Tukimvumilia leo kesho ataiba zaidi ya haya

Johnson Alex Otieno

Senior Member
Joined
Mar 14, 2013
Posts
172
Reaction score
57
SERIKALI YA WANAFUNZI UDOSO COED 2014/2015
MAAZIMIO YA KIKAO CHA BARAZA LA MAWAZILI LILILOKAA LEO TAREHE 19/ 06/2015 JUU YA UBADHILIFU WA KUTISHA ULIOFANYWA NA RAIS WA KITIVO CHA ELIMU NDG. JOHN FRANCISCO NZILANYINGI.
Yafuatayo ni maazimio ya kikao cha Baraza la Mawaziri linalomaliza muda wake juu ya ubadhilifu wa kutisha uliofanyika katika akaunti ya UDOSO COED uliofanywa na aliyekua Rais wa kitivo cha Elimu Ndg. John Francisco Nzilanyingi, Wizara ya Fedha inayo ongozwa na ndugu Shabani Ramadhani na Wizara ya Habari Usafirishaji na Matangazo inayo ongozwa na Ndugu Elias Boaz. Hii ni kuonyesha ni kwa namna gani ambavyo tumesimamia misingi ya haki, na uwazi katika kufanikisha hili. Baada ya kutilia shaka juu ya matumizi ya pesa ya serikali ya UDOSO baadhi ya mawazili wa serikali ya wanafunzi wakiongozwa na aliyekua waziri wa mikopo ndugu Mpandalume Simon Mpandalume, naibu waziri wa Katiba na Sheria ndugu Charles Josias, naibu waziri wa Mikopo Bi. Martin Lydia na Waziri wa Matangazo na Usafirishaji walianzisha vugu vugu la kuhoji juu ya matumizi ya pesa hiyo ambayo ni makusanyo ya pesa za Wanachuo ambazo wanazichanga kwa kujibana sana na hadi kutokuruhusiwa kufanya usajiri bila kukamilisha kulipia kiwango hicho cha shilingi 5000/=
Katika ripoti hii kiasi cha shilingi za kitanzania zaid ya Shilingi Milioni Sita laki saba na kumi na tatu Elfu (6,713,000) zinaonekana kuporwa na aliyekua Rais wa kitivo cha elimu ndugu John Francisco Nzilanyingi. Kwa ujumla ripoti hii imegaanyika katika sehemu kuu TATU ambazo ni
TAARIFA YA MIAMAMALA NA MATUMIZI YA KUTIA SHAKA ILIYOFANYWA NA RAIS ANAEMALIZA MUDA WAKE NDG JOHN FRANCISCO NZILANYINGI.
Moja ya muamala unaoonyesha ubadhilifu wa kutisha ni ule wa shilingi million 13 ambao malipo halis yalikua shilingi milioni sita laki laki nane na sabini na sita elfu (6,876,000/=),huku ndugu John Francisco Nzilanyingi akikiri kubaki na kiwango cha shilingi milioni sita laki moja na ishirini na tatu elfu na mia sita (6,123,600/=)ambazo alizitumia kwa matumizi yake binafsi.
Muamala wa pili uliofanyika tarehe 08, May 2015 ambapo zilitolewa shilingi laki nane na sitini na tano elfu (865000/=) ambapo matumizi halisi yalikua shilingi laki sita na thelathini na tano elfu(635,000) hivyo rais alijipatia kiwango cha shilingi laki mbili na elfu thelathini 230,000 kinyume na taratibu.
Pia kuna miamala iliyofanyika awali toka akaunti ya shirikisho kiasi cha shilingi laki tatu na elfu sitini (360,000/=) ambacho aliagiza kupatiwa pesa hizo kutoka wizara ya fedha kwa madai ya kuwapatia wizaraya Maji na Wizara ya Jinsia ambazo hawakupewa na Rais amekiri mbele ya baraza la Mawaziri kuwa hawakupewa.

TAARIFA YA MAKUSANYO NA MATUMIZI YA BAADHI YA WIZARA ZENYE KUTIA SHAKA.

Katika kufanya ukaguzi katika baadhi ya wizara ikiwemo;
Wizara ya Habari, Usafirishaji na Matangazo inayo ongozwa na Ndg. Boaz Elias tumegundua kuna makusanyo ya Takribani shilingi laki tisa na elfu themanini (980,000/=) ambapo kiasi cha shilingi laki sita na elfu ishirini na tano (625,000) ziliwasilishwa serikalini kupitia Wizara ya fedha kama ianavyo tanabaishwa naWizara ya Fedha kupitia Ripoti ya Fedha iliyofikishwa bungeni kabla ya kusomwa kwa bajeti yaMuhula wa pili. Hivyo baada ya mkokoto iliofanyikabaada ya Ukaguzi uliofanywa na aliyekua Waziri wa Maji ndugu Vicent Alistides kwa ushirikiano na aliyekua Naibu waziri wa katiba na Sheria ndg. Charles Josias ilibainika kuwa kuna upotevu wa shilingi laki tatu na elfu hamsini na Tano (355,000) ambapo Waziri wa Matangazo alishindwa kutoa ufafanuzi unaojitosheleza juu yaMatumizi ya Pesa hizi hali iliyoibua maswali mengi katika baraza la Mawaziri.
Wizara ya Fedha inayo ongozwa na ndugu Shaban Ramadhan ilifanyiwa ukaguzi na kubainika matumizi ya Shilingi Elfu themanini na tano tuu (85,000/=) ambazo hazikua na maelezo ya kujitosheleza na hivyo kuleta hali ya sinto fahamukatika mahojiano na baraza la Mawaziri. Pia kulibainika malipo feki yaliyolipwa kwa Mtu mwenye jina la Omary Said kiasi cha shilingi laki moja na ishirini na moja elfu121000/= ambazo pia hazikutolewa ufafanuzi wa Kujitosheleza. Hivyo Pesa iliyotumiwa na wizara ya Fedha kinyume na taratibu ni kias cha shilingi laki mbili na Elfu sita (206,000/=).

