Sirari, Tarime – Mara
Tarehe
11 Agosti 2025, majira ya saa
8:27 usiku, tukio la kutisha liliripotiwa kutokea katika makazi ya aliyekuwa mgombea udiwani wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Sirari, wilayani Tarime.
Mashuhuda wanasema kundi la watu wasiojulikana, wakiwa na
silaha za moto, walivamia makazi hayo baada ya
kuruka geti na kuanza kumtafuta mgombea husika. Katika harakati hizo, walimkamata
ndugu wa mwenye nyumba na kumchukua kwa nguvu. Tangu siku hiyo, hajulikani alipo hadi sasa.
Tukio hili limeibua hofu na taharuki miongoni mwa wakazi wa Sirari, hususan katika kipindi hiki cha kuelekea
uchaguzi mkuu, ambapo hali ya kisiasa na kiusalama mara nyingi huwa tete.
Mamlaka za usalama bado hazijatoa taarifa rasmi juu ya tukio hili, na juhudi za kumtafuta mtu huyo zinaendelea. Wakazi na viongozi wa kijamii wameshauri vyombo vya dola kuongeza ulinzi na kufanya uchunguzi wa kina ili kuhakikisha usalama wa raia na amani kipindi hiki cha uchaguzi.