Tukisema Mashabiki wa Yanga SC wanahitaji mara kwa mara Kuonana na Madaktari wa Magonjwa ya Akili muwe mnatuelewa tafadhali

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2015
Posts
8,018
Reaction score
16,802
Kauli Jumuishi za Mashabiki wa Yanga SC kabla ya Kucheza Leo Mechi yao na Mbeya City FC

"Hakuna wa Kumzuia Yanga SC kwa sasa iwe katika Viwanja vibovu vya Mikoani au vizuri vya Dar es Salaam. Leo tunaenda Kuiacha zaidi Simba SC kwa Alama 10 na tukimfunga Mbeya City FC leo tayari tutakuwa na uhakika wa Ubingwa kwa 75%. Mbeya City FC akitoka Sare au akitufunga Yanga SC leo tunakunya kutoka Avic Town Kigamboni hadi Mo Arena Bunju. Y

anga SC hii ya sasa chini ya GSM haina Wachezaji wa kutoka Sare au Kufungwa na Mbeya City FC na hata Vilabu vingine vyote kwani tumejipanga na tunajitosheleza kwa kila Kitu na ndiyo Timu Tajiri Tanzania nzima
"

Kauli Jumuishi ya Mashabiki wa Yanga SC mara baada ya kutoka Sare na Mbeya City FC Leo

"Mpira una Matokeo matatu Kushinda, Kufungwa na Kutoka Sare. Kama Mtani alifungwa na hawa hawa Mbeya City FC unadhani Sisi Yanga SC kutoka nao hii Sare tusimshukuru Mungu? Wachezaji wetu wametuangusha sana halafu tunauomba Uongozi uwe Wakali kwa Wachezaji kwani wengi wao huwa tunakutana nao katika Majumba ya Starehe.

Tayari zile Ndoto zetu za kuwa Mabingwa zinaanza Kufifia kwani kwa Simba SC na hivi walivyojipanga hizi Alama 8 wanaweza Kuzifikia na Kutuacha mwishoni tukabaki Kuchapana Bakora wenyewe kwa wenyewe
"

Wana Yanga SC wahini mkatibiwe Akili.
 
Subiri leo upakatwe na mbeya kwanza halafu ndo uje tuongee bahati nzuri mbeleko haipo
 
Mimi nadhani wewe ndiye unayetakiwa kwenda kupimwa akili. Kwa sababu unafahamu fika Yanga haipati ushindi nje ya uwanja! Isipokuwa ni ni baada ya dk 90 kumalizika.

Sasa ulitaka tuseme kwamba Yanga inaenda kufungwa kama timu yako ya simba inayo fungwa fungwa hivyo? Sisi mashabiki ni jukumu letu kuipa hamasa timu yetu, kama na nyingi mnavyo jitahidi kujipa moyo wa kuwa Mabingwa msimu huu!

Jambo ambalo haliwezekani hata kidogo.
 
Team kubwa viongozi wake wapo kwenye vikao na wakubwa wenzao. Na wanachangia maada

Champion ship
 
Unawasemea. GENTAMYCINE una tatizo na chuki na Yanga
 
Ukiona unaongelea sana usichokipenda jua unakipenda na kukitamani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…