Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Leo nikiwa kanisani nilikaa na bibi mmoja, mrembo ametengeneza nywele vizuri, kucha zina rangi na rangi ya mdomo. Bibi huyu alikuwa na fimbo ya kukunja kama kiti aliyokuwa anatembelea.
Kuna wakati alihitaji msaada kidogo lakini alipochoka alikunjua kiti cha fimbo na kukaa. Alivutiwa na moyo wangu wa kusaidia. Baada ya ibada nilimsaidia mpaka nje ya kanisa, aliniambia anaita tax imrudishe kwake. Nilimjibu kuwa ninamuona kama mzazi wangu hivyo asijali. Aliniambia ana umri wa miaka 96.
Nilishtuka nikamuuliza siri ya kuishi umri ule ni nini? Alisema maisha yake ya ujana alikuwa polisi. Hakukua na mapolisi wengi wa kike enzi hizo, nidhamu ya kazi iliwataka wafanye mazoezi ya kwata kila wiki. Alipiga kwata sana. Hata alipopanda cheo hakuacha nidhamu ya kufanya mazoezi. Alistaafu akiwa na cheo cha Kamishna.
Tuliishia kuwa marafiki, aliniambia ana msusi wake anamtembelea kila Jumamosi kumtengeneza kwa nywele za Jumapili. Huyu bibi si kama ma bibi wengi wa miaka 96.