Tukatae, tukemee na tukomeshe tabia ya kuzoea vurugu

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
Tatizo la wananchi kujichukulia sheria mkononi sasa ni janga la taifa. Hali hii imeachwa kustawi, ikashamiri na sasa ni janga ambalo linamnyemelea kila mmoja wetu.
Hakuna aliyeko salama. Ukiacha magenge ambayo katika siku za hivi karibuni yamekuwa yanakodishwa, kutumwa na kutekeleza uhalifu kama wa kuteka watu, kuwaumiza na hata kuua, tabia ya wananchi kimakundi kujichukulia sheria mkononi nayo inazidi kuwa tishio la usalama nchini.

Jana vyombo vingi vya habari viliripoti matukio makubwa mawili ya wananchi kujichukulia sheria mkononi, mkoani Mbeya, katika wilaya ya Momba kwenye mji mdogo wa mpakani wa Tunduma, zilitokea vurugu kubwa zikihusisha mapambano yenye chimbuko na suala zima la uhalali wa uchinjaji wa kitoweo; jijini Dar es Salaam katika wilaya ya Kinondoni eneo la Kawe vurugu kubwa ziliripotiwa zikidaiwa kusababishwa na kuuawa kwa dereva wa bajaj anayedaiwa kuuawa kwa risasi na mwanajeshi. Kote hali imekuwa ni tete sana.

Hizi siyo vurugu za kwanza kutokea, kwanza kwenye mvutano juu watu wa imani gani wana haki ya kuchinja kitoweo na wapi hawana, hali kama hii mkoani Geita ilisababisha kifo cha mchungaji mmoja eneo la Buseresere, kisa mvutano wa uhalali wa kuchinja kitoweo baina ya Wakristo na Waislam. Suala hili limo ndani ya jamii na inavyoelekea halijapatiwa ufumbuzi wa kina na wa kimantiki ili kila upande utulie.

Ama kuhusu vurugu zinazoibuka kila mara juu ya matumizi ya barabara baina ya madereva pikipiki maarufu kama bodaboda na wakati mwingine bajaj, zimekuwa ni moja ya viashiria vikubwa sana nchini kwa sasa juu ya watu kutokutii sheria.

Tangu kuibuka kwa usarifi mpya wa bodaboda na bajaj nchini, pamoja na unafuu mkubwa wa usafiri ambao wananchi wanaupata hivyo kurahisisha utendaji kazi wao katika shughuli za kujitafutia kipato, umekuwa na changamoto kubwa mbili, usalama wake lakini pia utii wa sheria za usalama barabarani kwa madereva wote hao, yaani bajaj na pikipiki.

Kila mahali wao ndiwo wenye haki ya kutumia barabara. Kwao hakuna sheria zaidi ya wao kuwa na haki ya kuendesha, kupita upande wowote wa barabara, kwenye taa nyekundu, kujichomeka katikati ya magari, kwa kifupi kufanya kila aina ya vurugu na vituko barabarani.

Katika kuendesha vituko hivyo, ikitokea ajali yoyote, madereva wa pikipiki wamekuwa kama jeshi, wanaitana, wanavamia gari lililohusika kwenye ajali, wanamuadhibu dereva, wanaharibu gari na tumeshuhudia mara kadaa wamechoma moto magari, hata pale waliposhindwa kulichoma moto walilipopoa kwa mawe na kuhatarisha maisha ya walioko ndani na watumiaji wengine wa barabara.

Katika tukio la Kawe ingawa hadi sasa habari kamili hazijatolewa, taarifa za awali zinasema kwamba dereva wa bajaj aliyeuawa alipigwa na wanajeshi wanaodaiwa kumfuata wakidai kuwa walipoteza vitu walipopanda kwenye bajaj yake.

Vijana walikusanyika kutaka watu waliokuwa wamefikishwa polisi watolewe kwa nguvu ili kulipiza kisasi. Huu ni uvunjaji mwingine wa sheria tena wa kiwango cha juu kabisa, kuvamia kituo cha polisi!

Tunasikitika kwa kifo hiki, hakuna mwenye mamlaka ya kutoa uhai wa wa mtu mwingine hata kama ni kwa kushukiwa kosa gani, kimsingi hata hukumu za kifo zinapingwa kwamba ni kinyume cha haki za binadamu, kwa maana hiyo hatuungi mkono kitendo cha askari yeyote awe polisi au mwanajeshi kutumia nguvu zake au silaha yake dhidi ya raia kiasi cha kuua.

Tunalaani na kuomba hatua zichukuliwe dhidi ya wahusika wote haraka iwezekanavyo. Tunawapa pole wote walioguswa na maafa haya kwa njia moja au nyingine.

Hata hivyo, hofu yetu kama ambavyo tumebainisha hapo juu, ni kuzidi kujengeka kwa utamaduni wa kufanya vurugu nchini, utayari na uharaka wa watu kukusanyika kutenda uhalifu kwa sababu eti hawakufurajishwa na jambo fulani; ndicho kilitokea Tunduma na Kawe; ni uvunjifu wa amani kwa visingizio ambavyo havina mashiko.

Tabia ya madereva wa bodaboda na bajaj kuitana, kujikusanya na kutenda uhalifu kwa kisingizio chochote imeachwa ikachanua, ikaiimarisha na sasa imekuwa janga.

Kama taifa tunaweza kuwa hatuoni kuwa hali hii kuwa si tishio la usalama barabarani tu na kwa maana hiyo kutishia watumiaji wote wa barabara na vyombo vya usafiri, lakini pia katika picha pana zaidi tabia hii inajenga jeshi hatari ambalo siyo rasmi katika kuvunja sheria na kuendelea harakati za kurejesha taifa hili katika sheria za mwituni, mwenye nguvu mpishe!

Tunasema kama tunataka kusaidia nchi hii, ni lazima nguvu kubwa ielekezwe kwa maderava wa bodaboda na bajaj kujenga tabia ya kuheshimu sheria, kuzitii bila kisingizio chochote vinginevyo tujiandae kwa maafa makubwa zaidi huko tuendako.




CHANZO: NIPASHE

 
Tabia ya madereva wa bodaboda na bajaj kuitana, kujikusanya na kutenda uhalifu kwa kisingizio chochote imeachwa ikachanua, ikaiimarisha na sasa imekuwa janga.

wengi wao wana kazi mbilimbili ikiwemo uporaji usiku kwahiyo abiria wao wakae chonjo. Kuna mmoja juzi alimbaka mke wa mtu kwa kumtishia kisu baada ya kumpakia kama mteja!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…