SoC03 Tukope tuwekeze la hasha

SoC03 Tukope tuwekeze la hasha

Stories of Change - 2023 Competition

File Suleiman

Member
Joined
Jun 5, 2023
Posts
9
Reaction score
7
Kuna mjadala mkubwa sana hapa nchini haswa kuhusu serikali kukopa na kupokea misada kutoka nchi tofautitofauti kama Amerika, Uchina, Falme za Kiarabu na Umoja wa Nchi za Ulaya, mjadala ni mkali na kila msomi na asiesoma huchambua kwa anavyoelewa wapo wanaopinga na wapo wanaounga mkono serikali kukopa na kwa andiko hili wote wapo sahihi mana wote wanaongea kutoakana na mitazamo yao na kwa mustakabali wa nchi la hasha wawe wanaongea kwa ajli ya matumbo yao.

Andiko hili linaanza na swali ambalo je Tanzania tunaweza jiendesha bila mikopo?
Jibu ni hapana tunaitaji mikopo, kwa hali tulionayo Tanzania hatuwezi jiendesha kikamilifu bila ya mikopo, hakuna nchi isiokopa, nchi zote zinakopa ila tunakopa kwa matumizi yapi?? na hapo ndio kiini cha andiko hili, hatukataii kukopa ila tunakopa kwa ajili gani?, tunakopa ili tufanye nini?? na tunavyokopa tunamini kwamba mikopo tunayoikopa itakua chachu ya maendeleo?, na kwanini tunakopa?, haya ni maswali ambayo lazima tujiulize mnoo kama wanachi ila pia watendaji wa serikali na viongozi wakuu haya maswali ni muhimu wajiulize katika kukopa.

Tukope tuwekeze la hasha
Kwanini andiko likawa na kichwa hichi cha habari? Mana yake andiko hili linakubali serikali ikope ila ikope kwa kuwekeza na je kukopa kwa kuwekeza ni aina gani?. Kukopa kwa kuwekeza ni serikali kuchukua mikopo na kuiwekeza katika miradi ya kimaendeleo ambayo iyo miradi kwa miaka ya badae italeta tija na kuwa sehemu ya mapato ya nchi yetu au ikasisimua ukuaji wa uchumi wa nchi yetu aina hii ya ukopaji ndio ukopaji wenye tija na faida mfano tukope tujenge reli ya kisasa ambayo kwa miaka ya badae itakua ni chanzo cha mapato kwamba huu mradi utakua unazalisha tutapata pesa na tutasisimua maendeleo hapa nchini, kama tunakopa basi tukope tujenge miradi ambayo kwa badae ni faida kwetu kama madaraja makubwa ambayo yatasaidia kuiunganisha nchi, tujenge mabarabara kama tunakopa basi tujenge miradi ya umeme yani kama tunakopa basi tuboresha sekta ya mawasiliano na uchukuzi kama tunakopa basi tukope kwa kuwekeza katika miradi ambayo kwa badae na sasa itakua ni sehemu kubwa ya kukuza uchumi wetu na pia itakua sehemu kubwa ya vyazo vya mapato katika taifa letu na zaidi ya hapo ni la hasha hili andiko linapinga aina iyo ya ukopaji.

Ukopaji gani wa la hasha?
Andiko hili la onya juu ya aina hii ya ukopaji moja serikali kukopa au kupokea misaada ambayo inaenda kutumika katika matumizi ya kawaida au matumizi yasio zaa au katika matumizi ya umuhimu ila hatuitaji kukopa kwa mfano kwanini serikali ikope au ichukue pesa za msaada kwa kujenga vyoo vya shule au madarasa au vitanda na madawati?? hili jambo ni aibuu narudia ni aibu ni vyema serikali ilalaimikiwe kutoza wanachi wake kodi ili iweze kujenga na kusimamia vitu kama ivi kwa pesa ya ndani, serikali kukopa ili kulipa mishahara wafanyakazi narudia hili pia hapana, nini mana ya uwepo wa wizara ya fedha na mipango nini umuhimu wa kukusanya kodi kama tunakopa au kupokea misada ya ujenzi wa vyoo? Madawati? Hapana jamani hili halikai sawa hata kukopa kujenga hosptali na shule pia hapana kwani kodi tunazokusanya zinafanya kazi gani? hadi tupokee misaada na mikopo kwa kununua dawa au kununua vitanda vya hospitali? Hapana huku sio mana nzuri ya kukopa naandika haya bila haya wala aibu tukumbuke ivi vitu tunaweza kufanya wenyewe na pia tukumbuke tunakopa na tunaitaji rudisha ivyo tutakua kila siku tunakopa kwa matumizi yasio zalisha hata kama yana umuhimu kiasi gani.

