Tukiwajibika kwenye madini na Tehama, Tanzania itasonga mbele
Abeid Othman
Kwa mujibu wa kamusi kuu ya Kiswahili toleo la pili la mwaka 2017, neno uwajibikaji linatokana na kitendo wajibika, ambalo kamusi hiyo imelitafsiri kama tekeleza jambo linalokulazimu kulifanya.
Ni vigumu mtu binafsi akapiga hatua bila kufanya yale yanayomlazimu kufanya. Vivyo hivyo kwa taifa lolote lile, lisipofaya yanayopaswa kufanywa, basi lisahau maendeleo.Hiki ndicho kinacholigharimu Taifa letu la Tanzania.
Moja ya kasoro yetu kubwa ni uwajibikaji mdogo katika ngazi mbalimbali kuanzia mtu binafsi na taifa kwa jumla.
Andiko hili litaangazia namna uwajibikaji usioridhisha hasa katika sekta ya madini na Tehama na namna unavyotufanya tubaki nyuma kimaendeleo licha ya ukweli kuwa taifa sasa lina umri wa zaidi ya nusu karne kama taifa huru.
Lakini uungwana si kuonyesha mianya tu, andiko litajaribu kutoa mapendekezo ya namna mianya hiyo inavyoweza kuzibwa na hatimaye kuipaisha nchi yetu kimaendeleo.
Nitoe mifano. Nimesema awali taifa lina miaka zaidi ya nusu karne lakini eneo nyeti lenye fursa kubwa za kuinua uchumi wetu yaani madini limehodhiwa na wageni.
Kila kona ya nchi migodi mikubwa inamilikiwa na kampuni za nje na hata pale tulipojithd kujitutumia kushiriki ktk utafutaj wa madimi hayo basi ni kwa ubia na kampuni hizo tena tukiwa na hisa pungufu kwa mfano mgodi wa almasi wa Williamson uliopo Mwadui, Shinyanga, Tanzania ina asilimia 37 za hisa. (Mwananchi, Novemba 16, 2022- Utata hisa mgodi wa Mwadui kuuzwa).
Kwa nini kama nchi tunashindwa kusimamia na kufaidi wenyewe utajiri huu? Majibu yanaweza kuwa lukuki lakini jibu moja kubwa hatuna wataalamu bobezi na wa kutosha.
Kwa kukosa wataalamu wa sekta hii kwa ujumla wake kuanzia uchimbaji, mbinu za kimasoko, sheria na hata siasa zake katika soko kimataifa, Watanzania tumekuwa tunaburuzwa.
Sote tunakumbuka namna Rais wa awamu ya tano, hayati John Magufuli alivyokuwa mara kadhaa akieleza namna Tanzania ‘inavyolizwa’ na wawekezaji kutoka nje kwenye sekta ya madini.
Kuna mahali kama taifa hatujawajibika kuandaa wataaamu wazawa wa kulinda hazina hii.
Na kibaya zaidi sioni kama kuna mkakati wowote wa kuandaa aina hiyo ya wataalamu ili angalau miaka kadhaa ijayo, Watanzania watamalaki kwenye sekta hiyo.
Hata kama mwelekeo sasa ni ushirikiano kati ya sekta binafsi na serikali (PPP), basi ni matarajio yangu sekta binafsi hiyo iwe ni ya wazawa na sio kama ilivyo sasa kwamba kwa sehemu kubwa sekta binafsi inayowekeza kwenye migodi mikubwa ni ile ya wawekezaji kutoka nje.
Ni kweli wanalipa kodi, ila ukweli ni kuwa wanachotengeneza kama faida na kupeleka kwao ni kikubwa kuliko kodi tunayowatoza.
Uwajibikaji kwenye Tehama
Mfano huu wa kutowajibika kwenye madini, ndio unaotutafuna hata katika maeneo mengine nyeti yanayosukuma uchumi wa dunia, ikiwamo sekta ya teknolojia, habari na mawasiliano (Tehama).
Leo nani asiyejua kama Tehama ndio injini ya uchumi wa dunia. Tunapozungumzia dhana kama Maendeleo ya Tano ya Viwanda, Tehama huwezi kuipa kisogo.
Mifumo yetu ya kielimu ni kwa namna gani inaandaa wasomi wa kuwa mabingwa katika maeneo kama akili bandia (AI), msimbo (coding), uchambuzi wa data (Data analysis) na aina nyingine za ujuzi wa kiteknolojia ambazo ndio nguzo ya maendeleo ya dunia hivi sasa?
Natambua upande wa Tehama wapo Watanzania wachache waliojitutumua kiubunifu na kuwa mfano wa kuigwa. Lakini je, wana sapoti ya serikali?
wamewekewa mazingira wezeshi ya kuweza kufanya makubwa zaidi kwa taifa lao?
Tufanyeje?
Andiko hili linahimiza uwajibikaji hasa kwa ngazi ya kitaifa kupitia serikali na mamlaka zake mbalimbali, ili hatimaye tuweze kuifikia ile azma ya Dira ya Maendeleo ya 2025 na 2050.
Lakini ili tufike huku kwa kuwa nchi ya uchumi wa juu kati na hata zaidi, lazima tuwe na wasomi na wataalamu wa kimkakati, katika sekta za kimkakati na watakaondaliwa kimkakati na kuthaminiwa.
Kwa mfano, Serikali kwa utaratibu itakaouweka, inaweza kuchagua wanafunzi kwa idadi maalumu kila mwaka katika ngazai mbalimbali ikawasimamia ipasavyo na kuwasomesha katika fani zote muhimu kwa mandeleo ya Taifa.
Tusiache kwa mfano wanafunzi vinara wa sayansi katika mitihani ya kidato cha nne na sita wakapotea tu kusikojulikana au tukawaachia wazazi wao kujua mustakabali wao wa kielimu.
Angalau idadi hii ndogo ya wanafunzi hawa vinara, ikawa chini ya uangalizi wa Serikali kwa kusomea fani za kimkakati kama Tehama, madini na nyinginezo ambazo ndio injini ya maendeleo katika dunia ya sasa.
Kupanga ni kuchagua, hebu tuchague utaratibu wa kuchukua wanafunzi vinara katika ngazi za chini, tuwalee na kuwasimamia hadi elimu ya juu huku wakisomea fani ambazo zina mchango katika kufikia dira ya taifa letu.
Tukumbuke kuwa hawa tutawasomesha kimkakati na kwa gharama, hivyo lazima tuwe na mifumo ya kuhakikisha baada ya elimu zao tunawatumia kimkakati huku tukiwajali na kuwajengea mazingira wezeshi ya wao kufanya makubwa kwa ajili ya Taifa lao. Tukiwajibika hili linawezekana.
Abeid Othman ni mkazi wa Dar es Salaam na anapatikana kwa simu 0754990083. Barua pepe: abeidothman@gmail.com

Upvote
2