Nikiwa kama mwana chama halali wa CCM nitabaki kusimama kwenye kanuni ya chama inayo sema kuwa ( nitasema ukweli daima fitina kwangu ni mwiko ).
Mimi siwezi kukaa ndani ya chama kwa kujipendekeza iwe ni kwa katibu mkuu , katibu mwenezi, au hata mtu yeyote ndani ya chama.
Ndio nasema hivyo kwa sababu, kwa muda mrefu sasa chama changu CCM kimeshutumiwa kwa tuhuma ambazo ni kubwa kuwahi kutokea hapo nyuma.
1: Kuheshimiana hakupo tena Ndani Ya Chama, Nasema Hivyo Niki Maanisha Kuwa Ndani Ya Chama Sasa Faragha Haipo ,Kila Mtu Sasa Ni Mbabe Kwa Mwenzake, Hivi Ilikuwa Ni Halali Kwa Katibu Wetu Mkuu Kumuita Mwanachama wetu mahiri na mtiifu ndani ya chama kwa kejeli na dharau kiasi kile ?
Namaanisha dharau alizo zitumia kwa kumuita mh Bernard Membe , tena bila ya aibu anasema kuwa hakuwa na namba za simu za Mh Membe , hivyo akaamua kutumia vyombo vya habari kumuita, tena sio kwamba alitumia chombo kimoja kama labda TBC , bali aliamua kufanya press conference.
Nasema hii ilikuwa ni dharau iliyo pitiliza.
2: Kwa muda mrefu chama chetu kimeshutumiwa kuwa kinahusika na kuwanunua Madiwani na Wabunge kutoka vyama vya upinzani, tena mbaya kabisa kukatokea katabia ka kuwarudisha hao hao kugombea kwenye nafasi walizo jiuzuli, hili nalo likaleta kaukakasi ndani ya chama.
3: Kama chama tumepoteza malengo yetu, tulikuwa na Sera ya Tanzania ya viwanda, ghafla upepo ukageuka na kuingiza Sera tofauti ya Tanzania ya kuwa vyama vya upinzani. Sasa najiuliza hivi kama chama dira yetu ilikuwa nini kujenga viwanda ili kuwaletea vijana wetu fursa za ajira au kuuwa vyama vya siasa ?
Wakati vijana wetu wengi wamemaliza vyuo vikuu wamekaa mitaani bila hata ajira , huku chama kina hangaika na njama za kumfunga Mbowe na Esta , bila ya sababu zozote za maana , zaidi ya fitina .
Hakuna jitihada zozote za kuwa wezesha vijana kupata mikopo ili basi angalau wajiendeleze kibiashara , lililo baki ndani ya chama chetu ni kukodoa macho kwamba leo Mh Zitto Kabwe atasema nini ili tumuweke ndani.
4: Mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu ikageuzwa kuwa swala la kisiasa, hivi kulikuwa na umuhimu gani kwa Polepole kutangaza kuwa chama kinatoa mikopo kwa ajili ya wanafunzi wanaosoma elimu ya juu, hivi swala la elimu lilikuwa ni jukumu la chama au serikali ?
Yapo mengi ila la msingi tunahitaji kiongozi atakayeleta mshikamano kwa watanzania wote bila ya ubaguzi kwa kisingizio cha utofauti wetu kupitia vyama vya siasa.
Hatumuitaji kiongozi anaye tubagua na kujenga chuki miongoni mwetu eti kwa sababu tu tuko vyama tofauti vya kisisa.
Hii Tanzania ni yetu sote , tushikamane kwa pamoja na tuwakatae viongozi wabaguzi wa namna yoyote ile.
Tunahitaji viongozi watakao heshimu sheria zetu za nchi tulizo jiwekea kama watanzania ili zituongoze.
Wote ni wahanga , natume yaona kwa macho yetu, chonde chonde chonde 2020 tusirudie makosa. Kama mtu amepewa nafasi na akashindwa hakuna haja ya kumuongezea muda atupishe .
Na ndio maana nasema kama atakuwa Membe au Lissu tuko tayari kumpokea.
Sent using Jamii Forums mobile app