Tukio gani alilowahi kukupiga mpenzi wako ambayo hutoisahau?

Tukio gani alilowahi kukupiga mpenzi wako ambayo hutoisahau?

Mbahili

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
281
Reaction score
525
Mimi stori iko hivi,
Mnamo mwaka 2020 nilianza kuwa na mahusiano na binti mmoja(mcha Mungu sana). Alikuwa anasoma chuo fulani jijini Arusha, nakumbuka hicho kipindi nilifanikiwa kupata tempo mahala fulani( si unajua hela za tempo) so, ikabidi niwe natumia muda mwingi kutembea wakati wa kurudi nyumbani.

Kwa kuwa ni mpenzi wangu halali na mcha Mungu mara alikuwa anakuja kwangu tunaspend weekend pamoja, sikuwa na wasiwasi. Siku moja mnamo mwaka 2021 alikuja kwangu kama kawaida yake ila kuna namba ikawa inapiga na kumsumbua (kila akiona hiyo call ananiangalia then hapokei). Nilimuuliza mbona hapokei simu anajibu ni mdeni anamsumbua(koz kuna kipindi alinambia anadaiwa kiasi kadhaa nikajikamua nikampatia) akaniambia ile hela aliongezea kidogo akalipia pango ila mdeni bado anadai chake.

Nikatafakari nikapata wazo, alivyotoka kwenda kuyapata maji, niliblock zile number then nilijua mdeni atatapika nyongo akiona amekuwa blocked.
Alipotoka kuoga tukala stori tukala then tukalala, but by saa 8 nikakumbuka kumtoa mfungwa niliemfunga jela hahaha.. kabla sijamtoa ikabidi niende kwenye blocked messages. Hapo nilichoka. Kumbe huyu mtakatifu wangu kabadilisha chongeo kuwa mtaji, yaani anatumia equation y=X² mm ndo y, jamaa ndo x². Akinipa mbili jamaa nne, akinipa 6 jamaa 36. Jamaa alituma message from saa 2 mpaka saa 7 huko. Nilipata full picha yaani. Dah nikazifuta, nikamu unblock jamaa asubuhi nikamwambia nmepata dharura inabidi nitoke(niliogopa hata kumwacha ndani).

Tulitoka akaenda chuo(nadhani kumfariji mr x². Sikuwaza wala nn. Nilishangaa how comes kwa cm yake tunapicha zetu tumepiga hata ukiona unajua she's in relation but jamaa huwa haangalii au. Nadhani ht wall paper kaweka tukiwa tumehug. (Au alikuwa na highest cheating IQ?

Harmonize anasema,"Hata za mwizi arobaini".
Siku moja nikiwa nmetoka kwa pilika zangu simu ikawa imekata chaji, na kuna mtu wa muhimu nilitaka wasiliana nae b4 sijashuka skani. Nikapita sokoni kuchukuq viwili vitatu, then nimpelekee tukapike then tuke bhana. Kweli nikapita nikanunua baadhi ya mahitaji nikaenda bhn.

Nilifika nikamkuta na best ake( her best friend looks so innocent) tukasalimiana just shem mbona umetususa and all that. Tukapika fresh nikaboost simu nikawa nataka kutoka mara ghafla mlango unagongwa. ....

Itaendelea............(1/2)
 
😂😂😂 we jamaa unaijua alosto kweli wewe
 
2/2 {kuchoka wanangu}

Tukapika fresh nikaboost simu nikawa nataka kutoka mara ghafla mlango unagongwa. ....
Sikuwa na wasiwasi koz nipo kwa mpenzi wangu napolipia kodi bana..
Mpenzi wangu akaenda fungua jamaa hakuingia wala hakuniona koz mlango hufungukia upande wa kitanda. Wakaongea kidogo, manzi angu akaingia ndani na kuchukua vitu kwa mfuko na kuniambia anampa mzigo wake anarudi. Sawa nkasema moyoni ngoja tuone litalapoishia...

Akatoka nje na mfuko, ila nikawa nasikia majibizano kidogo nje.. nikakausha kv sijui kinachoendelea. Jamaa ikabidi aingie ndani bhana kujiridhisha mimi ni nani koz aliona viatu vya kiume nje....

Alivyoingia ndani kanikuta nmechil kwa bed nachezea simu ya beibee.. kumuona jamaa, nikakumbuka sura hii hii ndio ilikuwa inatuma jumbe nyingi whatsapp but huwa naambiwa ni mdeni.

Alivyoingia alinikuta kamanda nakula ikabidi nimkaribishe akasema asante.. kumbuka hapo ndani tuko mtu 4, manzi angu na rafiki ake, mimi na mdeni. Akataka ongea nkamwambia tulia nimalize kula, koz nlikuwa na ubao kinoma na niliwaza huenda ugomvi ukawaka wakati sijala. So nilipomaliza ikabidi mazungumzo yaanze..

Jamaa: bro, we huyu nani wako?
Mbahili: kwani kakutambulishaje?
Jamaa: kaniambia kuna mtu anamdai sasa nikampa pesa amlipe, nampigia simu hapokei ikabidi nije kwake moja kwa moja.( na kweli alikuwa akipiga simu nilikuwa naona but sikuwa napokea mara nakata koz niko nacheza game kwa simu ya bebe.. nilitamani jamaa aje nimfahamu..
Mbahili: Ha! Mimi ndo mdeni sio? Hivi huyu unamjuaje?
Jamaa: Ni mpenzi wangu yapata miezi 6 sasa..
Mbahili: Dah! (Nilishindwa jizuia ikabidi nimuulize), vipi simu yake huwa hushiki?
Jamaa: hapana, sijawahi. Na hata hapa(akaelekea kwenye kisanduku katoa kitu.... Hee funguo)
Jamaa: Hata hii funguo ni yangu, huwa anakuja kupika kufua tunakula na kula tena kila siku.. Hata akiwa pepa, alikuwa anaamkia kwangu kila siku...
Mimi: (nilihisi kama nmemwagiwa maji barafu).. Vipi anayosema kuna ukweli? (Nampatia jina code mwajuma)
Mwajuma: huku akilia kwa kwikwi... muongoo huyo
Nikabidi nimpe jamaa namba kiaina akantext then nkamtumia meseji tukitoka hapa tukasove nje kiaina, ila huyu raia asijue tunawasiliana...

Kweli jamaa kachomoka, by saa moja namm natoka kwa bebe nkimpa moyo kuwa kuna watu wanataka wakuchafue tu...

Nilipotoka nkamcheki jamaa akaniskilizisha voice notes whatsapp, messages zote, yaani nilihisi ganzi but ndo uanaume.. nkakaa siku ya kwanza nkashindwa vumilia nkamblock.

Nifupishe story, hili pigo lilikuja ila namshukuru Mungu nimepima niko safi, ila mwanafunzi wa chuo usiweke nae malengo, utakuja kujicheka bure...
 
Hebu maliza hapo mzee. Extend hii story ulivyonana na jamaa ikawaje? Na manzi aliomba msamaha.
 
Hapo mwisho umekosea ungeandika .."usiweke malengo na manzi yyte utaumia" haijalishi ni mwanachuo au lah.We unawaza yako mwenzako nae anawaza yake.
 
Back
Top Bottom