Wakuu kama wote tunavyofahamu, juzi Jumatano majira ya saa 3 hivi usiku Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilitoa orodha ya Walimu waliopangiwa kwenye vituo vipya vya kazi. Ni jambo jema sana kwa wale waliobahatika kupangiwa vituo.
Hata hivyo kuna jambo lisilo la kawaida limejitokeza. Ni kwamba Wahitimu wengi kama sio wote wa Chuo Kishiriki cha Elimu Mkwawa (MUCE) wa mwaka 2010/2011 hawajapangiwa vituo vya kazi. Badala yake waliopangwa ni wale wa 2009/2010 yaani ambao tayri wapo kazini tangu Januari mwaka 2011. Nina wafahamu kwa majina, sura, vitu vyao vya kazi na Chuo walichosoma (MUCE) watu kama 6 hivi ambao tena wamepangiwa upya vituo mbali mbali vya kazi.
Ninayo Maswali hapa kwa Wizara zote zilizohusika na mchakato huo yaani TAMISEMI, MOEVT, PO-PSM na MOF..
1. Muda wote toka wahitimu hawa walipojaza fomu zao serikali haikugundua tatizo hilo?
2. Kama zoezi rahisi tu hili limeshindikana, itawezekana vipi kuondoa hicho kinachitwa watumishi hewa?
3. Je, huu sio mwanay wa Wakurugenzi wa Halmashauri kula fedha za serikali pale ambapo walimu hawa hawataripoti kwenye vituo vyao vya kazi?
4. Tumeambiwa kuwa majina yote ya walimu wenye shahada yanarekebishwa leo ili kuondoa huo utata, je huo sio mwanya wa kukaribisha mazingira ya rushwa/
5. Kuna njia zipi zilizowekwa kuhakikisha kwamba zoezi hili linakamilika kwa wakati li walimu watakaoajiriwa wapate haki yao kwa wakati?
6. Serikali ipo tayari kueleza nini kilipelekea hali hii?
Na mengine mengi