1.
Najua una rekodi kubwa sana ya mambo ya wakati huo, ila nakuomba tena upitie kumbukumbu zako vizuri na kwa makini. Ukweli ni kuwa mtindo alioanza nao Marehemu Maneti pale Vijana Jazz ulikuwa ni Koka Koka. Wimbo wa Kamata Sukuma ulitolewa kipindi kimoja na Niliruka Ukuta, na ulipigwa pia katika mtindo wa Koka Koka, ila kutokana na umaarufu ulioambatana na wimbo ule wa Kamata Sukuma, Maneti akapromote wimbo wa "Kamata Sukuma" kuwa mtindo uliorithi Koka Koka mwaka 1976 hivi, na ulidumu muda mfupi sana kabla hajaanzisha Heka Heka.
Mkuu Wangu,
1. Hemedi "Chiriku Tenor'" Maneti, alikuwa ni mmoja wa my favorate singer, kwa hiyo nilikuwa ninamfuatilia sana toka alipoanzia Vijana Jazz, lakini I could still be wrong ila tu ninakumbuka tena very clear kuwa Nyimbo za kwanza za Maneti na mtindo wake wa "Kamata Sukuma" ziko tofauti kabisa na zile za awamu ya pili ya "Koka Koka",
- Kwanza vyombo vilivyotumika kwenye awamu yake ya kwanza sio safi au clear kama za ya pili ambapo alitumia vyombo vizuri zaidi, nyimbo kama za Sabina, Kuruka Ukuta, Magdalena, Zubeda, Maneti specifically anautaja huu mtindo wa Kamata Sukuma kwenye kuziiimba na hii ilikuwa before 1977 kwa sababu kwenye mtindo wa "Koka Koka" ndio kuna wimbo wake wa kuungana kwa TANU Na AFRO, unaoitwa "Muungano Sasa Umekamilika".
- Kwa hiyo mtindo wake wa "Koka Koka" unaanzia mwishoni mwa mwaka 1976 na pia kwenye hizi songs kama kawaida yake anasema sana "wana-koka", na ndani ya hizi nyimbo ndio kuna CCM, Frelimo, Operetion Maduka, Masido, Zuhura (ukiusikiliza kwa makini sana hapa mkuu utakuwa in one statement Maneti anamuuliza Zuhura ataipata wapi tiketi ya "Koka Koka") Zubeda, Belibe, Djogolo Kalulu ni ndani ya hizi nyimbo ndio kwa mara ya kwanza anataja sana "Koka Koka" na "wana-Koka" na hizi alizitoa rasmi wakati wa kuanzishwa kwa CCM, ambapo ndani yake ndipo Mozambique walipata uhuru ndio maana aliimba kupandishwa kwa bendera ya Frelimo.
2.
Kumbukumbu yangu kuhusu wimbo wa "Niliruka Ukuta" ambamo sauti ya Marehemu Maneti ilikuwa haitofautiani na ile ya Marahemu Mbaraka inakuja vizuri sana. Vile vile chini ya mtindo wa Koka Koka, Maneti alipiga wimbo wa "Zuhura Ninaondoka" ambao binafsi nilikuwa nauhusisha sana na mpenzi wangu wa wakati huo Marehemu Zuhura (RIP). Nilikuwa nina T-Shirt moja ya Sunflag iliyokuwa na picha ya kichwa cha tembo kifuani; mgongoni nikaandika pale maneno matatu kwa style ya aina yake: maneno hayo yalikuwa ni Masika, Sokomoko na Koka Koka, ambayo ilikuwa mitindo ya muziki niliyokuwa naizimia sana wakati ule. Marafiki zangu wa wakati huo wa ujingani wakisoma post hii watakumbuka sana ninayosema. Wakati Maneti anatoa wimbo wa "Niliruka Ukuta," Mbaraka naye alitoa wimbo wa "Mshenga" ambapo Marijani naye alikuwa ametoa wimbo uliokuwa unasema "Wapangaji mnawaacha watoto wenu wanavunjavunja milango na madirisha ndani ya nyumba yangu, hivyo ni afadhali muondoke kwani mnaleta sokomoko ndani ya nyumba yangu": jina halisi la wimbo huu silikumbuki tena. Nyimbo hizi zilikuwa kiboko sana wakati huo ndiyo maana kwangu mimi muziki ukawa ni Masika, Koka Koka na Sokomoko.
