Tujitolee damu kwa hiyari kuokoa maisha ya wagonjwa

Tujitolee damu kwa hiyari kuokoa maisha ya wagonjwa

Visenti

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2008
Posts
1,025
Reaction score
329
blood donation.JPG
JE, KUNA MWANA JF HAJAWAHI KUJITOLEA DAMU?, TAFADHALI NAOMBA UTOE SABABU INAYOKUZUIA, JE NI KWASABABU YA DINI YAKO, MILA, HALI YAKO YA AFYA, KUOGOPA MAJIBU YA VVU, KUOGOPA SINDANO, AU SABABU YOYOTE INAYOKUZUIA USIJITOLEE DAMU KUOKOA MAISHA YA WENGINE, NAOMBA TUJADILI NA NITAJITAHIDI KUJIBU HOJA ZOTE NA KUTOA ELIMU
Mimi ni mchangiaji wa damu wa kudumu, hujitolea angalao mara mbili kila mwaka
 
Mkuu hilo nila muhimu sana tena la msingi kwa maisha ya binadamu!!!!:coffee:
 
Angalia mstari wa mwisho ktk hiyo post, mimi ni mchangiaji wa kudumu hujitolea angalao mara mbili kila mwaka,
hapa najaribu kuhamasisha wana JF wajitolee damu kupunguza vifo visivyo vya lazima na wahanga wakubwa ni akina mama na watoto, mahitaji yao ni makubwa sana na kuna shortage kubwa ya damu katika hospitali zote, I am curious kujua kwa nini wengi wetu tunaogopa kujitolea damu?
 
Umenena mkuu me cjawah kuchangia damu sababu ni asthmatic ila nipo kwenye blood donor club kama mhamasishaji. "donate blood save lives"
 
sina tatizo lolote napenda ila sijui nianzie wapi
 
Mimi sijawahi kutoa damu nadhani bado ninahofu ingawa natamani kufanya hivyo.kiafya ni mzima kabisa kwa vipimo halali nilivyopima dec mwaka jana,ila nina uzito wa kilo 47 na tatizo la low bloodpressure.nilitaka kutoa mwaka jana wakanambia nisubiri zifike kilo 50.ila kilichoniogopesha ni kwamba,damu yangu ni group O negative,na nasikia sisi watu wa group hili ni wachache hvyo wakikupata wanakufuatilia sana.wakihitaji damu ya group yangu watanisumbua hata kama kiafya si nzuri kutoa mara kwa mara.natamani sana kuchangia ila naogopa
 
Siogopi chochote kati ya ulivyo taja!Embu tuelekeze pakuanzia mi na shosti tukajitolee!
 
Zaidi hii inanigusa kwani nami niliwahi kusaidiwa damu na msamaria mwema wakati nikiwa na umri wa miezi sita nilipolazwa muhimbili baada ya kuugua maralia kali na dawa zote kudunda.aliyenisaidia hakuwa hata na undugu na mimi.nami nataka kuendeleza upendo huu kwa wengine.nipo tayari kuchangia damu
 
Hili ni jambo la muhimu sana,kujenga tabia ya kujitolea.Kama watu tunaweza kuhamasishana kukutana kwenye moja baridi moja moto,kuna wale walio kwenda Arusha kupunguza stress za maisha,kuna lile la kusaidia waathirika wa mafuriko,basi na hili pia linaweza kufanyika.Si lazima tukutane,bali tunaweza kuanza kwa kupeana taarifa ya unafanyaje ili uweze kujitolea damu kisha tukahamasishana kwenda kujitolea damu.Tafadhari muanzisha mada jibu maswali ya wadau hapo juu ili wakajitolee damu na kuokoa maisha ya watanzania wenzetu.Mie pia sijawahi kujitolea damu.
 
Umenena mkuu me cjawah kuchangia damu sababu ni asthmatic ila nipo kwenye blood donor club kama mhamasishaji. "donate blood save lives"

Ubarikiwe na uendelea kuhamsisha wengine
 
damu yangu ni group O negative,na nasikia sisi watu wa group hili ni wachache hvyo wakikupata wanakufuatilia sana.wakihitaji damu ya group yangu watanisumbua hata kama kiafya si nzuri kutoa mara kwa mara.natamani sana kuchangia ila naogopa
First Lady, kundi la damu yako ni special na adimu, usiogope hautasumbuliwa, watakuomba kiungwana na ni voluntary,hautalazimishwa, ikitokea inahitajika ujue anayehitaji hawezi ishi bila kumsaidia. unaweza kujitolea kila miezi minne (kila miezi mitatu kwa wanaume) bila madhara yoyote kiafya, hivyo uzito wako ukifikia 50kg anza kujitolea damu, kwani kila tone la damu linaenda kuokoa maisha ya mtu.
 
