Tujikumbushe yaliyopita: Mwalimu wako wa somo la HESABU/HISABATI mlikuwa mnamuita kwa jina gani?

TRIPLE H

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2013
Posts
651
Reaction score
349
Wadau,
Nataka tujikumbushe jambo hili kwa sababu wengi tuliopita shule za msingi na hata sekondari kila shule ilikuwa na majina bandia kwa walimu wa somo la hesabu/hisabati.Kwa mfano pale s/m Mugabe (sinza) mwl. wetu wa hisabati sisi darasa la sita tulimuita 'mibuti' kwa sababu kama angeuliza swali likakushinda au angetoa kazi usiifanye ungesikia anang'aka 'nitakulima mibuti' na pale loyola mwl. wetu wa 'mathe' tulimuita 'sequence' kwa kuwa aliifundisha mada hii kwa ufanisi zaidi.
Wewe kama ulipitapita school japo kidogo mwalimu wako kuna a.k.a/id fulani mlimpa.Jikumbushe kwa kutaja shule na 'id' ya mwalimu husika.Cheerio!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…