Ukweli ni kwamba tunaishi kwa kubahatisha bila kujua hatima yetu itakuwaje huko mbeleni.
Ninachojua nchi nyingi Ulaya na America, wao kwa kulijua tatizo hili basi wazee wanapofika umri wa kutojiweza wanawekwa kwenye quarters zao na huko kuna wangalizi maalum.
Hapa kwetu hakuna hilo. Ukimuuliza mzee akiishiwa nguvu kila mmoja ana jibu lake mwenyewe.
Kuna majibu kwamba watoto watakutunza. Lakini huko sasa hivi ni kubahatisha kwani huyo mtoto huna hakika atakuwa katika hali gani au nafasi gani katka dunia hii. Na anaweza akafa vilevile. Pia wategemezi wa hali hii inabidi sasa ukizeeka unyenyekee sana hao watoto ata kama unanyimwa stahili zako, maana wanaktunza.
Mimi nadhani tunajidanganya kutoliona hili kama ni tatizo. Leo tunachemka, tunabinyeza keyboard lakini ukweli ni kwamba tutazeeka na tutaishiwa nguvu. Je, tutaishije kipindi hicho.
Nimetoka majuzi kumtembelea shangazi yangu. Utotoni pale kwa shangazi kulijaa watu wa kila aina na kulichangamka kwa shughuli mbalimbali. Leo nimeguswa kuona shangazi yuko peke yake na anamuuguza mume wake kama vile hana watoto wakati ana watoto wanne wakubwa na kila mmoja anasema yuko bise na familia yake!
Shangazi anasema walitumia akili sana kujenga nyumba ambayo wameweza kuweka wapangaji ambao binafsi niliona wanamsaidia kumuuguza yule mume wa shangazi! Bila hivyo basi ina maana shangazi angekaa bila kupangisha basi angekuwa anauguza mwenyewe.
Wakati mnaleta maoni yenu, mimi wazo langu ni kwamba tujipange kuleta system kama ya Ulaya niliyosema. Walioko Ulaya watueleze inafanya kazi kwa kiasi gani. Kama ni kukatwa hela ili zitumike kukutunza uzeeni basi ni heri hizi pensheni ziwe zinalenga huko.
Bila kufikiri hivyo, basi ukweli ni kwamba kizazi cha wazee wa sasa hivi kina nafuu lakini kizazi chetu na uchumi mbovu kila waka sijui hali itakuwaje.
Nawasilisha.