Tanzania ni nchi yenye eneo kubwa sana kulinganisha na nchi nyingi afrika na duniani lakini ni nchi
ambayo inatumia sehemu ndogo sana yae neo lake kwaajili ya kilimo cha chakula na kibiashara.
Kutokana na taarifa ya (Global yield Gap atlas) asilimia 46 ya eneo la Tanzania lina rutuba na linafaa
kwajili ya kilimo cha mazao mbalimbali, lakini asilimia 23 tuu ya eneo lenye rutuba ndilo linalolimwa
kwa sasa na asilimia 77 ya eneo lenye rutuba halijatumika bado kwa kilimo chochote.
Nchi ya Tanzania bado inategemea sana kwa kiwango kikubwa baadhi ya mazao au mazalisho yatokanayo na mazao kutoka nchi za nje. Kwa mfano;
Kwa mwaka 2020 tanzania ilikuwa na uhitaji wa tani za ujazo 570,000 (laki tano na sabini) za mafuta ya kula, huku uzalishaji wa ndani ya nchi ukiwa tani za ujazo 250,000 (Laki mbili na hamsini) za mafuta tu.
Kutokana na upungufu huu Tanzania inatumia kwa mwaka takriban shilingi bilioni 443 za Kitanzania kwa ajili ya kuagiza mafuta kutoka nje ya nchi ambapo kwa kutumia hizo fedha au pungufu zaidi tunaweza kuhamasisha na kuwekeza katika kilimo cha alizeti katika mikoa kama Dodoma, Singida na sehemu za Mbeya katika kuzalisha mafuta ya kula, pia kilimo cha michikichi katika mkoa kama Kigoma ambapo ikisimamiwa vizuri kwa kilimo cha kisasa bila kutegemea sana mvua tunaweza kuzalisha tani za kutosha ambazo pia tunaweza kulisha na nchi za jirani. Uimarishaji sera za kilimo katika zao la michikichi na alizeti pia mafuta ya karanga kutaleta tija na manufaa makubwa sana ya kiuchumi katika nchi ya Tanzania.
Pia zao kama ngano uhitaji wake katika nchi ni mkubwa sana na uhaba ni mkubwa kutokana na uzalishaji pungufu.
Kwa mfano;
Kutokana na (IPP Media) mwaka 2020 Tanzania ilizalisha takriban tani 100,000(Laki moja) za ngano, huku mahitaji ya nchi kwa mwaka yakiwa takriban tani milioni moja (1,000,000) za ngano.
Hivyo Tanzania inakuwa na upungufu wa takriban tani laki tisa za tani ya ngano, kulingana na upungufu huo Tanzania imekuwa ikiagiza tani 900,000 huku ikitumia bilioni za fedha kwa mwaka mmoja.
Kama nchi na wadau wa kilimo wangeweka nguvu katika zao hili nchi ingekuwa katika nafasi nzuri sana ya kiuchumi kwa taasisi ya TARI wamefanya utafiti na kugundua kuwa kuna maeneo makubwa sana nchini yanayokubali kilimo cha ngano, hasa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini kama Mbeya, Songwe na Njombe.
Kwa kuboresha mifumo ya kilimo cha ngano na kuhamasisha wadau na wakulima mbalimbali nchini kilimo cha ngano kinaweza kuwa chanzo kikubwa sana cha uchumi wa nchi ya Tanzania .
Kwa mfano kwa muda sana nchi ya Tanzania imekuwa ikiagiza ngano kutoka nchi ya Ukraine, mwanzoni mwa mwaka 2022 nchi ya Ukraine imekuwa ikikumbwa na vita dhidi ya Urusi mbayo vita hiyo inaendelea hadi sasa. Kutokana na changamoto hiyo kumekuwa na uhitaji mkubwa na uhaba pia wa ngano nchini na hii kupelekea bei za unga wa ngano kuongezeka mara mbili zaidi ya bei ya mwanzoni ambapo adha hii imepelekea bidhaa zote zitokanazo na ngano kuongezeka bei sana na hii kumwathiri Mtanzania mmoja mmoja na uchumi wa nchi kwa ujumla. Hivyo ni vyema kuwa na sera na maono ya kuhakikisha nchi inazalisha ngano ya kutosha bila kutegemea nchi za nje.
Hayo ni baadhi tuu ya mazao mawili ambayo uzalishaji wake ni mdogo nchini na hii kupelekea uhitaji kutoka nje ya nchi yapo mengine mengi ambayo uzalishaji wake hautoshelezi nchini kama katani, pamba, kahawa na chai.
Pia nchi ya Tanzania imeweza kutumia vizuri ardhi yake katika kuzalisha baadhi ya mazao mbayo kama nchi inajitosheleza na kuweza kuuza nje ya nchi pia mfano;
Kulingana na Kilimo Forum takwimu za mwaka 2020 Tanzania ilizalisha takriban tani milioni 2.2 za mchele ambayo ni sawa na asilimia 33 ya mchele wote unaozalishwa katika nchi za Afrika ya Mashariki.
Kwa mikoa ya Nyanda zaJuu Kusini imekuwa wazalishaji wakuu wa zao la mpunga na mikoa ya Shinyanga na Tabora pia. Hii imepelekewa na uhamasishaji mkubwa wa kilimo cha mpunga kutoka kulima kwa ajili ya chakula tu mpaka kulima kibiashara ambayo hii imesaidiwa na sera nzuri na elimu juu ya kilimo cha mpunga. Nguvu hii pia tunaihitaji katika kilimo cha alizeti na ngano.
Je, tunaweza kama nchi kuimarisha kilimo bora na chenye tija kwa wananchi na nchi kwa ujumla, Kwa kuboresha na kuimarisha sera za kilimo, hii inajumuisha kilimo cha mkakati hasa kwa yale mazao ambayo bado kwa asilimia kubwa tumekuwa tukitegemea kutoka nje ya nchi na taasisi kama TARI kuimarisha utafiti wake nchi nzima ili kuweza kupata uhakika wa kilimo chetu kilicho bora na cha kisasa chenye kuleta mazao yenye hadhi ya kimataifa.
Kutoa elimu juu ya kilimo cha mazao ya kibiashara yenye tija kidunia, mfano kilimo cha mkonge ambacho kinazalishwa kwa kiwango kidogo sana nchini kimedorora kwasababu ya elimu duni juu ya kilimo hichi nchini, ambapo kampuni binafsi chini ya muwekezaji mkubwa nchini Mohamed Dewji wameweza kujikita katika kilimo hicho na hii kuipelekea kampuni hiyo kuwa katika nafasi nzuri kidunia katika uzalishaji wa zao hilo kwasababu wali thubutu na kuwekeza katika muda na fedha kwa miaka kadhaa
Hivyo basi ni vyema kama nchi kuzingatia mambo hayo na mengineyo ili kuendelea kijiimarisha katika sekta ya kilimo na uchumi wake na uhitaji wa watanzania kwa ujumla.

Upvote
4