Rare Sapphire
JF-Expert Member
- Jul 24, 2021
- 590
- 1,648
Ukiuliza watu wanaomiliki leseni za udereva walipata vipi leseni zao, asilimia kubwa watakwambia nilipiga mishe nikapita huku na kule nikapata leseni yangu. Wengi wa madereva hawa wanaomiliki leseni hizi hawajawahi kupata mafunzo rasmi ya udereva, jambo linalochangia kuwa na madereva ambao wawajui lolote kuhusu taaluma hii.
Unakuta mtu ni dereva wa chombo fulani cha usafiri lakini hata alama za barabarani tu hajui zinamaanisha nini. Mara nyingi watu hutafuta jamaa zao wanaojua kuendesha chombo husika, anamfundisha siku mbili tatu, akikariri vizuri basi anaingia barabarani halafu ndio unafuata mchakato wa kufanya mishemishe ili apate leseni. Jambo hili linasababisha matatizo mengi sana ikiwemo ongezeko hili la ajali tunalolishuhudia kila kukicha.
Je, tukisema leo tufanye jaribio kwa wamiliki wote wa leseni za udereva, unafikiri wangapi wataendelea kumiliki leseni zao?