Tukio gani lilikupishanisha na kifo?

Tukio gani lilikupishanisha na kifo?

Diwani

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2014
Posts
2,680
Reaction score
2,779
Katika maisha licha ya kuwepo na changamoto nyingi, kuna matukio ama changamoto ambazo zinakaa ndani ya mioyo yetu bila kutoka kwa sababu ya uzito wake hasa pale yanapo tufanya tunusurike kifo.

Niende kwenye tukio, Mwaka 2019, jijini Dodoma, kwa uwezo wa Mungu nilifanikisha kupata kaelimu kangu ka chuo, sasa wakati wa mahafali, nilitembelewa na wazazi wangu pamoja na dada yangu.

Wakati tunatoka ukumbini, kwa ajili ya kwenda kusheherekea nje ya mji, nikawa napiga piga picha na rafiki zangu, kitendo kilichofanya wazazi wangu watangulie na kunipa muda wa mimi kuendelea na ratiba zangu, wakaniambia tu, “tutakutana hotelini pale” nikawaambia hakuna shida, nikaanza kupiga picha, mara stori za hapa na pale ili mradi tu, tusemezane neno la mwisho kila mtu akipotea kwenye uso wa mwenziwe iwe kwaheri.

Sasa basi; shida ikaja kwenye usafiri wa kutupeleka huko kwenye shughuli baada ya pale ukumbini, si gari, bajaji wala boda boda iliyokuwa na nafasi ya mimi kujiegesha, zote zimejaa, nikawa nashuka mdogo mdogo nikitaraji nitapata hata boda huko mbeleni, ghafla ikaja dala dala imejaa, ila kuna mahala pa kuning’inia mlangoni, mwanaume nikajiweka, hapo nipo kwenye suti, nimeshika maji kichwani nimevaa kofia ya muhitimu [emoji310] nikaanza kushika bomba, safari ikaanza, gari ikaanza kutembea, sasa kwa kuwa kwa kimo cha pale nilikuwa mrefu kidogo, nikaamua kuivua ile kofia nikamvalisha kondakta, gari ipo kwenye moto na ndio ilikuwa inashuka mlima, konda yupo mbele yangu, tunaning’inia wote mlangoni, mara upepo mkali ukaja ukapita na ile kofia kichwani kwa konda, ghafla kama wenge hivi nikajikuta najaribu kuikamata mguu ukateleza nikaenda chini na hapo gari ipo mwendo, nikabiringika kwenye rami nikazunguka kama mara tatu hivi halafu nikaingia mtaroni kabisa.

Mwili mzima unaniuma, nikawa nimechunika na suti ishachanika hapo, sio suruali wala koti, watu kwenye gari wakabaki wametahamaki wakajua ndio tayari hivyo, kwisha habari yangu nikawa nawasikia akina mama kwa mbali wanapiga yowe, mwanaume nikaamka najikongoja, walivoona vile wakanikimbilia, nikaenda mdogo mdogo naifuata kofia, damu zinatoja mkononi, nikaichukua nikawa narudi kwenye gari, nikapanda gari watu hawaamini kama ndio mimi, safari ikaendelea, nashuka ndio nikaanza kujua kumbe nimeumia sana ndani kwa ndani, nikaamua kwenda kwa fundi watu wananishangaa, uzuri ni kuwa fundi mwenyewe alikuwa anashonea ndani kwake, hivyo nilikaa humo ndani nikajipa huduma ya kwanza.

Nikapigiwa simu nipo wapi, nikawa naongea kwa upole kweli, nikakaa pale kama nusu saa hivi kisha ndio nikaenda kule, mwili mzima unaniuma lakini hakuna aliwahi kujua nini kimenitokea (hadi leo) nilikaa chini kwenye kiti sijanyanyuka mpaka shughuli inaisha.

Vipi kwa upande wako?
 
Natoka shule na marafiki zangu mara mvua kubwa ikaanza kunyesha, tukajibanza kwenye nyumba ya jirani kama mita 70 kufika home. Mvua ikakata yakabaki manyunyu kwambali, tukaanza kutoka taratibu kuelekea home, ghafla ilipiga radi ya maana bila kujielewa tukajikuta tupo ndani nyumba ya jirani mkabala na yakwetu. Kuchungulia nje mti wa mnazi unawaka moto baada ya kupigwa na radi. Mpaka leo nimekuwa muoga wa radi.
 
[emoji46][emoji46][emoji46] aisee
 
enzi izo ni mayoung kuna sehemu tulikuwa tunaenda kuogelea mikoa ya pwani sasa sisi tulikuwa tunajifanya vigunge wazee wa kazi tukifika pale watu wanatushangilia tuko wengi hawa waarabu hawa watu wa pemba kuogelea yetu si kitoto pale tunapiga mpaka ksiwani parefu ila sidhani kama 1km inafika ila inakaribia uzuri wake kati kati kuna kuwa na boats na meli zimepark

bhana siku moja jumapili kama kawa wana hao tukajijaza tukavizia zile siku maji yamejaa tups yetu kama kawa tukajiunga kama 7 ivi tukaanza kuchapa maji sasa hatukuenda pamoja ikawa tunaogelea freestyle kikubwa kufika kisiwani ila ukitaka unapumzika kuna boats katikati siku iyo nikaona nipige ndefu bila kupumzika dah nilishikwa na msuli miguu imekaza duh naona kifo ichi natumia mikono kujipndisha juu tu miguu imekakamaa panic kinoma kupiga kelele nashindwa nimekaa kama dk 10 ivi na ile badiri we acha miguu imekaza maumivu kinomA mra miguu ndo inaachia nishajua nakufa nikazama kuibuka nikapata nguvu nikapiga makasia mpaka kweny boat moja ivo imeeandikwa cameroon sisahau mpaka leo nilikaa na lipofika kupata kutoa mwili kweny maji msuli ukanishika tena

mpaka wana wanakuja nawaeleza wanachek sana wanazani ni utani
 
Aisee maji, pole sana kaka
 
Aisee maji, pole sana kaka
ila kuogelea kama kawa kuna jmaa yetu mmoja mpemba yeye ni mvuvi kabisa alikufa maji alipozamia kutega nyavu akakutana na paper kaliwa vipanda vipande ila mi sio mvuvi kama yeye
 
Mwaka 2019 baada ya kutafuta ajira kwa bidii sana lakini sikufanikiwa nikaambulia kupata kibarua cha ulinzi kwenye kampuni ya ujenzi ya wachina...siku moja nikiwa eneo la rindo nikafatwa na wazee wa kazi wakaniambia ndani ya ofisi zile kuna pesa nyingi,kwa sababu mchina huwa hapeleki pesa yake benki...wazee wa kazi walihitaji ushirikiano kutoka kwangu niwape ramani ya jengo husika pamoja na ratiba za wachina muda wa kupumzika na muda ambao wanakuwa hawapo eneo husika...mwamba wa miamba nikakataa kuwapa ushirikiano jamaa.....tarehe 10/03/2019 ilikuwa ni siku yangu ya mapumziko na ndio siku wazee wa kazi walivamia usiku wakiwa na mapanga waliwakatakata walinzi waliokuwepo na kumjeruhi mchina mmoja kwa nondo..walifanikiwa kuondoka na kibunda...
 
Daaah haya mambo mm naonaga kwenye muvi tuu
 
Mungu akiwa upande wako aiseee
 
Mtumbwi ulizama ziwa Tanganyika, nakumbuka yale maji niliyaona meusi kabla sijapata akili ya kujiokoa..nilipoteza kila kitu majini na kubaki mimi na roho yangu.
 
Back
Top Bottom