Wakuu - Shosti, Che kalizozele, FirstLady, Lizzy na wana JF wote,

Kuna program ya kitaifa ya DAMU SALAMA (NATIONAL BLOOD TRANSFUSION SERVICE), yenye vituo saba (6 Bara na 1 Unguja), wataalamu (Blood donation teams) wanaratiba za kupita maeneo mbalimbali katika kanda husika nchi nzima, ukitaka kujitolea damu unaweza kwenda katika kituo (Blood Transfusion Center) kilicho karibu yako, au waweza kuwasiliana nao kwa cm (angalia orodha ya vituo na simu hapo chini) ili kujua mobile blood donation team ipo maeneo gani. pia unaweza kuwaalika sehemu yako ya kazi ili na wengine waweze kujitolea damu.


VITUO VYA MPANGO WA DAMU SALAMA (Blood Transfusion Centers)


  1. Mpango wa damu salama makao makuu (DSM) - 022 2181873
  2. Dar es Salaam (Mashariki) - 022 2181871
  3. Mwanza (Ziwa)- 028 2500470
  4. Moshi (Kaskazini)- 027 2752892
  5. Mbeya (Nyanda za Juu Kusini)- 025 2502430
  6. Mtwara (Kusini) - 023 2334291-3

The blood you donate gives someone another chance of life.
One day that someone may be a close relative, a friend, a loved one –or even you.
 
Mimi sijawahi kutoa damu nadhani bado ninahofu ingawa natamani kufanya hivyo.kiafya ni mzima kabisa kwa vipimo halali nilivyopima dec mwaka jana,ila nina uzito wa kilo 47 na tatizo la low bloodpressure.nilitaka kutoa mwaka jana wakanambia nisubiri zifike kilo 50.ila kilichoniogopesha ni kwamba,damu yangu ni group O negative,na nasikia sisi watu wa group hili ni wachache hvyo wakikupata wanakufuatilia sana.wakihitaji damu ya group yangu watanisumbua hata kama kiafya si nzuri kutoa mara kwa mara.natamani sana kuchangia ila naogopa

Mama wa kwanza we ni wa nchi jirani nini? Kuna kanchi raia weng ni negatives. Hahahaa.
 
Umeanza lini kujitolea damu? Mi ni mwanachama, natoa damu kila baada ya miezi maitatu. Mbali na kuokoa maisha ya watu, mie huwa natoa damu kama sadaka sababu sina vijisenti vya kutoa sadaka.
 
Sina neno la kuongezea maana member wengi wametoa comments zao zilizoshiba, zaidi tu najiskia uchungu mno moyoni mwangu, kiukweli umenigusa sana Visenti, nami nitakwenda kutoa damu kwa wengine, nakumbuka marehemu Mama yangu aliongezewa damu sana, tena za watu tusionaundugu nao ambazo zilimpa maisha mapya kabla ya mauti kumkuta, yeye aliugua cancer ya damu. Kwa ajili ya mama yangu nitatoa damu yangu, kwa maisha ya wengine kama walivyojitahidi kuokoa maisha ya mpenzi wangu mama yangu.
 
Mimi kama mama wa kwanza hapo....nna blood group O negative lakini shida kilo 50 sijazifikia na wala sina nia ya kuzifikia kwa miaka hii ya karibuni.

Tanzania wangefanya kaa nchi za nje ambapo kuanzia kilo 40 unatoa damu, wangepata watu wengi zaidi.
 
Safi sana mimi pia ni mchangiaji mzuri sana wa damu. Tatizo linakuja kwenye majibu tu mkuu
 
nadhani hakuna elimu ya kutosha kuhusu hili...na tatizo lingine ni kuwa unaweza kujitolea bure lakini damu hiyo haigawiwi bure inauzwa na wajanja.........hakuna uaminifu watu wanajali matumbo yao tu
 
Safi sana mimi pia ni mchangiaji mzuri sana wa damu. Tatizo linakuja kwenye majibu tu mkuu
Sijakuelewa mkuu, unamaanisha majibu ya damu (test results) zinzchelewa kutoka au unaogopa kupata majibu?
 
nadhani hakuna elimu ya kutosha kuhusu hili...na tatizo lingine ni kuwa unaweza kujitolea bure lakini damu hiyo haigawiwi bure inauzwa na wajanja.........hakuna uaminifu watu wanajali matumbo yao tu
Ni kweli kuwa kuna rushwa hospitalini, lakini tujitolee damu na tupambane na rushwa, mara nyingi sisi wenyewe tunakuwa soft sana kutoa chochote kwa wahudumu wa afya.
 
Back
Top Bottom