Mazingira ni eneo lote wanamokaa viumbe, akiwemo mwanadamu pamoja na viumbe visivyo na uhai. Viumbe hai hivi pamoja na vile visivyo uhai hutegemeana ama kwa njia chanya au hasi. Katika kupigania kwao maisha, ama kwa makusudi au bila makusudi huyaboresha mazingira na kuwaletea ustawi au huychafua na kuwapelekea didimio. Cha kutia akilini zaidi ni kwamba anayestawisha au anayefuja ni binadamu, khalifa wa sayari hii kama Mola alivyosema.
Zanzibar ina historia refu hapa duniani kwa kubahatika kwake kuweko eneo zuri kijografia- hali ya hewa mwanana, tofauti na ile ya joto la Majangwani au baridi ya Ulaya. Imejaaliwa kuweko masafa mafupi kutoka mama yake (Afrika) aliyekuwa na twika za mali na hidaya kama vile vito na mali ghafi za asili ya wanyama na miti. Iliwavutia watu wa mabara mengine kuja kwa ajili ya biashsara na mastakimu. Vizazi vya waliotajwa hapo juu ndio Wanzanzibari wa sasa. Tukumbuke kwamba walipokuja walikuwa wamebeba mchanganyiko wa mema na mabaya ambayo yalinyika na mema na mabaya ya wenyeji waliokuwepo wakati huo.
Inawezekana sote tunaelewa kwamba kichwa cha nchi ni mji wakemkuu. Kwa mfano, Tanzani ni Dodoma baada ya kuhamishwa kutoka Dar es salaam. Kwa Zanzibar ni Mji Mkongwe uliobatizwa jina la Stone Town kwa maana ya Mji wa Mawe. Jambo katika karne ya 19.
Maandishi ya kihistoria yanatuambia kwamba Mji Mkongwe kijografia vilitenganishwa na Pwani Ndogo au Pwani Chafu, kama wengine walivyozoea kuuita. Ilikuwa na upana wa takriban mita 100 na urefu wa kilomitamoja. Lau si ule mlizamu wa ardhi pale Kizingo, Mji Mkongwe ungalikuwa kijisiwa cha pekee, pembeni mwa Unguja.
Wakaazi wa siku hizo hawakuwajibika kwa kuichafua bahari hiyo ndani ya mji wao na kupelekea kubatizwa jina hilo baya.
Ama kweli penye wengi pana mengi. Eneo lilikuwa chanzo cha kila aina ya maudhi- mizoga na punda, mbwa na wakati mwengine binadamu! Mizoga hii pamoja na takataka nyeginezo zilihanikiza uvundo uliokaribia kuzing’oa pua za waliokatiria.Waswahili wana msemo, ’Avumaye baharini ni papa, kumbe wengine wapo’. Marehemu Mzee wangu alizoea kusema ‘Kutu kubwa ni ya mgeni’. Misemo hii miwili inatusuta tujiulize je hawa waliokuja Zanzibar kutoaka mabara mbali mbali ndio waliochafua mazingira yetu kama malipo ya nuksani baada ya kuwapokea kwa ihsani? Au na sisi wenyewe lulivaa njuga katika kukoleza nuksani hiyo? Jibu tunalo sisi wenyewe hata tukijificha njuguni.
Katika juhudi ya kuondosha balaa la Pwani hiyo serikali ya kikoloni ya Kiingereza ilipitisha fatwa ya kuifukia hatua kwa hatua kuanzia mwaka 1890 mpaka ukabakia mto mwembamba uluioanzia funguni, ambapo juu yaka palijengwa madaraja yaliyozaa jina la Mtaa wa Darajani. Mwisho na mto nao ukafukiwa kwa kujengwa barabara ya Hollis (sasa Benjamin Mkapa).
Wakati karne ya 20 inatuaga Mzee mmoja wa Kizungu alitembelea Mji Mkongwe. Alijikaga kwa umri wake mkubwa akieleza kwamba wakati yupo chini hapa akina Mzee Ali Hassan Mwinyi walikuwa katika shule za msingi, yaani watoto wadogo! Katika kwenda mbele alibinya pua yake akamwga kimombo labda kwa kebehi, ‘hm the town is still stinking! Yaani “mji huu bado unanuka tu”.
