Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha


Hii skando ya Taifa Star kucheza vifua wazi ilitokana na timu zote kuwa na jezi zenye rangi moja na Taifa Stars eti hawakuwa na jezi za ziada za rangi nyingine.

Inasemekana baada ya mechi hiyo, Julius "Kaizari" Nyerere alisusa kwenda mpirani!
 
Hivi, nani walikuwa lead musicians wa Cicko Kids? naona tumewasahau hawa.

Halafu kulikuwa na jamaa anaitwa Frank na dada zake!
 

Mie huwa nawashangaa wanaosema siku hizi Tanzania kuna wachezaji wazuri kuliko miaka iliyopita. Nikienda mpirani siwaoni hao wachezaji naona vurugu mechi tu. Support wanayopata leo Taifa Stars toka serikalini na wananchi ingekuwepo miaka ile basi si ajabu tungekuwa tumeshakwaa kombe la Afrika na pia kushiriki katika Kombe la Dunia.
 


Asante sana mzee FMES kwa kutufahamisha mengi kuhusu huyu mwanamuziki mahiri tuliyewahi kuwa naye. Kuna mengi yaliyokuwa yanatokea Dar siyafahamu hasa kwa vile wakati huo mimi nilikuwa naishi huko Tabora, na nilikuwa nafika Dar kwa msimu tu kutumia treni inayosafiri siku mbili njiani usiku na mchana. Hata hivyo, naona ugumu sana kukubaliana nawe kuwa mtindo wa Koka Koka ulianza mwaka 1976, kwa vile mimi niliandika T-Shirt yangu neno Kokakoka mwaka 1975 nikiwa nalihusisha na Vijana Jazz. Inawezekana huo mtindo wa Kamata Sukuma ulitumika mwanzoni mwa mwaka 1974 na haukuvuma kabisa kwa vile mtindo wa kwanza kujulikana ulikuwa huu wa Koka Koka.

Turudi nyuma tena; kumbuka kuwa kati ya mwaka 1975 na 1976 Vijana Jazz walikuwa wanarekodi nyimbo zao kwa kutumia Label za Moto Moto na kama hii hapa.


Partial listing ya Catalogue ya Moto Moto inaoinyesha santuri zao kwa utaratibu ufuatao:


MOTO 7-907 : Sabina/Niliruka Ukuta - Vijana Jazz Band , 1975
MOTO 7-918 : Magdalina No 2/Miaka Mingi - Vijana Jazz Band , 1975
MOTO 7-922 : Koka Koka No 1/Ujirani Mwema - Vijana Jazz Band , 1975
MOTO 7-923 : Shangazi/Gwe Manetu Fii - Vijana Jazz Band, 1975
MOTO 7-928 : Pili Nihurumie/Zuhura Naondoka - Vijana Jazz Band, 1976
MOTO 7-930 : Unakufa Kiofisa/Wajue Vijana Jazz - Vijana Jazz Band, 1976​


Unaona kuwa hata ule wimbo KokaKoka Namba 1 ulipigwa mwaka 1975, mwaka ambao wimbo wa Niliruka Ukuta ulipotolewa pia. Nina imani kuwa Zuhura Naondoka uliopigwa mwaka 1976 bado ulikuwa kwenye mtindo wa Koka Koka. Inawezekana nyimbo nyingine hazikuwekwa kwenye santuri, ila zilirekodiwa RTD tu. Unajua kuwa baada ya kuvunjika kwa EAC (1977,) kuna wakati mpaka wetu na Kenya ulikuwa umefungwa, na hivyo wanamuziki wengi wa Tanzania wakawa hawarekodi nyimbo zao huko Kenya tena; ndipo wakawa wanarekodia RTD kwa ajili ya kupiga redioni tu, wala hakukuwa na santuri tena. Nadhani hiyo ilipunguza sana mapato yao na hivyo kudororesha maendeleo ya Muziki kwa vile studio zote za kurekodi santuri zilikuwa Kenya.