Kwanini mikopo ya la hasha ni la hasha?
Nadra sana uende banki za kawaida tuu izi useme naomba kukopa sababu mama yangu mgonjwa anataka kufariki hawawezi kukupa aina ya mkopo huo bali mikopo yote ni ile ya uzalishaji banki zitatoa mikopo kwa wajasiriamali, wafanya biashara wenye biashara za kueleweka ndio sababu hata wamachinga hawana mkopo banki mana yake nini?? mana yake wanajua kabis hela wanazikopa zinaenda zalisha na wakopaji watarudisha na hii ndio mana ya kukupoa ila serikali haitakiwi kukupa kama baba au mama wa familia anaenda kukupa unga au sukarli dukani yani mangi au mpemba nikopeshe kilo mbili za mchele kesho nakurudishia kwa miaka mingi serikali imekua aina ya ukopaji huu ambao hauna faida kwa Taifa letu.

Mikopo inatutia unyonge, uoga na unyenyekevu kwa tuliowakopa, taifa linapojilimbikizia mikopo na misaada tunajenga nidhamu ya uoga na unyeneyekevu kwa tunaowakopa na hii inafanya tuzidi kuwa tegemezi na tusiochakata katika njia gani bora za kujiendesha akili zetu zinadumaa tukiamini kesho tutaenda kwa mangi kuchukua mchele kilo mbili, mtokeo yake hatuna sauti kwa wahisani wetu hata wakitaka kufanya tusichokipenda hatuna sauti ya kukataa bali tunaugulia moyoni na rohoni sababu uwezi maka na kukoroma kwa mtu anaekudai pia utampingaje mtu ambae ushakua tegemezi kwake? ivyo basi kuepusha hadha hii ni bora kama tunakopa basi tukope kwa ajili ya kuwekeza katika miradi ya maendeleo katika vitu vitasisimua ukuaaji wa uchumi wetu.

Mwisho ni kumbushe kua nchi kama nchi inahitaji mikopo inahitaji sana kukopa ila tuweke viwango vya ukopaji na sioni sababu ya kuchukua misaada ambayo nchi kama nchi inaweza kuihimili, tukumbuke misaada tunayopewa iwe ya bure au mikopo ni hela za wanachi wa nchi husika, ivi kweli Marekani au China kodi za raia wake anazotoza ni anazigawa bure tuu yani bure tuu sababu kuna nchi inaitwa Tanzania inahitaji mashimo ya choo? au Tanzania ni rafiki yetu mzuri kisiasa na kidipomasia basi tumfadhili hela ya bajeti yake ya mwaka 2023/24 yani raia wao watoe kodi kwa ajili yetu bure bure ivi inaingia akilini? jibu ni hapana lazima izo hela wanazotupatia zitarudi ivyo miasaada sio mizuri bora tukope kuliko kukubali msaada mana lazima kuna kitu wanakiitaji kama leo tuu hapa nchini tunalalamika kodi na utitili wa kodi alafu Tanzania ichukue kodi zetu ziende igawia Marekani iwape bure tuu ivi tutakubali??, Jibu ni hapana sasa kwanini nchi zilioendelea zifanye ivyo kwa nchi zinazoendelea? Mana yake wanakitu wanakitafuta ivyo tuwe macho na misaada.

Kwa kumalizia ni kwamba misaada na mikopo inatufanye tuwe wanyonge na katika azimio la Arusha 1967 katika kitabu cha Azimio la Arusha Ujamaa na Kujitegemea kilieleza wazi katika swala la mikopo kwamba serikali inakopa ili kupunguza maumivu ambayo inawabebesha wanachi katika kodi na tozo ndio mana inakopa ila pia serikali kama ikikopa basi ikope katika miradi yenye tija na yenye maendeleo ila pia kitabu kimejieleza wazi kabisa juu ya misaada kuwa ni tishio la uhuru wa nchi na inaweza hatarisha uhuru wa nchi yetu, hii ilikua 1967 andiko la baba wa taifa katika kupitisha azimio la Arusha je leo hii tunatekeleza vipi Azimio la Arusha katika swala zima la ukopaji na misaada? tutapokea kila msaada kisa tuu msaada? na tutakopa tuu kila mkopo kisa tunanafasi ya kukopa? la hasha kama tunakopa basi tukope kwa kuwekeza na misaada ni ina hatarisha uhuru wetu.
 
