Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Mtazamo wangu;
Kama tukichukua matajiri wakubwa 1000 wanaotokana na umiliki wa viwanda; viwe vya kati au vikubwa.
Pamoja na matajiri 1000 wanaotokana na kilimo; wakapewa sera nzuri ya kodi, sera nzuri kwa masoko ya nje, sera nzuri katika kuagiza vipuli, na wakawezeshwa kwenye mitaji ya kutosha n.k
Ndani ya muda mfupi, tatizo la ajira litakuwa limeisha na uchumi utakuwa kwa kasi sana.
Kitakachotokea ni nini?

- Viwanda vikubwa na vidogo vitakuwa vingi
- Upatikanaji wa bidhaa utakuwa mkubwa
- Fedha za kigeni zitakuwepo za kutosha
- Mashamba makubwa na ya kisasa kila kanda yatakuwepo
- Watu wengi sana wataajiriwa
- Ukuaji wa teknolojia utakuwa kwa kasi
- Utaongeza ukuaji katika sekta zingine
- Mapato ya serikali yataongezeka
- Hakutokuwa na njaa
- Uagizaji bidhaa nje utapungua na kuimarisha uchumi n.k