SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Wakati mgogoro wa Yanga na Feisal Salum ukionekana ukienda kumalizika, tukumbuke pia kulikuwa na mgogoro mwingine wa kimkataba kati ya Yanga na mdhamini wao mkuu SportPesa.
Ilionekana kutokana na ratiba ngumu za mashindano, mgogoro wa Yanga na SportPesa uwekwe pembeni kwanza hadi msimu utakapoisha. Za ndaaani inasemekana SportPesa mpaka sasa wamegoma kulipa bonus zozote za ligi ya NBC na zile za Kombe la Shirikisho kutokana na wao kuamini kuwa makubaliano ya mkataba yalikiukwa.
Kama mnakumbuka M-Bet walitangaza kulipa bonus baada ya Simba kuvuka hatua ya makundi ila mpaka leo hatujawahi kusikia SportPesa wakifanya hivyo kwa Yanga.
Kilichokuwa kinaleta ugumu zaidi katika mgogoro huu ni muingiliano wa maslahi uliopo kutokana na Abbas Tarimba kuwa si tu mtu muhimu ndani ya SportPesa lakini akiwa pia na maslahi ndani ya Yanga na ameonekana kuweka maslahi ya Yanga mbele zaidi ya SportPesa.
Kuonyesha Yanga wanajaribu kuwapoza SportPesa sasa hivi kuelekea mwishoni mwa msimu, wakijua lolote linaweza kutokea hasa kutoka makao makuu ya SportPesa, wakati wa halfa ya chakula iliyofanyika Ikulu, Yanga walivaa jezi zenye nembo ya SportPesa badala ya mdhamini wao wa Kombe la Shirikisho ambao ni kampuni ya Haier.