Upvote 6
Kuna mjadala mkubwa sana hapa nchini haswa kuhusu serikali kukopa na kupokea misaa kutoka nchi tofautitofauti kama Amerika, Uchina, Falme za Kiarabu na Umoja wa Nchi za Ulaya, mjadala ni mkali na kila msomina asiesoma huchambua kwa anavyoelewa wapo wanaopinga na wapo wanaounga mkono serikali kukopa na kwa andiko hili wote wapo sahihi mana wote wanaongea kutoakana na mitazamo yao na kwa mustakabali wa nchi la hasha wawe wanaongea kwa ajli ya matumbo yao.

Andiko hili linaanza na swali ambalo je Tanzania tunaweza jiendesha bila mikopo?

Jibu ni hapana tunaitaji mikopo, kwa hali tulionayo Tanzania hatuwezi jiendesha kikamilifu bila ya mikopo, hakuna nchi isiokopa, nchi zote zinakopa ila tunakopa kwa matumizi yapi?? na hapo ndio kiini cha andiko hili, hatukataii kukopa ila tunakopa kwa ajili gani?, tunakopa ili tufanye nini?? na tunavyokopa tunamini kwamba mikopo tunayoikopa itakua chachu ya maendeleo?, na kwanini tunakopa?, haya ni maswali ambayo lazima tujiulize mnoo kama wanachi ila pia watendaji wa serikali na viongozi wakuu haya maswali ni muhimu wajiulize katika kukopa.

Tuokope tuwekeze la hasha
Kwanini andiko likawa na kichwa hichi cha habari? Mana yake andiko hili linakubali serikali ikope ila ikope kwa kuwekeza na je kukopa kwa kuwekeza ni aina gani?. Kukopa kwa kuwekeza ni serikali kuchukua mikopo na kuiwekeza katika miradi ya kimaendeleo ambayo iyo miradi kwa miaka ya badae italeta tija na kua sehemu ya mapato ya nchi yetu au ikasisimua ukuaji wa uchumi wa nchi yetu aina hii ya ukopaji ndio ukopaji wenye tija na faida mfano tukope tujenge reli ya kisasa ambayo kw miaka ya badae itakua ni chanzo cha mapato kwamba huu mradi utakua unazalisha tutapata pesa na tutasisimua maendeleo hapa nchini, kama tunakopa basi tukope tujenge miradi ambayo kwa badae ni faida kwetu kama madaraja makubwa ambayo yatasaidia kuiunganisha nchi, tujenge mabarabara kama tunakopa basi tujenge miradi ya umeme yani kama tunakopa basi tuboresha sekta ya mawasiliano na uchukuzi kama tunakopa basi tukope kwa kuwekeza katika miradi ambayo kwa badae na sasa itakua ni sehemu kubwa ya kukuza uchumi wetu na pia itakua sehemu kubwa ya vyazo vya mapato katika taifa letu na zaidi ya hapo ni la hasha hili andiko linapinga aina iyo ya ukopaji.

Ukopaji gani wa la hasha?
Andiko hili la onya juu ya aina hii ya ukopaji moja serikali kukopa au kupokea misaada ambayo inaenda kutumika katika matumizi ya kawaida au matumizi yasio zaa au katika matumizi ya umuhimu ila hatuitaji kukopa kwa mfano kwanini serikali ikope au ichukue pesa za msaa kwa kujenga vyoo vya shule au madarasa au vita na madawati?? hili jambo ni aibuu narudia ni aibu ni vyema serikali ilalaimikiwe kutoza wanachi wake kodi ili iweze kujenga na kusimamia vitu kama ivi kwa pesa ya ndani, serikali kukopa ili kulip mishahara wafanyakazi narudia hili pia hapana, nini mana ya uwepo wa wizara ya fedha na mipango nini umuhimu wa kukusanya kodi kama tunakopa au kupokea misada ya ujenzi wa vyoo? Madawati? Hapana jamani hili halikai sawa hata kukopa kujenga hosptali na shule pia hapana kwani kodi tunazokusanya zinafanya kazi gani? hadi tupokee misaada na mikopo kwa kununua dawa au kununua vitanda vya hospitali? Hapana huku sio mana nzuri ya kukopa naandika haya bila haya wala aibu tukumbuke ivi vitu tunaweza kufanya wenyewe na pia tukumbuke tunakopa na tunaitaji rudisha ivyo tutakua kila siku tunakopa kwa matumizi yasio zalisha hata kama yana umuhimu kiasi gani.

