Tetesi: Tukio la Simiyu: Chanzo cha vurugu hakijakamatwa

Tetesi: Tukio la Simiyu: Chanzo cha vurugu hakijakamatwa

IHOLOMELA

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2010
Posts
1,807
Reaction score
1,675
Habari Wakuu.

Kama ilivyosikika na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii juu ya tukio la kuvamiwa na kuchomwa moto kwa kituo cha polisi na baadhi ya vibanda vya biashara na nyumba za askari huko Simiyu.

Inasemwa kuwa tayari raia 27 wamekamatwa kwa tukio hilo ila hatujasikia askari waliouwa watuhumiwa wa wizi kukamatwa. Ikumbukwe kwamba, chanzo cha wananchi kuvamia na kufanya uharibifu huo ni baada ya vijana wawili kuuwawa wakiwa ndani ya kituo hicho, wasingeuwawa hizo fujo zisingetokea.

Kwa kuwa hadi sasa hakuna taarifa za kukamatwa kwa chanzo cha vurugu (Polisi), je kuna haja ya kuliomba jeshi la polisi kuwakamata hao askari waliosababisha?

Nawasilisha kwa hatua zenu.
 
Ngoja niwahi siti niwasubiri wengine waje.
 
Kwani kanda hiyo Tarehe 26 ishafika eh?
 
Ni wazi uchunguzi wa kisayansi na majaribio ya maabara ulibaini waliokamatwa tu! Nakupenda TZ nchi yangu.
 
Nchi imefika pabaya inanuka damu !!! Ni muda wa kumwomba mungu sana maana yajayo yanasisimua !!!
 
Sasa naanza kuamini Yale niliyoambiwa baada ya yule mtumishi wa Mungu kutua Tanzania peku peku bila vuatu!
 
Back
Top Bottom