Tukio gani lilitokea mwaka uliofanya Mitihani ya Kidato cha 4 na hautakaa ulisahau?

Tukio gani lilitokea mwaka uliofanya Mitihani ya Kidato cha 4 na hautakaa ulisahau?

Mtoa Taarifa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2024
Posts
213
Reaction score
671
Mimi nakumbuka tukiwa Mtihani wa Geography tulitolewa chumba cha Mtihani kwa madau Pepa imevuja hadi Bungeni Wabunge wanayo. Tukasimamiswa wote Mtihani ubabadilishwa siku, wazimamizi na rangi mtihani kutoka Njano kuwa Nyeupe.
 
Sisi bwana nakumbuka pepa ilikuja na marking scheme, waandaaji naona walijichanganya sana. Dah!

Mwaka huo matokeo nchi nzima alama ya mwisho kwa kila mtahiniwa ilikuwa 95. Yaani waliamua kusahahihisha hadi ubora wa mwandiko na aina ya peni iliyotumika kuandikia, kwa vile hawakuwa na jinsi.
 
2004, mitihani ilivuja balaa, tulikuwa tunasoma boarding tulikuwa hatujui hata kinaendelea Nini.
Tuliporudi nyumbani ndio tunaambiwa Pepa limevuja balaa. Wenzetu wa shule za day waliokuwa wanajimini watafaulu.
Matokeo kutoka Sasa😂😂😂waliopata Pepa wacha waangukie pua.
 
Sisi bwana nakumbuka pepa ilikuja na marking scheme, waandaaji naona walijichanganya sana. Dah!

Mwaka huo matokeo nchi nzima alama ya mwisho kwa kila mtahiniwa ilikuwa 95. Yaani waliamua kusahahihisha hadi ubora wa mwandiko na aina ya peni iliyotumika kuandikia, kwa vile hakuwa na jinsi.
Mmh mwaka gani huo?
 
Huku kwetu pepa iliyokuwa ifanyike saa nane mchana ikakutwa mapema asubuhi imebandikwa kwenye ubao wa matangazo ofisi za elimu mkoa.
 
2012.. watu tulilamba zero balaa.. bunge likaingilia Kati mitihani usahihishwe upya, mwamba ndalichako akatokewa Necta... Jiwe akaja kumkumbuka 2015
 
Nakumbuka mwaka 2000 tulikua na paper ya commerce asubuhi…tumepiga paper vizuri wakati tunarudi home (shule ilikua ya day) tukakutana na washikaji ndio wanakuja kupiga paper hiyo hiyo…walijichanganya ratiba wakajua paper ni mchana kumbe ilikua asubuhi.
 
2012 😀 matokeo yametoka ya mwanzo una div 4, wakasahihisha tena mitihani wakatoa matokeo mengine unajikuta una div 1.7 😂😂😂
 
Nakumbuka siku ya mtihani wa mwisho wa vitendo( practical )Nilichelewa kwa sababu ya mvua kubwa iliyonyesha na siku hiyo nilifua sare za shule nikasahau kuzianua kwahiyo zilinyeshewa na nilienda hivyo nimeloa ndo ikawa sababu ya kunitetea kuingia kwenye mtihani sitasahau
 
Mimi nakumbuka tukiwa Mtihani wa Geography tulitolewa chumba cha Mtihani kwa madau Pepa imevuja hadi Bungeni Wabunge wanayo. Tukasimamiswa wote Mtihani ubabadilishwa siku, wazimamizi na rangi mtihani kutoka Njano kuwa Nyeupe.
Kufariki kwa marehemu kanumba mwaka 2012
 
Mimi nakumbuka tukiwa Mtihani wa Geography tulitolewa chumba cha Mtihani kwa madau Pepa imevuja hadi Bungeni Wabunge wanayo. Tukasimamiswa wote Mtihani ubabadilishwa siku, wazimamizi na rangi mtihani kutoka Njano kuwa Nyeupe.
Sitasahau tulifutiwa mitihani 1998...na ndo mwanzo wa polis kuisimamia mitihani
 
Enzi hizo sekondari kipindi cha mtihani wa taifa tulibahatika kupata msimamizi aliekuwa peace kweli. Ndipo tukamshwawishi atuvujishie pepa kwa gharama ya 5M tulio changa kijiji kizima.

