Nguza au Mchonga: Headmaster wangu "O" level.
Mwalimu Kibao: Huyu alikuwa discipline master, alikuwa ameanzisha kakibao kalikoandikwa "STUPID", ilikuwa ukiongea kiswahili tu mwenzio anakupa. Siku inayofuatia akiingia darasani anaanza kuuliza "who has got a kibao?", inafuatiwa na who gave you, hadi inamfikia yule aliyeachiwa siku iliyotangulia. Baada ya hapo mnapigwa fimbo, cha kufurahisha alikuwa akiita fimbo yake "Mwajuma"! Atasema utakula kibao na saa tisa na nusu shambani!
Archimedes: Huyu alifundisha physics form two, topic yake kubwa iliyotufanya tumuite Archimedes ni ile ya principles of archimedes. Alipenda sana kuigiza maneno ya "Eureka, eureka, eureka!" Those days banaa!!