Tujiulize kama Watanzania na Waafrika kwanini hatupati wabunifu wa kimataifa?


bado tunalalamikia wazungu tu kila kitu. Kuna vitu vichache kama system za Mpesa inawezekana chimbuko liko TZ. Lakini hatuwezi kusingizia wazungu kila kitu ni mazingira yetu. Wabunifu wa technology wengi ni vijana tu lakini wana mazingira mazuri. Mimi nipo nje miaka sasa na mambo mengi watu wanayosema sinkweli ni porojo tu ukiishi ndiyo unajua
 
uko sahihi lakini sikulenga kuwalalamikia wazungu bali kuonyesha mapungufu yetu kudhani kuna taifa linaweza kutusaidia sisi technology kwani kufanya hivyo kutakuwa na athali mbalimbali kwao ila kubwa ni kiuchumi na kiusalama pia si kweli kuwa wao hawana agenda zao,kumbuka tangu zama na zama ni hulka ya binadamu kutaka yeye na jamii yake wa survive Hivyo wakifanyachoiwe wazi au kwa kificho ni sehemu ya kutaka ku survive hivyo tusipotambua dhima yetu kama Watanzania kuwa tunapaswa kufikiri maisha yetu na vizazi vetu vijavvyo ni dhahili kuwa tutaangamia kwa ukosefu wetu wa maarifa tuidhani kuna watu toka sehemu nyingine kuja kubadili maisha yetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…