Tukio la binti kutendewa ukatili na wanaodaiwa kuwa ni askari, linanikumbusha kifo tatanishi cha mtoto wangu. Hatua zichukuliwe, binti apate haki yake

Tukio la binti kutendewa ukatili na wanaodaiwa kuwa ni askari, linanikumbusha kifo tatanishi cha mtoto wangu. Hatua zichukuliwe, binti apate haki yake

sifi leo

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2012
Posts
5,182
Reaction score
8,948
Mimi ni MZAZI, Mimi ni mlezi, Mimi ni mhanga mkubwa wa ukatili unaoendelea dhidi ya watoto wa kike.

Nina hakika kupitia hapa wasomaji wa Jamii forums mtakumbuka kisa kimoja nilikileta hapa nacho si kingine ni kile Cha kufiwa na mwanangu aliye kuwa mwanafunzi wa kidato Cha Tano shule ya sekondari Lindi gerls (Soma hapa na hapa)AMBACHO mpaka Leo hii Mimi naamini mwanangu alifia mikononi MWA mkuu wa WILAYA ya Lindi, ocd Lindi, mkurugenzi wa halimashauri Lindi, mwalimu mkuu wa secondari Lindi gerls na watumishi wengine wa Umma.

Ni kupitia hapa jukwaani nilielezea vyema jinsi watumishi wa serikali hii walivyousika kumuua mwanangu wa pekee, Leo hii usiku WA manane namwona Binti mdogo mwenye umri kama wa marehemu Binti yangu anafanyiwa ukatili wa namna hii?

Iko siku nitaanika jinsi vyombo vyetu vya Dora vinavyotumika vibaya dhidi ya raia wa Tanzania, ( ripoti ya UCHUNGUZI kutoka MAKAO MAKUU ya jeshi la polisi inasema mwanangu alikufa kifo Cha kawaida yaani aliumwa u.t.i na marelia ndani ya MASAA 12 akafariki, mkuu wa WILAYA,ocd, na mkurugenzi wakaona busara KABLA Mimi km MZAZI sijafika ENEO la TUKIO wanunue jeneza, wanunue nguo mpya, waandae gar la kubebea mahiti, wamvue nguo mwanangu wamvulishe nguo mpya wampake lipstick wamtie kwenye jeneza nikifika hosptali walikoniitia wanikabidhi mahiti, kwenye landlover na kunielekeza niende nikazike).

Leo hii mida hii usiku WA manane ninaweweseka picha ya kifo Cha mwanangu inanijia naamka nashika simu nakutana na ukatili mkubwa ukifanywa na vijana baadhi kutoka jeshini ila mkuu wangu wa Majeshi umelala usingizi wa pono?

Nimeumia sana naumia sana nikikumbuka yakuwa kifo Cha mwanangu ikulu ilimwelekeza RPC Lindi afukue mwili wa mwanangu uchunguzwe chanzo Cha kifo CHAKE lakini hakufanya hivyo kwa KUSHIRIKIANA na Mr wankyo kwa madai yakuwa aliyekufa amekufa ila wanao ishi waachwe kazini? Hata agizo la ikulu lapuuzwa? ( Najua taarifa kama hii ikimfikia mkurugenzi wa Jamii forums anaweza Lia machozi, Nina hakika andiko langu ili litamfikia atalisoma na atalia machozi mengi na kumwaribia siku ya Leo maana baada ya TUKIO lire KUANDIKwa hapa Moja ya watu AMBAO walinipambania ni yeye kwa KUHAKIKISHA anafikisha taarifa hizo OFISI zote usika,ikiwemo OFISI ya Rais idara maalumu( sitakiwi kutoa Siri ila ukweli utabakia moyoni, juhudi za mkurugenzi HUYU zilikuwa kubwa sana, popote ulipo max Mungu akupe njozi njema ndugu yangu usiku huu, AMBAO Mimi usingizi Sina na nazidi kuukosa ninapozidi KUKUTANA na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto wa kike.

Mkuu wa Majeshi, mkuu wa idara ya usalama wa taifa, mkuu wa polisi amkeni nchi ya Tanzania yaitaji ulinzi dhabiti, taarifa za kutekwa kwa raia sio drama it's real guys

Jitokezeni toeni neno.

Pia soma:
 
Pole sana mkuu

Haya mambo wakuyapigania jeshi la polisi ambalo ni very slack (kwakuwa baadhi yao ni wahalifu).

Ofisi ya DPP nayo ni very weak,

Waziri wa mambo ya ndani ni pambo tu la uzanzibari kuweka akidi sawa (ceremonial) sasa sijui kwanini uwa wanapeana zawadi wizara nyeti (hiyo ni dharau kwa raia).

Waziri wa elimu nae equally hajali

Waziri wa jinsia na watoto pamoja na kuonyeshwa kuguswa na mambo kadhaa ya jamii inaonekana hapati ushirikiano mzuri wa polisi kuingilia kila swala.

