Tujivunie Majasho ya Mama zetu katika kutuandalia leo yetu

Tujivunie Majasho ya Mama zetu katika kutuandalia leo yetu

Zee la Mandandu

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2022
Posts
1,064
Reaction score
2,603
Leo tutumie platform hii kutambua, kuthamini na kuheshimu majasho ya mama zetu katika kutuandalia maisha yetu ya leo.

Binafsi naheshimu na kutambua thamani za Baba zetu katika kutufanya kuwa tulivyo na nitaleta uzi wa kutambua thamani yao ila leo naomba tutambue harakati za mama zetu katika kutuandalia leo zetu.

Binafsi nimesomeshwa kwa mama kuuza vitumbua na ufugaji wa Nguruwe hadi nikamaliza degree yangu 2008 pale SUA.
images-1.jpeg

Nawe tumia nafasi hii kumsalute mama yako na kutambua pamoja na kuthamini thamani ya jasho lake alilolimwaga ili kukufikisha hapo ulipo.
 
Unawezaje kutenganisha kiatu cha mguu wa kushoto na kulia, ilhali vyote vimekusaidia kuingia maliwato.
Hata huo uzi uliousubirisha wa baba, ambao umepanga kuujadili baadae, kwa mantiki hiyohiyo, utakuwa na mapungufu.
Kwenye malezi, baba ana nafasi yake na mama ana nafasi yake. Try to be rational unless you are not organised upstairs
 
Unawezaje kutenganisha kiatu cha mguu wa kushoto na kulia, ilhali vyote vimekusaidia kuingia maliwato.
Kuna walew walio lelewa na Mama zao pasi na Baba, na kuna wale ambao Baba zao hawakuwa na msaada wowote ingawa waliishi nao. Mifano iko mingi sana katika jamii zetu.
 
Kwa hakika mkuu mama zetu wabarikiwe sana. Mimi Namshukuru Kwa mengi hasa kunipa kipigo Cha mbwa Koko On the sports bila kusubiri mzee Kwa hakika mama yangu alikuwa anastahili nilikuwa nikianza mbio yupo Nami sijui alipita umiseta ama alikuwa mwana riadha hata sijui.

Hongera sana mama yangu.

Natoa laana ziwaendee wote wanaotoa mimba Kwa kisigizio Cha maisha magumu kumbe lengo aendelee kudanga.

Mleta Uzi umetuonyesha jinsi mama anatakiwa awe amekusomesha Kwa kuuza vitafunwa hongera zake nyingi sana mama yetu.
 
Inauma pale unapofika 20+ years unakuja kugundua baba uliyeaminishwa ni baba yako sio baba halisi. Ili ku balance mizani pia mama zetu wana dark side zao. Vice versa is true
 
Upendo wa mama kwa mwana ni wa asili , mama anampenda mwana na yupo tayari kwa lolote mtoto wake awe salama na mwenye furaha.
Sina shida na upendo wa mama, mama ana stahili kila aina ya pongezi na shukurani.
Mimi binafsi tokea nilipo pokea majukumu ya kuitwa baba, nachoweza kusema hakuna kama baba, nimegundua baba anatoa sadaka maisha yake kwa ajili ya watoto, tokea siku mwanaume anapoitwa baba basi maisha yake yeye binafsi yamefikia kikomo, sitaeleweka ila kwa mwanaume aliye baba natumaini atanielewa.
 
Back
Top Bottom