demigod
JF-Expert Member
- Jan 2, 2015
- 8,292
- 15,250
Nimepata nafasi mujarabu kabisa ya kuketi kwenye kiti cha VVIP nikishuhudia mtanange wa mnyama mkali yaani Mwekundu wa Msimbazi alivyomgalagaza Topolo la kirundi. Kwa kiasi chake ninaweza kusema kuwa tupo vizuri, hatuja piga hatua sana kwenye suala la ubora ukilinganisha na kikosi kilichomaliza msimu. Kwenye ligi hakuna mpinzani ila wasiwasi wangu ni kwenye michuano ya kimataifa.
Licha ya kushinda kwa idadi kubwa ya mabao, bado hapakuonekana na ubora na utulivu kwenye safu ya ulinzi. Ukizingatia hata timu yenyewe tuliyoshindana nayo ni ya daraja la chinHata hivyo nimeona sababu ya kutafakari upya kuhusu timu wageni tunazo zialika kwenye tukio hili muhimu, maana mara zote tumeshuhudia timu dhaifu tu zikialikwa ili tutengenezewe imani ya kwamba timu yetu ni bora. Hilo viongozi maomba walifanyie kazi.