Mr George Francis
JF-Expert Member
- Jun 27, 2022
- 234
- 376
TUKIONA WAGONJWA NA MAITI KWENYE MAJENEZA PIA TUSEME 'ONE DAY YES.'
Tukiona magari mazuri na majumba ya kifahari ya watu tunasema "ONE DAY YES." Tena tukiamini kwamba ipo siku nasi tutafanikiwa kumiliki mali kama ambazo wanamiliki wengine.
Tukiona wagonjwa na maiti kwenye majeneza basi pia tunapaswa kusema "ONE DAY YES." Tena tukiamini kwamba ipo siku nasi tutakuwa wagonjwa na siku itafika pia nasi tutaitwa maiti kama tunavtiwaita wengine.
Maandiko katika kitabu cha AYUBU 14:1,2 neno la Mungu linasema
"Mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke
Siku zake za kuishi si nyingi, naye hujaa taabu.
Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa;
Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe."
Kama umezaliwa na mwanamke kama nilivyozaliwa mimi basi utake usitake hii lazima na wala sio ombi sote ni "ONE DAY YES.
Sisi ni wenye kurejea na kwake aliyetuumba tutarejea. Hata uwe mwamba kiasi gani hapa duniani lakini "ONE DAY YES."
Tunaposema "ONE DAY YES" kwenye kupata majumba, pesa na magari, hatuishii tu kusema bure bali ni lazima tufanye jitihada ya kuzipata la sivyo kusema tu "ONE DAY YES" itakuwa ni kazi bure na utazeeke bila chochote.
Kwa maana hii kumbe kusema tu "ONE DAY YES " unapoona au kuwaza kuhusu ugonjwa au kurejea kwa Mwenyezi MUNGU ina maana ya kuwa na maandalizi juu ya jambo husika.
Maandalizi ya siku ukifikwa na ugonjwa Je utakuwa na pesa ya kumudu gharama za matibabu? Kumbe inabidi uweke akiba.
Lakini pia Maandalizi pia ya siku ukiondoka duniani njia yako ni ya peponi au jehanamu? Kumbe inabidi kuacha dhambi na kutenda matendo mema ili kuwa salama siku ya mwisho.
Mimi sio mkamilifu na wala sio mwema sana lakini nimeona tukumbushane. Nakuhusia na kuihusia nafsi yangu, "ONE DAY YES."
Ahsante kwa muda wako kusoma andiko hili. Mwenyezi MUNGU akubariki sana.
It's Me Mr George Francis