Tukikubaliana na dhana za kuikejeli elimu kisa Profesa Muhongo kakejeliwa tutapotea kama Taifa

Wabunge wakiwa bungeni wanajiona kuwa wako sawa katika kila kitu. Tofauti zao (ikiwemo elimu) huachwa getini. Ndiyo maana hoja zao huwa zinaungwa mkono kwa kishindo. Endapo mmoja hutaka kwenda tofauti hupondwa kwa kudharauliwa, kuzodolewa na kuzomewa kwa nguvu zote!
by the way huyu mheshimiwa si ndiye yule aliyetua uwanja Sheikh Amri Abeid pale Arusha kwa mbwembwe nyingi akiwa na helicopter yake 2015 au majina yafanana?!!!
 
Kuna msemo kuwa if it quacks like a duck then it is the duck yaani: kama analia kama bata basi ni bata.

Jifunze kutofautisha kukaa muda mrefu darasani na kuelimika. Je mtu ambaye hafahamu background yako yaani hana idea kama uliwahi kusoma hadi kupata shahada, akiona hoja au matendo yako anaweza kupata hisia kuwa wewe ni msomi? usomi wako inatakiwa ujitee wenyewe na sio wewe utumie nguvu kubwa kusema kuwa wewe ni msomi.

Bill Gate hakumaliza chuo kikuu lakini ugunduzi wake ndio unaoifanya dunia iwe kijiji; Diamond hakusoma lakini mafanikio yake tena yaliyotokana na ubunifu (sio kuokota jiwe la thamani) umeiletea nchi mapato, ajira hivyo ukuequate ufahamu wake ni level ya Master' s degree au zaidi .

Mtu anapoajili wasomi baada ya kufanikiwa kwanza ni kutokana na sheria mbalimbali kuhitaji watu waliosomea utaalamu fulani ndio wafanye taaluma fulani hivyo ni lazima wataajili wataalamu. Pili hatusemi kuwa elimu haina mchango katika maendeleo ya mwanadamu au kuyafanya maisha yawe bora zaidi la hasha. Msukuma anachosema elimu sio cheti ni ujuzi na output. Je vinalinganalingana?

Kwa nini watu wanatunukiwa PhD za heshima na vyuo vikuu duniani kote? Ni kwakutambua mchango mkubwa walioutoa katika nyanja fulani.

Nikuulize swali katika lugha rahisi: Kuna msomi mtanzania anajua kugeuza mchanga/udongo kuwa machine? Na kama ukimkuta anajua basi ameonyeshwa na mzungu namna ya kufanya na yeye anakopi tu.
 
Nakubaliana na hoja yako ya ubunifu kuwa na faida unapotumika vizuri. Nachokiona kwa Msukuma ni aina fulani ya hoja ambazo zinaifanya elimu ionekane kama vile haina umuhimu.

Kwamba kama wasomi wenye ndio hawa basi hiyo elimu ya hadhi ya juu haina tofauti na sisi wa darasa la saba. Anajenga taswira mbaya kuhusiana na elimu wakati ndio silaha inayowatofautisha watu wa mataifa ya dunia ya kwanza na sisi wa dunia ya tatu.

Anakuwa kama anajifariji kwa kuwa na mafanikio akiwa ni mtu wa elimu ndogo akisahau kuwa ni wachache wenye kuweza kufanikiwa pasipo maarifa mengi yenye uhusiano wa moja kwa moja na elimu.

Hata hao mabilionea ambao wanasifika kwa kupata pesa bila ya kumaliza vyuo vikuu, wametajirika kwa ushirikiano wa moja kwa moja wanaoupata kutoka kwa wataalam wenye elimu ya sekta zilizowatajirisha.

Huyo Diamond asingedumu kwa miaka mingi akiwa na pato kubwa kama sio mikakati na mipango yenye msingi wa elimu kutoka kwa wasaidizi wake aliowaajiri.
 
Nashukuru kwa hoja yako nzuri, nami niongezee (supplement) kidogo kwenye hoja yangu.

Elimu ikitumika vizuri ina mchango mkubwa sana katika kuyafanya maisha ya mwanadamu yawe bora.

Hii dunia ya kwanza na ya tatu zina tofauti kubwa sana ya maendeleo, lakini kuna wakati dunia nzima ilifanana kwa maana yote ilikuwa ni mapori, milima, mabonde, jangwa bila kitu chichote, lakini nguvu ya elimu ndio imeifanya iwe tofauti kiasi kwamba unaweza dhani iliumbwa vipindi tofauti kumbe yote iliumbwa kwa siku saba tu.
 
Phillipo Bukililo ,

..ukifuatilia HISTORIA ya siasa za Tz utaona kwamba wanasiasa wetu huwa hawashindani kwa hoja bali kwa propaganda na kuchafuana.