Kadhia ya Pwani ilituonesha ya Musa kumbe kuna ya Firauni yaliyokuwa nanakuja (astaaghafirullah), tufuatane mguu kwa mguu, tukayaone.
Mtu na akili yake anakwenda kujisaidia haja ndogo kwenye uchochoro katika Mji Mkongwe wakati wa usiku, pahala ambapo kukicha tu ni mapito ya watu wengi. Akianzisha mmoja kituko hichi na wengine hufuata mfano wake na hata wengine kudiriki kwenda haja kubwa kwa vile tu usiku ni nguo, haonekani. Walisahau msemo kwamba ‘usihadaliwe na usiku wa giza ukanya njiani’ Hawa si makosa yao peke yao bali na mamlaka za miji zinapokosa kuweka vyoo vya umma. Unajua unapobanwa na haja akili hukuruka mpaka uitue.
Pale Forodhani penye Bustani ya Kumbukumbu ya wafalme wawili (Geoge V wa Uingereza) na (Khalifa bin Haroub wa Zanzibar) ni pahala pa watu wengi wanaokuja kupunga upepo. Hapo kale kulikuwa na choo cha umma lakini miaka ilivyosonga mbele kikageuzwa Ofisi biafsi ya kusaidia watalii. Wengi wetu tulisema, lo salalaa! Kauli hiyo ilitua juu ya nyoyo tiifu za Serikali yetu. Hivi sasa vimerudia matumizi yake kama vyoo, ingawa kwa malipo madogo. Si haba mtu apatapo hushukuru. Wapo walowajibika kuyafanya mazingira yawe ya uhakika.
Mtu na fahamu zake anweka vitu visivyofaa katika michilizi ya maji taka na kupelekea kuziba kwa michilzi hiyo na maji ukiyazuia njia yake hujia mwilini. Hali hii hujitokeza karibu kila pahala tena mara kwa mara. Wakati mvua inaponyesha katika Mji Mkongwe na viunga vyake karo za majumba hufufurisha maji najisi yanayozagaa juu ya sakafu za mji badala ya kupenya chini kwa chini kwenye njia zake. Sisi tutokao nje ya mji hutubidi kukunja suruali zetu mara tu tunapoingia mjini. Oho! i likuwa iwe kinyume chake!
Mtu anayeweza kuitwa dada au kaka, mama au baba, bibi au babu anakula karaknga za kuchemsha na maganda anayatupa chini ya kiti chake. Na iwapo ni za kukaanga huzifikicha kasha akazipuuliza ‘fyu’, maganda yakaenea kwenye deki, kisa utingo hamuoni. Na kubwa zaidi wako wanaodiriki kula miwa, machungwa au hata ndizi na maganda wakayarembea dirishani kama yuko ndani ya daladala, na kama yuko nje havimshughuilishia hutafuta pahala pa kusitiri taka hizo. Huziacha papo hapo au kuzitupa ovyo!
Mwengine atapita na gari lililobeba kifusi, mchanga au saruji bila ufuni blangeti nyuma yake ikiwacha kiwingu kizito cha vumbi mithili ya roketi inapofyatuka kuelekea anga za juu, Vumbi hili huleta taharuki kubw njiani hususan kwa wenye matatizo ya kupukuwa. Alhamdulillah vyombo vya dola vimeweka kanuni kufunika malighafi hizo wakati wa kuzisafirisha laikini kiumbe mzito, wengi hawafuati.
Baadhi ya magari ya kutapisha karo pamoja na watapishaji wa kutumia misuli wanaojuilkana kama wazamialulu hutapakaza matapishi hayo musimostahiki na maradhi yakatembea kama ifuatavyo: mtoto anadunda mpira wake unabeba vimelea na kurudi mikononi na. Anakutana na andazi analila bilaya kunawa. Maradhi yanaingia tumboni, anaugua. Goli la kwanza. Anawaambukia wenzake, akiwemo jamaa wa wale watapishaji wa karo, goli la pili, la tatu na kuendelea. Maradhi lazima yadhibitiwe, kuyaeneza ni sawa na kuweka mtaji ambapo hasara wala sio faida yake itaenea kwako na wengine.
Sasa ni muhimu kila mmoja katika jamii ajitahidi yeye mwenyewe na kuwasidia wengine vikiwemo vyombo vya dola kuyatunza mazingira yetu ili tuishi kwa salama na amani.

Upvote
1