Uchaguzi 2020 Tujitokeze kwa wingi kupiga kura tarehe 28 Oktoba, 2020

Uchaguzi 2020 Tujitokeze kwa wingi kupiga kura tarehe 28 Oktoba, 2020

Joined
Sep 20, 2020
Posts
48
Reaction score
40
Na V. M

[emoji736]Hakika nimejionea Mwaka 2020- Kumeendelea kuwa na Ushiriki mzuri wa Wanawake katika mchakato Mzima wa Uchaguzi; [emoji994]

Nchini Tanzania kumekuwa na hamasa na muamko mkubwa mno wa Ushiriki kwa wanawake-

Kama Taifa tunajivunia kuwa na Makamu wa Rais Mwanamke (anayetetea nafasi yake) na tuna imani naye na Utendaji wake, ameendelea kuwa mama wa Mfano, Mwanamke Kiongozi wa Mfano kwa Taifa letu la Tanzania[emoji1241]

Kuna Wanawake wengi wamejitokeza kwenye mchakato Mzima wa kupitishwa na vyama vyao kushiriki kwenye Uchaguzi wa Kitaifa wa 2020, kwa ngazi mbalimbali na tunajivunia Wanawake wa Shoka wote waliopata nafasi ya kujitokeza na waliopata nafasi za kuteuliwa na vyama vyao kuwakilisha kwenye Kata, Majimboni na Taifa ambapo Nchi yetu inaelekea kuwachagua Viongozi wetu Tarehe 28 October, kwa ngazi tofauti tofauti- Urais, Ubunge (Bara), Uwakilishi (Zanzibar) na Udiwani

Wanawake waliopata dhamana ya kuwania nafasi mbalimbali, jukumu Lao si tu kuwakilisha wananchi wa maeneo yao kwa ngazi tofauti tofauti.

Bali kuendelea kuonesha uwezo wa Wanawake, juhudi za Wanawake, na utashi wa wao katika nafasi za uongozi pindi pale watakapoamiwa na kupata dhamana za kuongoza Taifa letu la Tanzania kwa ngazi husika[emoji1241]

[emoji736]Ushiriki wa Wanawake si tu kwenye kuwania nafasi, bali pia kwenye Ushiriki katika Kampeni- kuwa wasimamizi wa wagombea (Campaign Managers and Strategists), kusimamia Kampeni mtandaoni, kufanya Kampeni field, kufanya Kampeni nyumba kwa nyumba, na Ushiriki wa jumla kwa ngazi tofauti tofauti.

Tumejionea Kampeni zilizofanywa kwa weledi mkubwa na Wanawake wote- na imani yangu ni kuwa Wanawake, Mabinti wengi zaidi wataendelea kuinuka kupitia Wanawake wa Shoka wanaoendelea kujitolea kikamilifu kwa ajili ya ustawi wa Taifa letu Tanzania

Ni bayana Wanawake wameendelea kushika mstari wa mbele katika Ushiriki kwa nyanja zote. Ushiriki, usimamizi, na maamuzi kiujumla, nasi sote tunajivunia nguvu yetu.

[emoji1417]Rai yangu haswa kwa Mabinti ni kuendelea kushiriki, kujifunza na kujitoa,kujinoa na kuenga hoja, aidha kuwa na uelewa wa kina wa masuala yote yanayohusiana na Maendeleo ya Taifa letu la Tanzania [emoji1241]

Mwenyezi Mungu aendelee kulinda Taifa letu na kubariki Viongozi na Watumishi wote waendelee kufanya maamuzi sahihi yenye manufaa kwa taifa letu, Yaani yenye ustawi kwa Taifa letu la Tanzania [emoji1241]

Mabinti, Wakinadada, Wanawake wote tujitokeze kwa wingi kupiga kura Tarehe 28 October 2020, Tufanye maamuzi sahihi ya kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kusimamia Maendeleo ya Taifa letu la Tanzania.

Tuhakikishe tunatumia vema haki yetu ya Msingi na tunashiriki kikamilifu na tunamaliza zoezi la kupiga kura, Salama salmini.
Mwenyezi Mungu aibariki Tanzania yetu, Amina[emoji2972][emoji1241]
 
Asante kwa kutukumbusha, Watanzania tuna hasira na msaliti wa Nchi kutoka ubeligiji

Amemtukana Rais wetu kila aina ya matusi na uongo, hasira zetu tunazielekeza kwenye boksi la kura
 
Asante kwa kutukumbusha, Watanzania tuna hasira na msaliti wa Nchi kutoka ubeligiji

Amemtukana Rais wetu kila aina ya matusi na uongo, hasira zetu tunazielekeza kwenye boksi la kura
Hatuwezi kuunga mkono watu wenye maslahi binafsi, wachonganishi na wenye kutafuta mbinu mbalimbali za kutuvuruga Watanzania.
TAREHE 28 OKTOBA tujitokeze kupiga kura
 
Back
Top Bottom