..naweza kukurudisha miaka ya nyuma mpaka wakati wa Nyerere vs Kambona kuhusu azimio la Arusha na siasa ya Ujamaa.

..looking back unapata hisia kwamba muda mwingi ulitumika ktk propaganda dhidi ya ubepari kuliko kuelimishana kuhusu uzuri na manufaa ya ujamaa.

..hata wakati wa suala la Aboud Jumbe na madai ya serikali tatu hali ilikuwa hivyohivyo ambapo tulimezeshwa hoja za upande mmoja tu, na hoja hizo zilichanganywa na propaganda nyingi.

..Naweza kuongeza mifano mingi zaidi lakini nitakuwa nakuchosha.

..kwa mtizamo wangu nadhani Watanzania hatuna utamaduni wa kushindanisha hoja. Tumezoea kuchafuana na kuzushiana.

..Tangu taifa letu lilipoasisiwa maamuzi makubwa yamekuwa yakifanyika kwa kutumia propaganda badala ya majadiliano ya kina na kisomi.

..Tukirudi kwa Msukuma vs Prof.Muhongo, nahisi kwamba kuna watu wako nyuma ya mashambulizi aliyoyatoa Msukuma. Prof alikuwa anaishauri serikali, it does not make any sense kwa mbunge mwenzake kuanza kumshambulia.
 
Yeye kuwa tajiri asiye na elimu zaidi ya ile ya darasa la saba sio sifa kama anavyodhani. Wapo watu wengi tu wanaoshindwa kufika popote kimaisha sababu ya elimu zao ndogo.
Ila pia wapo watu wengi wenye elimu kubwa ambao hawajafika popote kimaisha
 
Sahihi mkuu
 
Maadui wakuu wa taifa:
(1) Ujinga
(2)Umasikini na
(3)Maradhi.
Adui namba moja hapo juu ndo anamsibu Mh. Msukuma. Pia hakana staha kale kajamaa ni ka kupuuza tu.
Jamaa huyu kiburi kimeanza kupungua baada ya mjomba kusafiri maana kila kitu alikuwa anasema kaagizwa na mjomba katutesa mno huko kwetu, alafu akiwa anakuja jimboni kwake anakodi magari ya msafara mara gari la kingora, walinzi boardguard utazani ni msafara wa Raisi, kwenye kikao anaacha magari yote yananguruma yanachoma mafuta mpaka muda wa kikao kitakapoisha, uwa nacheka tu kwa ufupi uwa anatamani nafasi za wasomi lkn hanakosa sifa ya kuwa pale
 
Mkuu we kweli tindo , well narrated bro
 
Hawa wakina muhongo wapigaji tu na ndiko tunakoelekea Mungu atuepushe jamani
 
Kosa la mhongo ni kusema hydro electric ni umeme uliopitwa na muda, kwamba Dunia imeachana na maji siku nyingi wako kwenye gas tu.

Hapo ndio kosa la mhongo lilipo na ameonyesha wazi kabisa kua ana masilahi binafsi na gesi na makampuni yanayouza mitambo ya kuzalisha umeme wa gesi.

Production mix mimi nakubaliana nae kabisa ila kuponda maji huo ndio utaahira wa muhongo aliouonyesha.
 
Yeye kuwa tajiri asiye na elimu zaidi ya ile ya darasa la saba sio sifa kama anavyodhani. Wapo watu wengi tu wanaoshindwa kufika popote kimaisha sababu ya elimu zao ndogo
Msukuma ana utajiri gani wa kuweza kusema mbele ya watu? Huyu ni mtu ambae kila siku anakwepa kulipa kodi na ndio maana anatumia ubunge wake kuwatisha maofisa wa TRA wasimthibiti. Mimi nina ushahidi wa kumuonesha huyu msukuma akiwa amekopa toka mabenki mengi nchini na kutumia ubunge wake kukwepa kulipa hayo madeni. Hivi niandikapo ana kesi chungu nzima kwenye mahakama zinazohusu udhalimu wake wa kutaka kuibia mabenki!!

Hakuna Tajiri anayejiita Tajiri Kweli ambaye hana Elimu ya kutosha; katika Orodha ya FORBES ya matajiri duniani hakuna hata mmoja aliyesoma shule ya Kayumba!!! Mzee BAKHRESSA makampuni yake yanaendeshwa na watoto wake waliosoma na kuelimika.

Matajiri huweka utajiri wao wazi. Tajiri uchwara msukuma anaweza kutuambia HOW MUCH HE IS WORTH? Mabasi yake rote ni ya kukopa na hajarudisha fedha anazodiwa hata na Wafanyabiashara wenzie!! Kwenye nchi zilizostaarabika huyu msukuma asingekuwa mbunge kwani hana HADHI hiyo.
 
Prof.Muhongo ni lulu ya Taifa! Labda nachoona tangu zamani hajui kuimba mapambio.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…