Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,655
[h=2]
Tukibadili Fikra tutabadili mwelekeo wa Taifa letu kwenye Tija[/h]
Kizazi chetu kinakabiliwa na changamoto nyingi sana kama Taifa. Tumerithi taifa ambalo limegawanyika na lisilokuwa na malengo ya pamoja wala maono. Kiwango cha uzalendo wa watu wetu kimeshuka mno katika hali ya kuogopesha na kunifanya nijiulize ni wapi tunaelekea? Pengine hili ni swali ambalo kila raia aliyekomaa kifikra anapaswa kujiuliza, Kila raia anayewajibika kwa jamii yake na kwa Taifa lake anapaswa kujiuliza swali hili. Ni nini mwelekeo wetu kama Taifa? Ni nini matumaini yetu? Sisi tunaoishi sasa hivi tuna wajibu wa kutengeneza mazingira bora kwa vizazi vyetu vijavyo. Tuna wajibika kupokeza Taifa hili likiwa moja na lenye amani kwa kizazi kingine. Tunawajibika kupokeza Taifa hili likiwa lenye watu wenye mashirikiano. Ni sisi tutakaolijenga Taifa hili kuwa Taifa bora au baya kwa akili zetu na jitihada zetu.
Lakini ni lazima kwanza tuwe na akili za utaifa. Ni lazima tujue kujitolea kwa Taifa hili. Ni lazima tutambue kila raia wa Taifa hili ana wajibika kwa Taifa lake, kwa jamii yake na kwa familia yake vitu hivi vitatu ni lazima vizingatiwe. Hatutaweza kubomoa kimoja kwa faida ya kingine. Haki zetu zote na maendeleo yetu tunayapata katika Taifa hili. Hapa ndipo nyumbani kwetu hatuna nchi nyingine.
Wito wangu kwa watu wa Taifa hili ni kufikiria upya kuhusu mwelekeo wa Taifa hili. Kufikiria upya kuhusu baadae yetu. Ni lazima tufuate njia iliyo salama ili Taifa hili liendelee kuwepo. Njia ya ushirikiano umoja na uzalendo. Njia tuliyoichagua kwa sasa kama mapito yetu haitotufikisha popote. Hatutaweza kujenga Taifa hili katika ubinafsi. Hatutaweza kujenga Taifa hili katika fikra za ubinafsi. Ni lazima tujenge Taifa hili katika misingi ya fikra sahihi zinazojali baadae ya watoto wetu na ukuaji wa Taifa letu.
Taifa hili linahitaji uongozi na dira. Linahitaji atayeleta upya uzalendo na kuamsha roho ya kulitumikia Taifa hili kwa watu wote. Hii ni muhimu sana hatutaweza kulijenga Taifa hili bila kujitolea kwa watu wetu ili kuona Taifa hili likiendelea. Ni muhimu kuacha fikra hizi za ubinafsi na kuangalia utaifa zaidi. Haya mambo ni muhimu sana ili kujenga Taifa hili. Kama kila mtu akijiangalia mwenyewe hatutaweza kujenga Taifa hili. Tunahitaji kurudisha hii roho kwa watu wetu. Lakini hili halitowezekana pasipo uongozi wenye uadilifu na wenye dhamira ya dhati ya kuleta maendeleo kwa watu wetu. Fikra za watu wetu ni lazima zibadilike ni hatua ya kwanza ya maendeleo yetu kama watu wetu wakibadili fikra zao za ubinafsi na kutambua tumekua Taifa ili tushirikiane. Kuendelea kwetu kutategemea sana umoja wetu na kujitolea kwetu kwa Taifa.