Waziri wa habari doesn’t know how to pressure other institutions to be accountable (hawana hizo mbinu za propaganda).

Kwa kifupi ni nchi ya hovyo, una kila sababu ya kufikiria foul play kama awakukupa fursa ya kufanya independent postmortem.
 
Pole sana mkuu. Sijawahi kupatwa na tukio la aina hiyo, lakini nimeumia sana mwanao kufia mikononi mwa vyombo vya dola vinayopaswa kumlinda!

Hata sijui ningefanya nini kitu kama hicho kama kingenitokea ?! Ningeweza hata kuamua kwenda Congo kwa muda, ili nikirudi niondoke na angalau hata mmoja wa waliohusika. Inaumiza sana!
 
Mkuu pole sana, matukio ya ukatili wa kijinsia yapo mengi sana ñakini cha ajabu hatua stahiki hazichukuliwi kwa wahusika. IHii hutokea kwa sababu inategemea tu ni nani kahusika moja kwa moja ama yupo nyuma ya tukio husika.

Wahanga wengi wa matukio ni watu maskini, na wapangaji na watenda uovu huu huwa ni watu wenye fedha za kuhonga ama wenye mamlaka juu ya vyombo vya dola, kiasi kwamba wahanga wa matukio hayo hawawezi kuwafanya kitu chochote kile zaidi kuwalalamika tu.

Wahusiia hulindana ili kuchelewesha hak kutendekai ama kupoteza kabisa ushahidi. Baada ya muda kila kitu kinasahaulika na maisha yanaendelea kama kawaida.
 
Vip ile issues ya mkuu wa mkoa simiyu imeishia wap?
 
Mkuu wewe ni dini gani ?
Kwenye Biblia kuna simulizi kuhusu maisha ya "Ayubu". Jamaa alikuwa na watoto wakiume 7 na mabinti 3 na wote walikufa siku moja kwa uonevu wa Ibilisi.

Ayubu alischosema ni;
"BWANA ametoa, na BWANA ametwaa".

Ni kweli inauma, lakini, wakati mwingine inabidi kumwachia MUNGU.

Hakuna namna ya kuirudisha "jana", jana imepita na mambo yake. It's time to forget the past and move on.

Ukiendelea kuishi kwenye maumivu ya jana utateseka zaidi sababu kesho nayo inakuja na maumivu yake tusiuoyajua. Vua maumivu ya jana, sahau kabisa yaliyopita, angalia mbele, mtumainie MUNGU.
 
Pole sana mkuu

Haya mambo wakuyapigania jeshi la polisi ambalo ni very slack (kwakuwa baadhi yao ni wahalifu).

Ofisi ya DPP nayo ni very weak,

Waziri wa mambo ya ndani ni pambo tu la uzanzibari kuweka akidi sawa (ceremonial) sasa sijui kwanini uwa wanapeana zawadi wizara nyeti (hiyo ni dharau kwa raia).

Waziri wa elimu nae equally hajali

Waziri wa jinsia na watoto pamoja na kuonyeshwa kuguswa na mambo kadhaa ya jamii inaonekana hapati ushirikiano mzuri wa polisi kuingilia kila swala.

Waziri wa habari doesn’t know how to pressure other institutions to be accountable (hawana hizo mbinu za propaganda).

Kwa kifupi ni nchi ya hovyo, una kila sababu ya kufikiria foul play kama awakukupa fursa ya kufanya independent postmortem.
Umeongea vizuri sanaaaaaaaa; lakini hugeandika yote haya; Summary: WEAK PRESIDENT, CORRUPT GOVERNMENT, BANANA REPUBLIC; full Stop. The Head Of State is responsible directly.
 
Mkuu wewe ni dini gani ?
Kwenye Biblia kuna simulizi kuhusu maisha ya "Ayubu". Jamaa alikuwa na watoto wakiume 7 na mabinti 3 na wote walikufa siku moja kwa uonevu wa Ibilisi.

Ayubu alischosema ni;
"BWANA ametoa, na BWANA ametwaa".

Ni kweli inauma, lakini, wakati mwingine inabidi kumwachia MUNGU.

Hakuna namna ya kuirudisha "jana", jana imepita na mambo yake. It's time to forget the past and move on.

Ukiendelea kuishi kwenye maumivu ya jana utateseka zaidi sababu kesho nayo inakuja na maumivu yake tusiuoyajua. Vua maumivu ya jana, sahau kabisa yaliyopita, angalia mbele, mtumainie MUNGU.
Yaani mwa 2024, unasoma hii, inashangaza, huwezi kuelewa kama wewe unajiita binadamu. Yaani hadithi ya Agano la Kale wewe unaichukulia kama ilivyo; sasa kama unaamini hivyo kwa nini unaenda shule? Yaani mtu aue mwanao ati umwachie Mungu? Duuuu. Ni kweli CCM watatawala Milele hii Nchi; maana 99% wanaamini kama wewe.
 
Back
Top Bottom