Kwa wale ambao wanasikia jina la wimbo Niliruka Ukuta bila kuufahamu, nimefanikiwa kuupata online: Gonga hapa uusikilize na kuuangusha (download MP3) kwenye computer yako ukiependa.
 

Attachments

  • mototomo.jpg
    9.1 KB · Views: 581
MOTO 7-907 : Sabina/Niliruka Ukuta - Vijana Jazz Band , 1975
MOTO 7-918 : Magdalina No 2/Miaka Mingi - Vijana Jazz Band , 1975

Hapa kuna zilizokosa nyimbo kama Zubeda, na Salima kabla ya kugeuka kuwa Koka Koka,

Anyways, mkuu Kichuguu heshima mbele sana unajua once in a while huwa nina tabia ya kutayarisha Disco maalum ninaloliita "Old is Gold" nitakapokuwa tayari nitakufahamisha na mahali, mara ya mwisho nilipolifanya kidogo nile law suit kwa sababu nilizidisha watu kuliko uwezo wa jengo na ukumbi,

Otherwise, heshima mbele mkuu na salute kwa historia nzito sana na ubarikiwe pia kwa hizi info.
 
...hata timu yetu ya taifa kuna kipindi walicheza mpira 'kidari wazi', sijui ilikuwaje wakati wa kubadilishana jezi!!!,...(aliyekuwa Rais wa Sudan) Nimeiry huyo akiikagua timu, King Kibaden wakati huo bado dogo, (anaonekana kwa nyuma pale!)

Mkuu heshima mbele sana,

1. Mwalimu alikuwa hapendi kwenda mipirani, siku hiyo from no where akaamua kwenda, viongozi wa FAT wakaanza kujiuma uma jezi hakuna, Mwalimu aliapa kutokwenda tena mipirani.

2. Hapo kwenye picha nimewaona:-

- Mohamed Chuma, Omari Zimbwe, Abdulrahaman Juma (Nahodha), Then Rais wa Sudan Gen. Jaffar El-Nimeiri, Kitwana Manara "Popat", Abdallah Kibadeni anayechungulia kwa nyuma.

Duh! Mkuu Kichuguu, hands down maana this is perfect!
 
Hapa kuna Mangara Tabu Mangara na Tambwe Leya. Je walikuwa na nyadhifa gani kitaifa, na kwenye picha hii walikuwa wakifanya nini, na ni lini?

Mkuu Kichuguu,

Hapa naowaona kwenye picha ni Tambwe Leya (Then Kocha wa Yanga toka Zaire), Gibbson Sembuli (RIP) (Then Nahodha wa Yanga), Joseph Mbwambo (RIP) aliyekuwa kiongozi wa Yanga, na Mzee Tabu Mangara Tabu (RIP) (Then Mwenyekiti wa Yanga),

Sikumbuki ulikuwa ni mwaka gani, lakini najua for a fact kuwa ilikuwa ni in the middle ya the 70s, ilikuwa ni kwenye uwanja wa ndege wa Dar, Yanga walikuwa wamerejea kutoka Zanzibar walikonyakua kombe la Afrika Mashariki na ya Kati kwa kuifunga Simba, magoli 2-1, yaliyofungwa na Sembuli na Sunday Manara, goil la Simba lilifungwa na Saad Ali kama sikosei.

Ubarikiwe mkuu!
 
Safarilands.org

The Nyiramba Tribe Origins:Traced from African Tribal Migrations from the time of Bahima Empire
URL: SafariLands.org: People & Culture: The Nyiramba Tribe Origins:Traced from African Tribal Migrations from the time of Bahima Empire
Posted: Tuesday October 24, 2006 12:49 AM BT
By Dr. J. Kitundu
A group of Bantu speaking family of Clans called the Anilyamba migrated from what is now Rwanda/Uganda borders (area called Bahima west of Lake Victoria) along the southern shores of Lake Victoria (which they called Nanza) until they came to settle in the eastern coast of Lake Victoria which is now Mara Region near Musoma. This happened 100-200 years ago.

