Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

1.
Cosmo ya Ilala ilipewa jina baada ya ile Cosmo au Cosmopolitan timu aliyokuwa aikichezea Edison Arantes Do Nascimento-Pele alipokuja kucheza mpira wa miguu Marekani.

Mkuu Cosmos, hebu cheki tena walikuwepo kabla ya Cosmos ya US haijaanzishwa na Pele kwenda huko, maana kumbuka hiki kilikuwa ni kipindi cha zile khanga zenye maneno "Pele na Santos ni Wageni Wa Yanga" au umesahau mkuu?

Pele alikuja bongo baadaye akiwa ame-retire tayari lakini alipita tuu kwa siku moja mjini Dar, baada ya Yanga kushindwa kuhimili malipo aliyokuwa akiyataka ili aonyeshe kabumbu, nakumbuka jinsi Marehemu Joseph Mbwambo kiongozi wa Yanga then alivyohangaika sana na hiyo safari ya Pele, mabapo hata Pele mwenyewe alimsifu sana alipokuja pale airport kutokana na juhudi zake kubwa za kumhangaikia ili aje, alikuwa njiani kwenda Nairobi akipelekwa na Coca Cola.


2.
Hivi Yanga Fadhili Bwanga baada ya kipigo cha Simba 1976 alikimbilia wapi

Yeye na Yusuf Kaungu, Haidari Abeid, Ismail Abeid, Mohamed Tall, Jumanne Masuminti, Aluu Aly, Ahmed Amasha, walihamia Uarabuni kucheza sok ala kulipwa, Tall na Masuminti hawa kukaa muda mrefu walirudi wenginer walibaki nadhani mpaka leo.
 

Kuna Jamhuri Jazz ambao ndio chimbuko la Simba wa Nyika au Arusha Jazz, na Atomic Jazz. Nyimbo zao kama "Kipande cha Papa " = Jamhuri pamoja na "Joyce" = Atomic kwa kweli zilivuma sana miaka ile.
 

New York Cosmo ilikuwa operational kutoka 1971-1985. Pele alijiunga nayo nafikiri 1975 mpaka alipostaafu 1977.

Unless Cosmo ya Dar ilianza kabla ya 1970 na kujiita Cosmo kupitia timu za UK (highly unlikely).

Hivi kwani Cosmo, Pan na Red Star Nyota Nyekundu si karibu zilianza wakati 1975-1977 au?
 

kama kumbukumbu zangu ziko sawa, cosmo walikuwepo kwenye mwishoni mwa 60s au mwanzoni mwa 70s. pan na nyota nyekendu ni za baadae kwani zilitokana na migogoro iliyotokea yanga na simba.

hususan pan ambayo ilianza na wachezaji kama pondamali na kassimu manara pamoja na wengine ambao baada ya kutoka yanga walianzisha timu (nimesahau jina) ambayo haikudumu kisha wakaanzisha/wakaenda pan.
 
cosmo,has been around miaka mingi sana,naahisi jina came out of the english word COSMOPOLITAN,yaani in those days ikimaanisha mchanganyiko wa watu mbalimbali,yaani waarabu,waswahili,wahamiaji toka bara etc,etc
 
Hivi wimbo wa kwanza wa Remmy akiwa Makassy haukuwa Asumani (Athumani)?
 
huko kwenye bendi ya msondo,mbona tumesikia story nyingi za kutisha,eti enzi hizo ukienda na mkeo,wanaume wanakutaka wewe,mkeo hawamtaki. jamani ati ile story ya zamani kwamba RANGE ROVER hairuhusiwi kupaki nje ya benki ni kweli? je mnakumbuka lile meli la dini MV LOGOS,likidock dar tunavyoenda kukusanya mivitabu ya dini
 
...RANGE ROVER hairuhusiwi kupaki nje ya benki ni kweli?

...nami niliisikia sana hadithi hiyo, labda kwakuwa zile 'Pijo' 404 za polisi wakati huo zisingefua dafu kufukuzana na twin turbo za Range enzi zile πŸ˜€

View attachment 2403

...hata timu yetu ya taifa kuna kipindi walicheza mpira 'kidari wazi', sijui ilikuwaje wakati wa kubadilishana jezi!!!,...(aliyekuwa Rais wa Sudan) Nimeiry huyo akiikagua timu, King Kibaden wakati huo bado dogo, (anaonekana kwa nyuma pale!)
 

Naam FMES, hujakosea kabisa. Timu hiyo ilikuwa inatumia jina la Cosmo hata kabla ya Pele kujiunga na Cosmo ya New York. Jina la Cosmo lilitokana na timu hiyo kuwa na mchanganyiko maalum wa waarabu na weusi kuanzia wachezaji hata viongozi ulikinganisha na timu nyingine maarufu za wakati huo ikiwemo Simba na Yanga.
 

FMES, madisco yote hapo juu yalikuwa 9, 10 ilikuwa ni Mbowe debe zilizokuwa zinapigwa pale zilikuwa ni kali mno na mara chache sana kusikia debe zilizokuwa zinapigwa Mbowe katika disco lingine lolote lile.