Mitihani yote tuliofanya kweli maswali yalikuwa yaleyale kama tuliovujishiwa na kudiscuss. Shida ikaja kwenue pepa la mwisho ile kufunua tu maswali yote ni tofauti kabisa. Nyuso za kila mmoja zilikunjamana maana hatukusoma tulitegemea kitonga kingeendelea. Ndipo uvumilivu ukamshinda Peter Bhatazaar na kuamua kuropoka kwenye chumba cha mtihani "mbona tumekupa Pesa ya maana alafu unatupa kitu kisicho chenyewe"

Patashika ilioendelea hapo haielezeki. Kwa ufupi tu. Hivi sasa mimi ni bodaboda na uyo Peter ni mvuvi
 
1998 pepa ilifutwa yote , sisi tulikuwa seminary hatukupata pepa hata moja.
Bora ilivyofutwa manake story nilozozisikia kwa watu wa day dsm walikuwa wana booklets walikuwa wanafanyia pepa nyumbani kwenye chumba cha mitihani walikuwa wanabadilisha booklets tu wanatoa ile waliyofanyia nyumbani wanakusanya
 
Du!... Mwaka ni 1978. Mwezi mmoja kabla ya kuanza mtihani, si nduri Iddi Amin Dadah akaamua kuingiza jeshi lake ndani ya Tanzania na kuteka eneo lote la kaskazini la mto Kagera?

Tulilazimika kujiandaa na mtihani wa kidato cha nne wakati huo huo tukijiandaa kwa vita, tulichimba mahandaki ya kila aina maeneo mengi tu ya Kinampanda. Mahandaki ya L, V,Y, I n.k.... Mbaya zaidi tukazuiliwa kufanya Graduation, baada ya mitihani mabasi yakaja kutusafirisha kimya kimya. 😂
Mambo ya kuvuja mitihani naona ni miaka hii hii ya Tik Tok!
 
Daaah sisi tulikutana na Physics theory ngumu sana kwa darasa letu, tukawa tumejiandaa vizuri kwa Practical kadhaa za Physics tukijua kabisa hizo ambazo Mwalimu alitufundisha zitakuwepo na tutajipatia marks kirahisi . Kilichotukuta ni Practical ambayo hatujawahi kuiona kabisa.
Ndipo kulikuwa na kilio na Kusaga Meno ndani na nje ya mtihani😭😭
 
Mtihani wa Basic Mathematics ulivuja vijana wa hovyo wakaanza hadi kuubandika katika nguzo za umeme kama matangazo ya show za Akudo Impact, kufika shule tukaambiwa tujiandae kwa mtihani wa mchana wa Civics mtihani ambao ulitakiwa uwe wa kwanza yaani Basic Mathematics ndiyo ukawa mtihani wa mwisho kufanywa baada ya mitihani ya masomo yote kupita.
Mtihani wa Kiswahili pia ulivuja jambo lililopelekea kuletewa mtihani wenye vitabu ambavyo hata kwenye mtaala hatukuwahi kuviona.
Huwezi amini paper zote zikawa zinaandikwa chini kuwa ni (hpp), vijana wa hovyo wakatafsiri kuwa hulipati popote
 
2004, mitihani ilivuja balaa, tulikuwa tunasoma boarding tulikuwa hatujui hata kinaendelea Nini.
Tuliporudi nyumbani ndio tunaambiwa Pepa limevuja balaa. Wenzetu wa shule za day waliokuwa wanajimini watafaulu.
Matokeo kutoka Sasa😂😂😂waliopata Pepa wacha waangukie pua.
Nakumbuka paper la civics boys walilipata wakajichimbia chimbo kusolve, Asubuhi ndio tunasikia. Basi tukawalaumu na kuwaona mashetani. Kuingia kwenye paper kumbe silo, weeeh walidataaa🤣🤣🤣

Tulikata tamaa kabisa kuendelea kusoma huku tukisikia story za paper kuvuja, huku wengine wakisema tutarufia mitihani.
 
2012.. watu tulilamba zero balaa.. bunge likaingilia Kati mitihani usahihishwe upya, mwamba ndalichako akatokewa Necta... Jiwe akaja kumkumbuka 2015
Pepa lenu lilisahishwa mara mbili 😂
 
Back
Top Bottom