Tukemee vimelea vya ukatili, kabla hatujaingia katika majuto

Tukemee vimelea vya ukatili, kabla hatujaingia katika majuto

Joined
Nov 6, 2016
Posts
77
Reaction score
271
TUNALOJUKUMU LA KUDHIBITI HALI YA UKATILI NA UNYAMA UNAOJENGEKA KATIKA WENZETU

Na Comrade Ally Maftah

Nilipata kusikia tukio la dada aliyefanyiwa ukatili wa kijinsia nikajidhibiti sana nisitazame tukio hilo, ila kwa bahati mbaya sana nimeona kipande kidogo cha tukio lile.

Tukio limenitafakarisha mno nimejiuliza maswali mengi sana baada ya kuona tukio lile.

1. Nimemwona mwathirika akiomba radhi na kusema hatorudia tena, lakini jamaa walikosa utu kabisa, hawakuguswa kabisa na msamaha aloomba mwathirika.
2. Kuna sauti inaashiria watendaji wa jambo ni watumishi wa uma, ambao wanalipwa kwa kodi zetu.
3. Uungwana na ustaarabu wa mwafrika ulipotea kabisa, utendaji wa uhalifu pamoja na uchukuaji wa video haikuwa taratibu za tamaduni zetu, tendo lililofanyika haliweze kutendwa na mtu mwenye hekima, na mtu asingeweza kurecord tukio lile, unamuumiza mtu na unamdhalilisha.

Sisi wazalendo tuchukue hatua za kudhibiti ukatili unaojionyesha kwa watoto wetu angali wadogo, tuwafundishe watoto wetu kuheshimu wanawake, tuwakanye kuhusu kulipiza kisasi, tuwafundishe kuhusu kusamehwme.

Mfano mzuri wa binadamu aliyekamilika tunauona kwa Dr Samia, anatufundisha kwa vitendo kuhusu kusamehe, kuridhiana, kujadiliana na kupendana.

Nafikiri chanzo cha tukio kinatokana na kutokuwa na uvumilivu, kuwa na kiwango kikubwa cha chuki na kulipiza kisasi, kama wale vijana walitumwa na mwanamke kwa wivu wa mapenzi basi somo kuhusu uvumilivu, kusamehe, kuridhiana na kukubali uhalisia litiliwe mkazo, kama kuna hali ya matatizo kwenye ndoa ni bora tuzungumze, tukishindwa tuvishirikishe vyombo mbalimbali vya kuleta maridhiano, kama BAKWATA, taasisi za usuluhishi na maridhiano, na mabaraza mengine ya kidini.

Upande wa pili ndugu zetu watumishi wa umma, tunawaomba mzidishe upendo kwetu mkumbuke nyinyi mpo hapo kwa ajili ya kutuhudumia na si kutuumiza, sisi tunawapenda sana, ila kuna wenzenu wanashindwa kutoa huduma sahihi.

Mwisho nitoe pongezi kubwa sana kwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es Salaam, kwa sisi tulokuwa kwenye uwanja wa Taifa tumeshuhudia hali ya utulivu na amani pamoja na idadi kubwa ya washabiki wa mpira wa miguu, tukamkanda mtani goli moja kila mtu akalala unono

NDIMI
Comrade Ally Maftah
PAKOME WA MCHONGO
Comrade Wa Yanga

IMG-20240809-WA0040.jpg
 
Nchi imeozaaa Yale ya wewe unanijua Mimi ni nani yamerudi kwa kasi ya 5G Tatizo wanalindana viongozi wajuu wakiwa na jambo lao kama la Mikataba mibovu ya kuchuuza rasilimaliJW wanawalinda JW nao wakifanya lao la hovyo wanalindwa na mfumo kuwakumbusha serikali tunatakiwa kulindana kula keki ya taifa
 
Hivi huyo aliyewatuma naye wamemkamata?????

Ova
 
Back
Top Bottom