The exact localities where they inhabited have villages and areas which are called: Iramba, isanzu, Ruruma, Kirumi, Shemschem, Makalama, etc, which are still used in the areas in which they stopped. These names are also the same names which are used in the Iramba district in Central Tanzania....quite far from the Mara region.

The reason the Nyiramba migrated out of the ancestral lake zone area is because they were a peaceful people and not a warlike people. They were driven out by the warlike Kurias who migrated from the the North of Lake Victoria to the Eastern part of the Lake due to their wars with the Maasai. Until today the Kuria tribe and the Nyiramba's call one another "Jokey" , i.e. Watani because they fought a war between them long ago.

The Nyiramba migration was not smooth. On moving east and southward across the Serengeti, they encountered the warlike Maasai herdsmen. In the fight, the Nyiramba broke into two groups, one moved north-easterly while another moved south-westerly to cross the Sibiti river basin at two different points: one to the south at Kitangiri Lake and the other though what is now Karatu district.

Some of the old stories contain references about coming from a place where "the water moved back and forth." This does not refer to a tidal area, but it refers to the large marshi area on the Sibiti River.

If it rains a lot in the Lake Eyasi area, the water flows west in the Sibiti River, If it rains a lot in the Kitangiri Lake area, the water flows east in the Sibiti River. The basin is very flat and no bridge has yet been built to cross this difficult area.

The north easterly group went on moving until the Usambara and Pare mountains where they were forced to move south westerly towards the central plateau through what is now Kondoa, then further south to Iringa, There they were forced to moved northward by the war strong Hehe tribe until today they are also jokes (watain) about the Nyiramba. Here the Muhwa forced them out and they walked up from the Rugwas Reserve into the central plateau.

Part of the jouney was also to avoid being captures for slavery as well as to avoid war. Also sometimes they stopped for long periods of time and intermarried.

They entered the Central plateau from the south through Ukimbu land now called Ushora and Usure where evidence of the first settlements is found.

On migration further north they met the groups which had crossed at the Kitangiri lake. This group had migrated only a short distance compared to the Karatu crossing group. Both came to the Irama plateau which they have so named Lyamba. Some continued to the low areas around the plateau which is called Mbuga.

Among the group which crossed near Kitungiri Lake was a clan elder called Kitundu who supervised the Anakumi clan assisted by his famous sister called Musua. The Anakumi, clan of Kitundu and his sister Musua, came to settle at a place called Kisana, just east of what is now New Kiomboi. Some of the same clan settled at Ruruma, Kirumi, Kinakumi and at a further northern part Isanzu.

Of interest to us is where the clan elder Mzee Kitundu and his sister Musua settled until they died. This is Kisana village which is just north of rumuma in the present Iramba District.

The Anakumi clan has multiplied a lot, but they still trace their origins at Kinakumi and Kisana villages....

Full article at: The Nyiramba Tribe Origins: Traced from African Tribal Migrations from the time of Bahima Empire in Central Africa

Copyright © 2005, Safarilands.org

To this day in Majita there is a place called Iramba. Kitundu and Magembe are Bajita names.
Rev. Kishoka upo hapo?
There are more of us who came from Burundi than we realize.
 
Last edited:
Hii skando ya Taifa Star kucheza vifua wazi ilitokana na timu zote kuwa na jezi zenye rangi moja na Taifa Stars eti hawakuwa na jezi za ziada za rangi nyingine.

Inasemekana baada ya mechi hiyo, Julius "Kaizari" Nyerere alisusa kwenda mpirani!

Sawa kabisa Rev. na hiyo ni sheria ya FIFA kwamba kunapotokea timu mbili zina jezi zinazofanana basi ile ambayo iko nyumbani ndiyo inatakiwa ibadilishe jezi. Na Taifa Stars walienda uwanjani na pair moja tu.

