Tukimwita christopher columbus "mshirikina" itakuwa ni kosa?

Tukimwita christopher columbus "mshirikina" itakuwa ni kosa?

Wickama

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2009
Posts
1,466
Reaction score
1,196
Wanaukumbi,

Christopher Columbus ni jina linalohusishwa uvumbuzi la bara la Amerika. Potelea mbali utata wa kama ndiye aliyefika wa kwanza maeneo hayo au la. Inajulikana pia kuwa Columbus alikuwa ameshiba imani ya dini yake na hata baadhi ya maeneo aliyofanikiwa kuyaona aliyaita majina yanayoambata na imani yake.

Utata wa bwana huyu ni kuhusu safari yake ya kwanza kuelekea huko bara la Amerika. Imeripotiwa kuwa Christopher Columbus alimfuata Mnajimu wa nyota ili amtazamie kheri na shari ya safari yake kabla hajasafiri.

Mnajimu huyu, alimweleza Columbus kuwa baadhi ya nyota zilikuwa zimefungamana vizuri zikiashiria kuwa kungetokea tukio kubwa la kihistoria na kwa maana hiyo kumpa "go-ahead" ya safari. Safari hii ya columbus ndio iliyoliona bara la Amerika na kumwingiza katika histotia iliyotukuka.


[h=3]ASTROLOGY, FAMOUS PEOPLE, HISTORY[/h][h=1]Christopher Columbus consulted an astrologer named Pierre D’ailly about the journey which eventually led to his ‘discovery’ of America[/h][h=2][/h]Christopher Columbus consulted an astrologer named Pierre D’Ailly about the journey which eventually led to his ‘discovery’ of America.
D’Ailly told Columbus that Saturn and Jupiter were going to be conduct during this time and that this conjunction usually meant that some big historical event was going to happen.




Source: Christopher Columbus consulted an astrologer named Pierre D'ailly about the journey which eventually led to his ‘discovery' of America | DidYouKnow

Nauliza, kwa desturi hii ya Columbus kumtafuta mtu huyu wa nyota kwanza kabla hajasafiri ni halali kumuita gwiji huyu Mshirikina? Au ku-consult nyota kabla ya kufanya jambo sio ushirikina?
 
huezi mwita mshirikina unajua kuna ulimwengu wa mwili na wa roho sasa hao wanajim wanatumia majin na ushirikina kuangalia nyota na mambo mengine ya rohoni so sithani km ni sahihi ila angomba wamsaidie labda apo tungemuhusisha.... but de fack from the story z hakua mtu wa Mungu coz alitegemea wanadam instead of God
 
Samahani Mkuu, naomba kutoka nje ya mada, hivi hao Doberman pinscher unao au ni picha tu uliyochukua mahali? Nawatafuta sana.
 
Samahani Mkuu, naomba kutoka nje ya mada, hivi hao Doberman pinscher unao au ni picha tu uliyochukua mahali? Nawatafuta sana.
Kuna afande mmoja huku Tanga anaweza kukusaidia kuwapata. Hii picha ipo kwenye google images za hao mbwa, niliipenda kwa kule kuonyesha discipline na seriousness. Nafuga aina tofauti ya mbwa, labradors.
 
Kuna afande mmoja huku Tanga anaweza kukusaidia kuwapata. Hii picha ipo kwenye google images za hao mbwa, niliipenda kwa kule kuonyesha discipline na seriousness. Nafuga aina tofauti ya mbwa, labradors.

Bei zake zikoje?
 
Sikiliza wimbo wa Burning Spear "Christopher Columbus"
 
Back
Top Bottom