Von soden= mwalimu wangu wa history la sita (topic ya scramble for and partition of africa)
Diki short form ya DICTATOR= rector wangu secondary alikuwa mkali dunia nzima
Perfomerr= Mwalimu wangu na manual work cordinator, huyu jamaa alikuwa kama john cena ulingoni
Maya= mwalimu wangu wa commerce na book keeping; alikuwa mtu mzima but she behaved like a teenager
Lawino= mwalimu wangu wa literature aligombana na mumewe zikachapwa kavu kavu shuleni tena baada ya parade ya saa tisa.
Kanyundo= mwalimu wangu wa history alikuwa mfupi hujawahi ona!
Babu= ni kawaida kwa walimu wazee
Mandible= mwalimu wangu wa biology form three alikuwa na mdomo mpana balaa
Kenge= huyu ticha alikuwa mkali halafu ana sura ka jiwe
Nyerere= mwalimu wangu wa siasa la tano, mwaka mzima alifundisha juu ya azimio la Arusha
kipipa= alikuwa mwalimu wangu wa kiingereza la nne, alikuwa binti na kiherehere usiombe ukutwe na kosa halafu upelekwe ofisini na ye awepo alikuwa na umbo la mviringo mwili mzima ka mpira.
Kimbilio= huyu alikuwa maza angu si mnajua alikuwa ticha wa primari? alikuwa mpole na alipenda kuwatetea madenti!
Faru huyu aliitwa Mwl Byarugaba, alikuwa akitokea kule BK kwa kina iwe, alikuwa ka faru, uwe na kosa huna ukikutana naye unakula kwenzi (nyundo). Alipenda sana kunywa "pingu" hata aubuhi alikuwa nzwi!
Kuni= huyu mama nadhani hakuwa na bajeti ya mkaa manake kila ijumaa alituagiza kuni!
Jamani tumetoka mbali!