Asia Mohamed yuko wapi kweli.
 
Samahani kwa kutoka nje ya mada,kuna mzee mmoja miaka kama mitano iliyopita alikuwa anasoma sana taarifa ya habari pale ITV,jina limenitoka,nikumbusheni tafadhali!
 
Samahani kwa kutoka nje ya mada,kuna mzee mmoja miaka kama mitano iliyopita alikuwa anasoma sana taarifa ya habari pale ITV,jina limenitoka,nikumbusheni tafadhali!
Nadhani ni R. Masako. Aliyekuwa akikiendesha kipindi cha Kipima Joto. Alijiunga na siasa akashindwa na kastaafu sasa.
 
Vick Msina, Sunday Shomali, Ramkim Ramadhani ( RIP), Lyongo, Vick Mtetema
 
Umenikumbusha mbali sana!

Nakiri kuwa tulikuwa na Watangazaji.Sasa hivi tuna watangazaji wa Chap chap, kujuana kwingi, ujanja ujanja nk.Kiufupi Tasnia ya Habari imevamiwa na Utumwa mamboleo.

Katika upande wa Television, now days tupo na kina George Maratu, Charles Masanyika, Mabele Makubi, Spenser Lameck, Hemed Kivuyo nk.Huwa najiuliza, kwenye interview walipitaje?.Nb;kama huna japo a, b, c, d's za Mass comm and Journalism tusibishane katika hili.

Mwisho wa siku naishia kupata majibu kuwa, WALIBEBWA.Then nazima Tv.

Big up sana kwa uliowataja huku nikirudia kum-mention Masoud Masoud (Manju wa muziki) kwa mara ya pili.Huyu Jamaa ana skills za hatari kuhusu Muziki hana mfano, Ana ujuzi wa Lugha zaidi ya 3 (Internationally).Alikuwa na sauti hiyo!!!, lazima uipende.Then majigambo 0.Big up kwake.

Walikuwa wakitangaza mpaka Unasisimka.Unahisi upepo umesimama kwa Muda.
 
Vp Julius nyaisanga mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…