Salam wakuu,
Nakumbuka back in days shuleni, kulikua na formula zilizotengenezwa kama nyimbo hivi ili kufanya wepesi kwa wanafunzi kukariri. Kwa mfano, kwenye periodic table kulikua na: Halo hemedi lile beberu bora chinja na ondoa figo nene na mgeni aliyeua simba pale serengeti club arudi kwao canada.
Vile vile kwenye kukariri planets kulikua na: Mama veronica egesha mapaja juu ya sanduku upate nenepa paja. Je ni zipi nyingine unazikumbuka?