MAAZIMIO YA BARAZA LA MAWAZIRI KWA PANDE ZOTE MBILI BAADA YA KUJIRIDHISHA NA USHAHIDI NA MAEEZO YA UPANDE WA WATUHUMIWA.

1.Rais mstaafu ndg John Francisco Nzilanyingi afikishwe mahakamani kwa kughushi sahihi za mawaziri, manaibu mawaziri na Wabunge wa UDOCE. Suala hili linafanyika mara moja na halihitaji mashauriano ya aina yoyote na utawala wa chuo kikuu cha Dodoma. Suala hili ni kosa la jinai na lisilopaswa kufumbiwa macho hata kidogo.

2. Kuita vyombo vya habari na kuvijulisha juu ya ubadhilifu uliofanyika na ndugu John Francisco. Suala hili pia ni la lazima lifanyike haraka ili kuweka dhana ya uwazi na uwajibikaji katika jamii ya wana UDOM na Taifa kwa ujumla.

3. Kutuma waraka kwa Marais wa vyuo vyote Tanzania Kupitia TAHLISO kuwajulisha juu ya ubadhilifu uliofanywa na Mwenyekiti wa TAHLISO ndugu John Francisco.

4. Baraza limeazimia kwamba ndugu John Francisco arudishe pesa yote aliyokiri Kuiba kiasi cha Shilingi Milioni Sita laki saba na kumi na tatu Elfu (6,713,000) kuanzia leo Tarehe 19-06-2015 kufikia siku ya Jumapili ya tarehe 21-06-2015. Endapo hatakua amerudisha pesa hadi siku ya Jumatatu asiruhusiwe kufanya mtihani wa mwisho unaoanza jumatatu ya Tarehe 22-06-2015. Na endapo hili litakiukwa wanafunzi wote watagomea mtihani huo kushinikiza maamuzi haya kutekelezwa.

5.Sheria za chuo zichukue hatua mara moja kwa kufuata katiba ya UDOSO na students By Laws kumsimmamisha masomo mara moja ili kuweza kutoa fundisho kwa viongozi wa namna hiyo.

6. Wizara zote zilizobainika kufanya ubadhilifu wa pesa kama ilivyo bainishwa hapo juu zinatakiwa kurejesha kiwango hicho cha pesa na kuzikabidhi kwa Serikali mpya kabla yaKuanza mitihani siku ya Jumatatu. Na pia pesa hizo zitumiwe na serikali mpya katika kuboresha miundombinu mbali mbali kwa Manufaa ya Wanachuo. Na taarifa ya matumizi hayo yasomwe mbele ya wanachuo wote na ziandikiwe taarifa Maalumu.

7. Kuita wanachuo kwa pamoja leo tarehe 19/06/2015 na kuwatangazia juu ya maovu yaliyo fanywa na ndugu John Francisco Nzilanyingi siku ya saa kumi kamili Jioni.

8. Kuita kikao na serikali mpya na kuwajulisha juu ya hatua tulizofikia katika kusimamia suala hili na kukabidhiwa majukumu ya kusimamia kesi hii hadi itakapo fikia Tamati.

Ni matumaini yetu kuwa maazimio tajwa hapo juu yatatekelezwa kama tulivyo afikiana katika kikao halali kilicho fanyika leo Tarehe 19/06/2015 katika ofisi ya Rais iliyopo Block Q 15.Shukrani za dhati kwa wajumbe wote waliohudhuria kikao na kutoa ushirikiano wao kuanzia mwanzo hadi mwisho kama orodha ilivyo ambatanishwa hapo chini.

Wako katika ujemzi wa Taifa
……………………. ……………………..
MAARUFU KHADIJAH CHOTTA PETER
MAKAMU WA RAIS 2014/2015 KATIBU MKUU UDOCE 2014/2015

KAMATI ILIYOTUMIKA KUANDIKA RIPOTI HII
JINA WADHIFA SAHIHI
CHARLES JOSIAS MWENYEKITI ……………..
VICENT ALISTIDES KATIBU ……………..
MAJIDU HASSAN I MJUMBE ……………..
MARTINE LYDIA MJUMBE
 

Mmefkia wap?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…