Muziki wa bendi ilikuwa ni Amana Kwa Nuta Jazz Band. Huko ilikuwa ni kuvaa tshirt tu ili kuonyesha ukubwa wa kifua chako kama meza ya kulia hakuna mashati halafu partner wako ni chupa yako ya bia. Unaiweka mbele yako chupa yako ya bia na kucheza nayo, unaongea nayo na kuizungukazunguka na mtu haigusi akiigusa tu basi ni ugomvi wa hali ya juu. Wakati mwingine ilikuwa ni chupa tupu haina beer maana umeshakunywa umemaliza....LOL!
 
...Golf Club Zanzibar Circa 1800, funny thing, mpaka sasa hili jumba la mbao bado lipo pale Viwanja vya Maisara,

...Ikumbukwe hapo 'GOFU' kama panavyojulikana sana unguja, (mpaka miaka ya mid-1990's) kuwa kati ya sehemu chache kisiwani palipokuwa panaruhusiwa kuuzwa pombe, ukiachilia mbali Hoteli ya Bwawani, na Kilimani Bar, tofauti na sasa ambako watu wanajinywea ulabu nje nje kama kwa Kimti, rahaleo, Michenzani nk

...what a piece of history!!!


View attachment 2406

View attachment 2407
 
huko msondo kuna story nyingi,sijui ni uongo,eti jambazi lolote ambalo ni wanted na polisi,wanakamatwa kirahisi,maana lazima waende kucheza msondo.msondo akipiga muziki mauzo ya bia ni madogo,sababu kila mtu ameshakunywa gongo.lile jambazi rajabu mgogo lilimpiga kichwa corporal john(mbwa wa polisi)na kuuwa hapohapo katika ukumbi wa amana
 
New York Cosmo ilikuwa operational kutoka 1971-1985. Pele alijiunga nayo nafikiri 1975 mpaka alipostaafu 1977.

Unless Cosmo ya Dar ilianza kabla ya 1970 na kujiita Cosmo kupitia timu za UK (highly unlikely).

Originally, Yanga ilikuwa inaitwa Young Africans Sports Club, Simba ilikuwa inaitwa Sunderland, Cosmo ilikuwa inaitwa Cosmopolitan,

Yes Cosmo, ya bongo ilikuwepo toka enzi za mwishoni mwa the 60s, wakati Pele anahamia New York, Cosmo ya bongo ilikuwepo, Wakati mchezaji wa kimataifa Chinaglia anahamia Cosmo ya New York, toka Italy bado Cosmo ya bongo ilikuwepo,

Nafikiri utakuwa unakumbuka timu moja iliyokuwa one level na Cosmo, kwa jina Nungu FC!
 

Sawa kabisa FMES, sikumbuki timu ya Cosmo ilianza kutumia jina hilo lini lakini mwishoni mwa miaka ya 60 tayari walikuwa wanatumia jina hilo na wakati huo yule mchawi wa kusakata soka duniani Edson Arantes Dos Nascimento au kwa jina maarufu la Pele alikuwa bado yuko Santos ya Brazil.
 
Pan African

Mkuu GT,

Hapo umesema sawa kabisa, kama ninakumbuka vizuri waliosimama kuanzia kushoto ni:-

- Athumani Kilambo, Juma Matokeo, Adolph Rishad, Rashidi Idd "Chama", Hussein Mkweche, Juma Pondamali, Kassim Matitu, Patric Rugaimukamu.

- Waliochuchumama kuanzia kushoto ni Vivian, Clement Joseph, Omari Kapera, Juma Shabaani, Gordian Mapango, Mahamed Yahaya "Tostao" na Kitwana Manara "Popat".
 
Ama umaarufu wa Gofu Club umechangiwa sana na jamaa wa UWT, kwani kile ndio kijiwe chao kiasi cha kunywa ulabu kwa bili....πŸ˜€ πŸ˜€
 
Ama umaarufu wa Gofu Club umechangiwa sana na jamaa wa UWT, kwani kile ndio kijiwe chao kiasi cha kunywa ulabu kwa bili....πŸ˜€ πŸ˜€

...na palivyo walking distance tu 'kutokea ofisini' ndio kabisaaa πŸ˜€
 
Hapa kuna Mangara Tabu Mangara na Tambwe Leya. Je walikuwa na nyadhifa gani kitaifa, na kwenye picha hii walikuwa wakifanya nini, na ni lini?

 

Attachments

  • Mangara.jpg
    51.4 KB · Views: 332
Katika miaka ya sitini, timu ya Simba ilikuwa ikijulikana kama Sunderland. Je ni lini walipobadili jina na kuitwa Simba? Ninadhani kuwa itakuwa ni kati ya 70 na 71 hivi, ila sina uhakika. Naomba mwenye nondo kamili azimwage hapa.
 

Washabiki wa Msondo walikuwa wababe, hadithi mtaani zilikuwa ni kuwa kila mshabiki akiingia Amana, alikuwa anaweka skwea ya mita moja kwa moja no entry na ukiingia ni kibano!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…