Ni muhimu tukajipanga sasa na kujenga nidhamu na uwajibikaji kwa watu wetu. Kwakuwa bila nidhamu hatutaweza kujenga chochote. Baadae ya Taifa hili inategemea sana busara zetu na maamuzi yetu. Kama tukijipanga maendeleo yetu yatakuja haraka zaidi ya tunavyotarajia. Hili ni jambo la muhimu sana kuzingatia. Ubora wa Taifa lolote unategemea sana ubora wa fikra za watu wanaojenga Taifa hilo. Ili Taifa hili liendelee lazima tuwe wamoja na tujipange. Tunapufikiria kuhusu mimi na familia tufikirie pia kuhusu Taifa na jamii. Ni lazima tukubali hatuwajibiki ipasavyo kwa jamii na kwa Taifa letu. Ni lazima tujitambue sasa kama Taifa, wakati ndio huu wa kuleta fikra zetu pamoja ili kuleta mapinduzi. Ufisadi unaturudisha nyuma kama Taifa ni lazima tuongelee madhara yake kwakuwa umemea sio kwa viongozi tu hadi kwa raia wengi na ili tulete maendeleo ni lazima tubadili fikra hizi za hatari.
Tunajua kwa uzoefu ufisadi na ubinafsi huleta vurugu na fujo katika jamii na matokeo yake sio mazuri. Na pia ni kikwazo kwa maendeleo ya nchi na haki za watu. Huleta pia disorder katika jamii na kufanya nchi isitawalike. Ni muhimu kubadilika sasa kwa faida ya kizazi kijacho na usalama wa nchi. Mambo haya ni muhimu sana. Ni lazima turudishe akili za watu wetu katika Utaifa na katika uzalendo ndani ya familia katika jamii na katika Taifa. Ni lazima tubadilishe fikra zetu ili tubadilishe mwelekeo wa Taifa letu. Pasipo uzalendo hakuna kiongozi atakayefanya jambo kwa faida ya UMMA. Aina hii ya fikra lazima ibadilike kutoka chini kabisa kama tunahitaji mapinduzi katika Taifa hili. Viongozi wanatoka katika jamii ili tubadilishe Taifa lazima tubadilishe mentality ya jamii. Lazima Elimu ya uraia itolewe juu ya Utaifa na uzalendo na umuhimu wa mtu kuishi katika Taifa. Ni lazima uwepo ushawishi wa kuwafanya wengi wa watumishi wetu wa UMMA kuirudia mioyo yao na kufanya kazi kwa faida ya Taifa. Haya ni mambo ambayo mwanasiasa yeyote makini ni lazima ayaone kwa mustakabali wa Taifa hili. Ni lazima turudishe tumaini hili kwa Taifa. Ni lazima turudishe tumaini hili kwa nguvu kazi yetu yote. Ni lazima turudishe uzalendo na uwajibikaji kwa Taifa.
Watu wa Taifa hili lazima wahisi utaifa wao na dani ya roho zao na wawe tayari kulitumikia. Sisi ni watu wamoja. Majaliwa yetu ni mamoja kama Taifa. Naamini kama tukiji organize kwa pamoja kukabiliana na matatizo yanayotukabili kama Taifa bila ya ubinfasi tutafika. Ni lazima tujue ni wapi tunataka kwenda kama Taifa. Ni nini azma yetu na malengo yetu. Taifa hili halijazaliwa kusudi liwe ombaomba, tuna nafasi ya kukua kama tukilipenda na kulitumikia Taifa hili.
Tunapozungumzia mabadiliko ni pamoja na kulipenda Taifa hili, kupenda Raia wenzako kwa moyo wote na kuwa Tayari kuwatumikia. Ukweli ni kwamba hatujawa Taifa kusudi tunyonyane au kundi moja likandamize kundi jingine. Tumekuwa Taifa ili tufikie kilelele fulani cha mafanikio na ndio hasa itakayo kuwa sababu ya furaha yetu kama Taifa. Mafanikio yetu ya pamoja iwe ndio furaha yetu. Lazima tukumbuke tunawajibu kwa vizazi vijavyo, ni sisi tunaotengeneza baadae ya vizazi vyetu. Lazima tuvipende vizazi vyetu ambavyo havijazaliwa kwa kuwatengenezea mazingira bora kwa kufanya kazi kwa bidii na kwa kupendana kama raia wa Taifa hili. Tumaini hili lazima lizame katika mioyo yetu. Lazima tujue tunapotaka kwenda kama Taifa.
