Nyumba za serikali ziliuzwa kwa bei ya ubuyu. Thamani tu ya ardhi kutokana na maeneo zilipokuwa zimejengwa ni kubwa kuliko hata majengo yenyewe. Rais Magufuli ni wazi kuwa analifahamu hili hasa kutokana na weledi wake kwenye ardhi na ujenzi. Naomba baada ya kumaliza kuweka sawa kwenye madini na viwanda vilivyouzwa kwa bei ya vibua tuhamie kwenye kurudisha au kudai bei halisia ya nyumba zile ili waliozinunua ama wazirudishe au waongeze hela kulingana na bei halisi ya soko ya nyumba hizo