Kwanini mikopo ya la hasha ni la hasha?
Nadra sana uende banki za kawaida tuu izi useme naomba kukopa sababu mama yangu mgonjwa nataka kufariki hawawezi kukupa aina ya mkopo huo bali mikopo yote ni ile ya uzalishaji bnki zitatoa mikopo kwa wajasiriamali, wafanya biashara wenye biashara za kueleweka ndio sababu hata wamachinga hawana mkopo banki mana yake nini?? mana yake wanajua kabis hela wanazikopa zinaenda zalisha na wakopaji watarudisha na hii ndio mana ya kukupoa ila serikali haitakiwi kukupa kama baba au mama wa familia anaenda kukupa unga au sukarli dukani yani mangi au mpemba nikopeshe kilo mbili za mchele kesho nakurudishia kwa miaka mingi serikali imekua aina ya ukopaji huu ambao hauna faida kwa Taifa letu.

Mikopo inatutia unyonge, uoga na unyenyekevu kwa tuliowakopa, taifa linapojilimbikizia mikopo na misaada tunajenga nidhamu ya uoga na unyeneyekevu kwa tunaowakopa na hii inafanya tuzidi kuwa tegemezi na tusiochakata katika njia gani bora za kujiendesha akili zetu zinadumaa tukiamini kesho tutaenda kwa mangi kuchukua mchele kilo mbili, mtokeo yake hatuna sauti kwa wahisani wetu hata wakitaka kufanya tusichokipenda hatuna sauti ya kukataa bali tunaugulia moyoni na rohoni sababu uwezi maka na kukoroma kwa mtu anaekudai pia utampingaje mtu ambae ushakua tegemezi kwake? ivyo basi kuepusha hadha hii ni bora kama tunakopa basi tukope kwa ajili ya kuwekeza katika miradi ya maendeleo katika vitu vitasisimua ukuaaji wa uchumi wetu.

Mwisho ni kumbushe kua nchi kama nchi inahitaji mikopo inahitaji sana kukopa ila tuweke viwango vya ukopaji na sioni sababu ya kuchukua misaada ambayo nchi kama nchi inaweza kuihimili, tukumbuke misaada tunayopewa iwe ya bure au mikopo ni hela za wanachi wa nchi husika, ivi kweli Marekani au China kodi za raia wake anazotoza ni anazigawa bure tuu yani bure tuu sababu kuna nchi inaitwa Tanzania inahitaji mashimo ya choo? au Tanzania ni rafiki yetu mzuri kiasiasa na kidipmloasia basi tumfadhili hela ya bajeti yake ya mwaka 2023/24 yani raia wao watoe kodi kwa ajili yetu bure bure ivi inaingia akilini? jibu ni hapana lazima izo hela wanazotupatia zitarudi ivyo miasaada sio mizuri bora tukope kuliko kukubali msaada mana lazima kuna kitu wanakiitaji kama leo tuu hapa nchini tunalalamika kodi na utitili wa kodi alafu Tanzania ichukue kodi zetu ziende igawia Marekani iawepe bure tuu ivi tutakubali??, Jibu ni hapana sasa kwanini nchi zilioendelea zifanye ivyo kwa nchi zinazoendelea? Mana yake wanakitu wanakitafuta ivyo tuwe macho na misaada.

Kwa kumalizia ni kwamba misaada na mikopo inatufanye tuwe wanyonge na katika azimio la Arusha 1967 katika kitabu cha Azimio la Arusha Ujamaa na Kujitegemea kilieleza wazi katika swaa la mikipo kwamba serikali inakopa ili kupunguza maumivu ambayo inawabebesha wanachi katika kodi na tozo ndio mana inakopa ila pia serikali kama ikikopa basi ikope katika miradi yenye tija na yenye maendeleo ila pia kitabu kimejieleza wazi kabisa juu ya misaada kuwa ni tishio la uhuru wa nchi na inaweza hatarisha uhuru wa nchi yetu, hii ilikua 1967 andiko la baba wa taifa katika kupitisha azimio la Arusha je leo hii tunatekeleza vipi Azimio la Arusha katika swala zima la ukopaji na misaada? tutapokea kila msaada kisa tuu msaada? na tutakopa tuu kila mkopo kisa tunanafasi ya kukopa? la hasha kama tunakopa basi tukope kwa kuwekeza na misaada ni ina hatarisha uhuru wetu.
Lkn kwel
 
Back
Top Bottom