1. Ni kweli kabisa mkuu unayosema, lakini "Niliruka Ukuta" ulikuwa ni wimbo wa kwanza kumuingiza Maneti kwenye ligi ya juu kimuziki nchini ndio kwa mara ya kwanza wananchi tulianza ku-pay attention kuwa Maneti naye yumo kwenye list,
2. kwenye ule wimbo "kamata Sukuma" aliuutumia kuwataja wanamuziki wenzake wote wa Vijana Jazz, lakini kwenye wimbo wa "Zubeda" ambao ni safu hiyo hiyo ya kwanza na 'Salima" Maneti specifically ndio anathibitisha kuwa Kamata Sukuma ni mtindo sio wimbo tu kama wengi tulivyofikiri kwenye ule wimbo wa "Kamata Sukuma" kwa sababu katika kipindi hicho kizima cha mwanzoni ilikuwa nadra sana kwa Vijana Jazz kusemwa wazi kuwa wanatumia mtindo gani, ni mpaka ukienda kuwaona live as I did ndio ungejua kuwa "Kamata Sukuma" ni mtindo, lakini walipongia kwenye awamu ya pili ya "Koka Koka" ndio kwa mara ya kwanza wakawa kwenye matangazo yao wanasema wazi kuwa wao ni "wana-Koka"
2.
Kuna watu wengine wanaweza pia kuthibitisha hili. Hebu soma hapa:
Marehemu Maneti alipochukua uongozi wa bendi ya Vijana Jazz alianza nao na mtindo wa Kokakoka. Vibao maarufu vya mwanzo mwanzo vya bendi hiyo vilikuwa "Nimeruka Ukuta" uliofahamika na wengi, "Sabina" na Magdalena". Kwenye wimbo wa Sabina alimuomba mpenzi wake Sabina arudi kwani siku nyingi zilikuwa zimepita tangu aondoke na kwenye wimbo "Magdalena" alikuwa analalamika kuzuiwa na wazazi wake kumuoa Magdalena kwa sababu alikuwa na ulemavu wa jicho wakati yeye alikuwa akimpenda sana.
Pamoja na nyimbo hizo, nyimbo nyingine za mwanzo mwanzo za bendi hiyo zilikuwa, "Zuhura Naondoka", "Kamata Sukuma" waliotumia kujitaja majina, "Salima", "Nimeruka Ukuta Namba Mbili" na "Magdalena Namba Mbili" ambamo Maneti alifurahi baada ya wazazi wake kukubali amuoe Magdalena.
Hapa mkuu hata huyu aliyeandika hii article amechemsha big time, kwa sababu kwenye nyimbo zote alizozitaja hapo juu licha ya kwamba niliwaona kwa macho yangu Vijana Jazz wakipiga hiyo miziki, pia bado ninayo kwenye collection yangu ni kwamba, Maneti specifically anatamka neno "Koka Koka" kwenye nyimbo za "Zuhura" na namba mbili za Magdalena na "Kuruka Ukuta" lakini not kwenye nyimbo za before that.
- Mwandishi wa article hii anayo kumbu kumbu kubwa sana na facts nyingi sana za Vijana Jazz, lakini ni hapo tu alipochanganya madawa, hizi nyimbo alizozitaja hapo juu hazikutolewa kwa wakati mmoja, hapana zilitolewa kwa nyakati mbili tofauti:-
- Nyimbo za Sabina, Magdalena, na Kuruka ukuta, mwandishi amesahau wimbo wa "Zubeda" zilitolewa mara ya kwanza Maneti anaingia kwenye taifa kama kiongozi wa bendi ya Vijana na mtindo wa "Kamata Sukuma",
- Na hizi za "Zuhura" na namba mbili za "Kuruka Ukuta" na "Magdalena" ndio kwa mara ya kwanza Maneti anamuuliza Zuhura, ataipata wapi tiketi ya "Koka Koka" hizi zilitoka kwenye awamu ya pili ambapo ndani yake kulikuwemo pia nyimbo za kuipongeza CCM kuungana na Afro, na pia kuwapongeza Frelimo na uhuru wa Mozambique.
