kaligopelelo
JF-Expert Member
- Jun 20, 2013
- 2,832
- 4,070
Habarini za asubuhi.
Wakuu kwa juhudi tunazofanya kupigania uhai wetu,ni dhahiri shida huongeza maarifa.
Ukija kuangalia ugonjwa wa covid-19 kwa sura yake na namna ulivyoondoka na uhai wa watu wengi kwa muda mfupi.
Na pia kwa namna ambayo tulikuwa tunatabiliwa mazito hasa waafrika na wale wenye ngozi nyeupe wanaoishi ulaya na amerika. Kuwa huenda dunia ikashuhudia waafrika wakipukutika Kama kuku wanaougua homa ya mdondo. Lakini kinachoendelea mpaka sasa nadhani kinastaajabisha,mi niseme tu mola wetu mlezi anatupigania.
Harakati zetu zikazaa matunda kwa nchi ya Madagascar ambao kwa utafiti wao wamefanikiwa kugundua dawa ya mitishamba inatengenezwa kutokana na mti unaoitwa ARTEMISIA. Na dawa hiyo wakaiita jina la covid organic.
Covid organic umefanikiwa kuponya watu kadhaa Madagascar hatakama WHO hawataki kuitambua dawa kuwa inaweza kutibu Covid-19.
Harakati hizo za kupambana kuhakikisha tunaokoa uhai wetu na wa familia zetu zikapelekea kugundua kile tunachokiita kumuwahi mdudu kabla hajaweka makazi. Tukaja na mbinu ya kujifukiza. Bila shaka kupitia mbinu hii pia Kuna natija inayopatikana, hasa kwa watu wengi ambao walikutwa na tatizo, na wengine ambao walijihisi kuwa ni wagonjwa kupata ahueni baada ya kupiga nyungu.
Bila ya shaka ugunduzi zaidi unaweza ukaendelea na watu watakuja kubaini dawa maridhawa ya kuponesha korona moja kwa moja.
Hivyo nilikuwa ninaomba kwa juhudi hizo tulizozifanya kwa covid-19 tuhamishie kwa VIRUSI VYA ukimwi navyo ibaki stori. Tuache kuwasubiri wazungu kuwa ndio tegemeo letu,na badala yake tutumie akili zetu ma rasilimali zetu katika ubunifu na ugunduzi.