Ukweli ni kwamba , hatutaweza kulijenga Taifa hili pasipo kulipenda kwanza. Ni lazima tulipende kwanza ndipo tutakapo litumikia kwa mioyo yetu yote. Tujenge Taifa ambalo Raia wanaheshimiana kwa dhati na kushirikiana katika ujenzi wa Taifa lao na viongozi wakitenda Haki na kuwajibika. Hili ndilo Taifa ninalo lihitaji ambalo wanawake na wanaume wanashirikiana na kuheshiamiana katika ujenzi wa Taifa lao, ambalo wazazi wanawajibika kwa pamoja katika malezi ya watoto. Hatujawa Taifa kusudi kila mmoja ajiangalie mwenyewe, tunawajibu kwa kila mmoja wetu.. Tunachohitaji ni Taifa hili kusonga mbele kwa nguvu ya umoja wetu. Sisi ni Watanzania na ni lazima tuungane pamoja ili tupambane na matatizo yanayotukabili sasa hivi, ili tupambane na uovu unaolikabili Taifa hili.
Tuna changamoto za rushwa, uzembe na kutokuwajibika kwa watu waliopewa dhamana. Wakati wa kutawaliwa kama waafrika na kama watu weusi ni lazima uishe kwa kuamua sasa na kwa dhati kuwa wamoja na kutia juhudi katika kujikomboa. Nina amini kwa dhati kabisa tunauwezo wa kuwa Taifa kubwa kama mataifa mengine. Ni jitihada zetu na kujitolea kwetu na dhamira yetu isiyififia ya kuleta mabadiliko. Ya kuona maisha ya mwafrika na mtanzania yakibadilika. Natumaini siku moja kuona WANAUME KWA WANAWAKE WAKIJITOLEA KWA DHATI KULITUMIKIA TAIFA HILI. Mabadiliko haya lazima yaje na yaonekane. Kwa juhudi za pamoja ni lazima tutashinda kama tumedhamiria kwa pamoja kukusanya nguvu zetu na uwezo wetu wa kiakili. Watanzania tuna uwezo wa kuwa Taifa kubwa.
Nafikiri tofauti kuhusu Taifa hili. Naliona katika macho ya uwezekano. Taifa hili linauwezo wa kuwa kitu chochote linachotaka ni juhudi zetu na umoja wetu na jitihada zetu zisi zisizofifia.
Katika kizazi chetu leo hii tuna viongozi wanaogawa watu na kuondoa umoja wetu ambao ni nguvu yetu ya kuleta maendeleo. Uchu na ubinafsi umetamalaki. Wajibu wetu wa dhati kwa kila mmoja wetu ni kuliona Taifa hili likisonga mbele ni kuona Taifa hili likisonga mbele na kuliletea heshima yake.. Vijana wa Taifa hili ambao tunaishi sasa tunawajibu huu, majaliwa ya taifa hili yanatutegemea sisi ni lazima tuwe Taifa lenye malengo. Ni lazima tuwe taifa lenye ushawishi na nguvu. Ni lazima vijana tujikusanye tufanye mapinduzi haya kwa faida ya Taifa na heshima yetu na vizazi vyetu vingi vijavyo.. Hili ni lazima tulidhamirie. We must have a fighting spirit. The spirit of those who conquer and not conquered. Ili tuwahadidhie watoto wetu jitihada zetu na mafanikio yetu tuliyoyaleta kwa Taifa letu, lazima tuwe na kitu cha kuwaelezea vizazi vyetu vijavyo ni nini tumefanya kwa Taifa letu. Ni lazima tuwe Taifa la washindi.. lazima tuwe wamoja.
MABADILIKO YA KWELI YATAKUJA KAMA TUKIWA WAMOJA NA KAMA TUKIBADILI MITAZAMO YETU KUHUSU TAIFA LETU. WATOTO WETU NI LAZIMA WALIPENDE TAIFA HILI KAMA WANAVYOJIPENDA WENYEWE.. TUMAINI LANGU HALITOFIFIA KWA WATU WA TAIFA HILI NA BAADAE YETU. UPENDO WANGU UENDE KWA WATANZANIA WOTE NA UJUMBE HUU WA MATUMAINI KWA BAADE YETU.