Ninamwomba sana Mwenyezi Mungu asikie kilio cha watu wengi wanaojali maslahi pana ya wananchi wengi kuhusu kusimamisha mchakato wa kuelekea kwenye upigaji kura za Ndiyo au Hapana kwa katiba inayopendezwa. Karibu watu wote wenye nia njema na nchi hii walipiga kelele, wanapiga kelele na bado wataendelea kupiga kelele kusisitiza kwamba katiba ni suala la MARIDHIANO na wala sio suala la USHINDANI.
Tukubali kwamba tulikosea tangu mwanzo kulifanya jambo la katiba ni la misimamo ya vyama vya siasa na madhehebu ya dini. Na bahati nzuri Mungu ni mwema kwamba kwa hali ilivyo katiba hii haiwezi kupigiwa kura kwa sasa japokua watawala bado wanasisitiza kuwa lazima kura ipigwe. Kwa mazingira yaliyopo haiwezekani labda kama Serikali wameamua kuilipua nchi na baadaye kujilipua wenyewe.
Kwa mtazamo wangu hatua za awali ambazo zilishirikisha watu wenye uelewa na weledi (Tume ya kukusanya maoni, mabaraza ya katiba, na Bunge maalum la Katiba) ndizo zilikua msingi mkubwa wa mafanikio ya katiba mpya. Kwa mawazo yangu hao ndio baadhi ya watu wenye uwezo wa kifikra nchini. Lakini bahati mbaya wote tunakumbuka kilichofanyika kwenye Bunge la Katiba na baadhi ya mabaraza ya Katiba.
Kwenye Bunge la katiba ndiko matumaini ya kupata katiba mpya yenye kutatua matatizo ya kimfumo yanayotusumbua sasa yalizamishwa na kuzikwa hivyo tunaoelewa kidogo tulikata tamaa ya kupata katiba bora. Huko ndiko Maprofesa na Madakatari wa shule walipokua wameamua kujidharirisha wazi wazi kwa michango yao. Kuna wakati fulani nilipokua namwona profesa tena wa siku nyingi anachangia nilitamani kufukia uso wangu chini ya ardhi ili nisiendelee kumsikiliza jinsi anavyodhalilisha wasomi kwa hoja zake.
Hatua zile tatu za mwanzo ndizo zilikua muhimu sana, na baada ya hapo ndio ingeletwa kwetu wananchi wote kwa ajili ya taratibu tu za kuipitisha kwa sababu tulio wengi hata mtugawie hizo katiba pendezwa kila mmoja na yake ili tuzisome, ni wazi kwamba ni asilimia sio zaidi ya kumi (10%) wanaweza kuelewa na kuoanisha na maisha halisi.
Kwa mantiki hiyo, kama tungepiga kura kwa katiba hii pendezwa kama ilivyo na udhaifu pamoja na utangano uliopo, basi MATOKEO YAKE INGEKUA NI KAMA KUFANYA SURVEY YA KUJUA NANI ANASIKILIZWA/KUBALIKA NA WANANCHI KATI YA CCM AU UKAWA.
Mwisho nawashangaa baadhi ya makundi kuipigia kampeni hii katiba ili ipitishwe ati kwa sababu haki zao zimezingitiwa kwenye katiba inayopendekezwa, hivi hawa watu wanaishi kwenye kisiwa peke yao? Huu ni ubinafsi ulipindukia na unatakiwa kudhitiwa mapema sana. Kwa sababu tu maslahi yako yamezingatiwa ati hakuna sababu ya kupigia kelele masuala ya Maadili ya viongozi wa umma, suala la uwajibikaji kwa viongozi wa umma wanapofanya makosa au sehemu wanazosimamia zinapofanya makosa, madaraka makubwa ya Raisi, muundo tata wa muungano.
Kuna siku niliandika na kusema kwamba muhimu tujadili mambo muhimu yaliyoachwa na mabaya yaliyomo badala ya kujadili yale mazuri ambayo wote tunakubaliana nayo
Mwenyezi Mungu tunakuomba Ibariki Tanzania ili nchi iwe na Amani ya kweli.