Davidmmarista
JF-Expert Member
- Apr 11, 2024
- 1,367
- 2,451
Wadau wa JF, habari zenu?
Katika hali ya sasa ambapo bei za mazao hubadilika mara kwa mara, ni muhimu kujua mwenendo wa soko ili kufanya maamuzi sahihi ya biashara na ununuzi. Leo tunajadili bei za mazao mbalimbali kote nchini.
Je, mkoani kwako bei zikoje kwa mazao haya?
Nb.Tutajie na mazao mengine yaliyo sahaulika!
Wakulima, wafanyabiashara, na walaji tushirikiane kupata taarifa sahihi za soko!
Tafadhali taja mkoa wako na bei unazozifahamu.
Waungwana karibu kwenye mjadala! 👇👇

- Mahindi – Bei ya kilo/gunia?
- Maharage – Ni aina gani zinapatikana zaidi, na bei yake kwa gunia/kilo?
- Mbaazi – Soko lake lipoje kwa sasa?
- Viazi mviringo – Bei ya soko imekaaje?
- Viazi vitamu – Zinalanguliwa vipi?
- Mpunga – Bei ya gunia au debe?
- Mchele – Aina ipi inauzika zaidi?
- Ngano – Bei ya kilo au gunia kwa sasa?
- Ulezi – Unapatikana kwa bei gani?
- Mtama – Bei yake imeshuka au imepanda?
- Alizeti – Wanaosaga mafuta hali ikoje?
- Karanga – Zinauzwa vipi kwa kilo?
- Korosho – Soko lake lipoje kwa msimu huu?
- Kunde – Zinalanguliwa vipi?
- Njugu mawe – Bei ya sasa ni kiasi gani?
- Miwa – Gunia au mzizi mmoja unauzwaje?
- Ndizi mbivu/mshale – Bei ya sokoni ni shilingi ngapi?