Labda niwaombe samahani wananchi kwa kuiendeleza hii habari kwa muda mrefu, lakini nilikuwa na heshima sana na Maneti (RIP), ambaye alipoanza muziki na Vijana Jazz, alituvuta vijana wengi sana then kwa sababu alitumia sana mtindo unaofanana na bendi iliyokuwa maarufu sana enzi zile na vijana ya Orch. Sosoliso toka Zaire, ya kina Matadidi Mabele Mwana Kitoko na Loko Masengo kwenye mtindo wake wa "Kamata Sukuma",
lakini alipobadili tu na kuingia kwenye "Koka Koka", yule mpigaji wake wa Solo Hamza Kalala 'Komandoo" alijitoa Vijana na kuingia UDA JAZZ na ndio maana hata kwenye awamu ya pili ya Maneti, style ya upigaji solo sasa ikabadilika kabisa kwenye mtindo wa "Koka Koka" maana sasa leading solo alikuwa ni Hassan Dalali ambaye upigaji wake wa solo gitaa ulikuwa ni opposite kabisa na Kalala, ingawa baadaye Kalala alirudi tena Vijana, lakini this time alirudi akiwa na style mpya ya solo kama ya Mosesengo Fan Fan, aliyeingia Makassy akitokea kwa Lwambo..
Niliwahi kuhudhuria sana maonyesho yake Maneti live, katika sehemu kama Banana Bar njia panda ya airport, Ukumbi wa Police Chang'ombe, Vijana Social Hall Mwananyamala, na Police Mess Obey, Maneti alikuwa cool na kwa mara ya kwanza nilipata bahati ya kuchati naye one on one, ilikuwa wakati yeye na bendi yake wanasafiri kwenda Bujumbura, ambako walialikwa na bendi moja ya taarabu kule kitongoji cha Buyenzi, Bujumbura. Nilikutana naye nikiwa training ndani ya Meli ya MV. Liemba nice guy na cool pia, alionekana kua na wasi wasi sana kuhusu mashabiki wa muziki wa Bujumbura, wataipokea vipi Vijana Jazz, akiwa na wasi wasi sana akaniambia kuwa "...nasikia huko Bujumbura wao wamezoea wa-Zaire wakali kama kina Papa-Wemba sasa sisi Vijana bongo itakuwaje?..." alikuwa na wasi wasi sana kwenye hilo.
Kwa bahati nzuri tulipofika kule, kilikuwa ni kipindi timu ya maarufu ya mpira ya Intere (International) ambayo then ilikuwa inamilikiwa na rais wao Bagaza, walikuwa ndio kwanza wameajiri wachezaji kadhaa kutoka bongo, ninawakumbuka sana nao ni kina Katwila, Isaack Mwakatika, na George "Best" Kulagwa, Bujumbura ni mji mdogo sana hawa wachezaji walikuwa known na kila mtu kule mpaka watoto wadogo, tena walikuwa maarufu sana kwa hiyo Ads zote za Vijana Jazz zikawa tied na hawa wachezaji, as the results Vijana Jazz wakaweza kuvunja record pale mjini mpaka ikabidi wapigie kwenye uwanja wa taifa wa mpira, on the way back Maneti was happy na ndio akatunga wimbo wa "Bujumbura".
Aliporudi Dar, aliamua kuanza kuutafuta ubunge, infact alikua amesha make a big progress, lakini kwa bahati mbaya akatangulia kwenye haki akiwa ameacha mtoto na dada mmoja pale Mwananyamala Diana (Nafikiri utakumbuka kua aliwahi kuwa na wimbo wa kumsifia sana Diana), next na anapoishi Mkulu DJ JPP (Pantalakis), dada ambaye enzi hizo alikua Air Hostess. Mungu amuweke mahali pema sana peponi Mwanamuziki Hemedi Maneti, na hapa naweka kalamu chini.
Ahsante Wakuu.