Tukio kuuuubwa la burudani linakuja, Wasafi beach party, hii si ya kukosa.

Tukio kuuuubwa la burudani linakuja, Wasafi beach party, hii si ya kukosa.

samsun

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2014
Posts
7,386
Reaction score
5,965
Ni tukio kuuubwa kabisa la burudani kuwahi kutokea Tanzania na East Africa kwa ujumla wake na tukio lenyewe ni WASAFI BEACH PARTY wakishirikiana na VODACOM TANZANIA wanakuletea wasanii vipenzi vya watanzania na Africa nzima kwa ujumla.

Tukio hili la burudani litaongozwa na msanii namba moja Africa mashariki DIAMOND PLATNUMZ akiwa na wasanii wengine wa LEBO KUUUUBWA Afrika mashariki na kati ya WCB,ambao ni Harmonize,Rayvanny,Rich Mavoko na mwanadada pekee kwenye lebo hiyo Queen Darlin.

Haya sasa wadau,mjichange ili kama vipi twende tukapate burudani ya muziki mzuri kutoka kwenye kundi la wasanii wa LEBO KUUUUUUUBWA KABISA Africa.



Kumbuka tukio hili kwa hapa Dar es Salaam litafanyika pale Jangwani sea breeze tarehe 24/12/2016, na kiingilio kwa hapa Dar ni 30,000/= kawaida na wale watu maalum tsh 100,000/= na tukio lingine litakuwa Iringa 25/12/2016 siku ya sikukuu ya X mass, na litafanyika kwenye uwanja wa Samora na kiingilio ni tsh 10,000/= kwa wote. KARIBUNI WOTE BILA KUKOSA.






 
Siez kupoteza muda kwenda kutizama watu hao, si bora nijifungie geto niskize zangu nyimbo ya africa ile ya AJE....
Hili ni tukio la burudani,na si la kwenda kuwatazama, na hata wao hawatapenda kuona umeenda kisha umekaa unawatazama bila kujumuika kwenye shangwe,kwahiyo karibu kwenye burudani.
 
Ha ha ha... bora nisklze zangu ngoma nzuri hiyo ya AJE
Hili ni tukio la muziki wa live sio la kuusilikiliza kwenye cd,nje ya kuwaona wasanii wa WCB na wasanii WAALIKWA wakiimba live na bendi,lakini pia kwenye tukio kubwa kama hili utaweza kuona na vitu vingine (nje ya stage) vitakavyokuongezea siku za kuishi, maana wanasema kwenye wengi kuna mengi. Kwahio kama utakuwa na pesa na muda unao si vibaya ukatoka kwenda kuona dunia nyingine ya burudani inafananaje.
 
Hili Tangazo la biashara lilitakiwa kuwa kule kwenye jukwaa la matangazo madogo na sio humu.

Ila umwambie Aliekutuma bila Darassa Hakuji mtu hapo.
 
Hili Tangazo la biashara lilitakiwa kuwa kule kwenye jukwaa la matangazo madogo na sio humu.

Ila umwambie Aliekutuma bila Darassa Hakuji mtu hapo.
Ushabiki wangu ndio ulionituma,si unajua sisi wengine tunasapoti kwa vitendo na si kwa matusi. Darasa anaweza kuwepo,ila bado ndio mazungumzo naye yanaendelea.
 
Back
Top Bottom