Unalolizungumzia ni kweli kabisa ndugu, hili tatizo la misamiati ya kifundi ni kubwa sana. Kila nyanja ya teknolojia ina istilahi yake maalum. Kama teknolojia hiyo haikuwahi kutumika au kufahamika huku kwetu, inakuwa ngumu sana kuiweka kwenye lugha yetu ya Kiswahili. Wataalamu wetu inabidi waumize vichwa kutafuta msamiati unaofaa kuzungumzia hii teknolojia mpya. Katika kufanya hivyo, mimi nadhani wataalamu wanajiuliza maswali yafuatayo:
1. Je teknolojia hii ishawahi kutumiwa katika utamaduni wa jumuiya yoyote ya nchini kwetu? Kama ni ndiyo, je neno gani linafaa kutumiwa kwenye dhana inayohitajika? Kwa njia hii ndio maana tulipata maneno ya asili 'bunge' na 'ikulu'(maneno ya kisukuma) kuelezea dhana mpya za 'parliament' na 'state house'
2.Je, hilo neno jipya linaweza kuingizwa kama lilivyo kwenye mfumo wa lugha yetu?(Rejea neno 'camp' lilivyobadilishwa na kuwa 'kambi' ' man-of-war' kuwa 'manowari' etc)
3. Je, kuna uwezekano wa kutohoa neno jipya?
Ujio wa sayansi ya kompyuta na television ndo umetuvuruga vibaya sana katika kupata maneno yetu ya kiswahili. Uwanja wa misamiati ya Kiswahili umepanuka sana hapa Afrika ya Mashariki kwa sababu Kenya na Tanzania kila mmoja ana baraza lake la kiswahili. Wakenya walileta neno 'runinga' kuzungumzia television, Tanzania wakaanza na neno 'kiona-mbali' lakini baadaye likaachwa, na kubakiwa na hilihilo la 'runinga'
Ni katika kujibu namba 1-3 ndio tumejiundia maneno mengi ya kitaalamu tuliyo nayo.
Ni kazi kubwa ndugu yangu: usiibeze wala kuishutumu!
mkuu nashkuru kwa maelezo yako,.tatizo la watungaji wa lugha ya kiswahili wako top down approach, hawaweki uzito, kama sisi watumiaji tunaelewa ama tunatumia wakitoacho katika maisha yetu ya kila siku. ukichunguza pia utagundua walioko kwenye haya mabaraza ni wazee sana(watu wazima) ambao hawajichanganyi na jamii vyakutosha na lugha yao mara zote ni ile ya magazeti makini na ripoti za serikali.
pia tunahaja yakutambua uwepo wa kiswanglish kwani ndio lugha inayopata nguvu east afrika na maeneo ya kazi, kama ambavyo tulichakachua kingereza na kuweka maneno ya kiswahili, nimeona kwenye literature mbalimbali na oxford dictionary maneno kama shamba, panga, ugali n.k yakitumika kama ni sehemu ya maneno halali ya kiingereza cha afrika mashariki. ni ajabu kuona tunauwezo wa kuchakachua lugha za wengine lakini ya kwetu inatupa shida. mambo ya kuperuzi lugha za kiarabu na kuita ni kiswahili sanifu yanatupeleka mbali na watumiaji wa lugha.
wasanii na wanamuziki wa east afrika maranyingi wanatumia kiswanglish na wale ndio wasambazaji wa kubwa wa kiswahili katika jamii. mfano tukianza kutafuta jina la yahoo na google kwa kiswahili, baadae bing, opera, . uzoefu unanionyesha watatunga tuu lakini sisi hatukitumii kabisa mitaani tunamoishi na wanafanya maisha magumu kwa wanafunzi wanaosomea kiswahili kwa kukremu mambo mengi complicated.
mfano ;chukulia umekwenda dukani ukamwambia muuza duka nipatie rununu, ama nipatie ngamizi ya kupakata atakuelewa???definitely atakuona wewe mteja wako ni psychopath
umegusia swala la kutumia lugha za wasukuma n.k. lugha za makabila zinaisha na kuchakaa,
tukiangalia vitabu vya dini siku hizi wanaweka kiswahili cha kisasa, hivyo tunahaja yakutambua lugha inapitia mabadiliko na sio kuanza kuchimbua makabila na kutafuta walisemaje zamani. ustaarabu wa lugha ni pale unapoheshimu utamaduni wa mwenzake na kuruhusu mwingiliano. mfano neno Volt ni la kifaransa lakini waingereza wamelikubali na wanalitumia pia.