Kuna mechi nyingine ya Taifa Stars na timu ya taifa toka Ethiopia ambayo Mwalimu aliamua kwenda kuiona. Wahabeshi wakaanzisha vurumai uwanjani wakati mechi inaendelea na ikabidi mabomu ya machozi yapigwe na baadhi ya wachezaji wao walipata mkong'oto toka kwa FFU. Hili na lile la timu kucheza vifua wazi likamkatisha tamaa Julius hakukanyaga tena katika mechi yoyote ile ya Taifa Stars.
 

msondo kulikuwa ndio maskani ya wababe. nakumbuka mtu ukiingia unaweza ulizwa "kijana umekuja mupweke au na mukaka yako?" kisha mtu unajibu "na mukaka wangu" halafu unapandisha t-shirt yako kidogo kumuonyesha muuliza swali nanga/kisu ulichobeba lol
 
msondo kulikuwa ndio maskani ya wababe. nakumbuka mtu ukiingia unaweza ulizwa "kijana umekuja mupweke au na mukaka yako?" kisha mtu unajibu "na mukaka wangu" halafu unapandisha t-shirt yako kidogo kumuonyesha muuliza swali nanga/kisu ulichobeba lol

...ha ha ha... hillarious! 😀

Zamani undava/Utemi ilikuwa ndio desturi eeh!?... nakumbuka kipindi fulani madogo walisumbuliwa sana na yanki mmoja mitaa ya ilala/uwanja wa karume aliyekuwa anajiita eti Mtemi Sigasiga!

Mndava huyo kwanza alikuwa na tabia ya kuacha signature yale kutani kila anakopita mfano wa Graffiti, Sigasiga kapita hapa,... halafu madogo wakikutwa na raba mtoni lazima wamuachie,... 😀

Tabia ya ubabe zilikuja rithiwa mpaka mashuleni, 'Vita' baina ya shule za Tambaza na Kinondoni katika mechi za Mpira hususan pale Uwanja wa shule ya Muhimbili, enzi hizo kina Athumani China, Amasha, etc
 
Mwanakijiji,
Tumetoka mbali. Hiyo tabia ya kwenda airport niliendelea nayo hadi hapa Marekani mpaka walipozidisha parking fees.

Hivi kwanini tulikuwa tunafunga safari kwenda Airport kuangalia ndege zikipaa na kutua? Yaani mgeni akija kutoka bara mojawapo ya maeneo ya kumpeleka ilikuwa Airport.!!

...cha ajabu basi, wakati huo zilikuwa zinakuja ndege za mashirika makubwa kama PAN AM ya marekani, SABENA ya ubelgiji, AEROFLOT ya mrusi, ALITALIA ya muitaliani, LUFTHANSA ya mjerumani, hata AIRFRANCE ya mfaransa! ...Jumatatu mpaka jumapili kwa ratiba nilijua saa ngapi na siku gani ndege gani ingekuja pale Dar Airport, terminal 1

Wakati/Baada ya kujengwa Terminal 2 kuboresha huduma, mashirika yote hayo yakasitisha huduma kuja Dar es salaam mpaka leo, tumebakiwa na BRITISH AIRWAYS, SWISSAIR na KLM tu toka Europe, na walobakia ni waarabu wa EMIRATES, QATAR. ...sijui GULF AIR bado wanatua?, maana nao shughuli ilikuwa inawapata kutua kwanza Zanzibar kisha Dar kwa ndege kubwa.

What happened? miaka hiyo ya 70's na 80's wasafiri wazawa hawakuwa wengi kama miaka hii, au ndio kusema watalii nao wamepungua? Sidhani madai ya usalama duni katika kiwanja chetu zilichangia, au?.
 
Inawezekana si habari ya usalama duni tu, na hali ya kiuchumi ya haya mashirika nayo haikuwa nzuri. Baadhi mpaka leo yako ktk hali mbaya, mashirika yaliyoendelea kuja sasa hivi yanatesa sana. Karibu kila shirika lina safari za kila siku tena moja kwa moja, na kama KLM ndio wanatesa kweli ni kama wanakuja mara 2 kwa siku kwani ukitaka kuja na kufika mchana wanakuunganisha na Kenya Air kupitia Nairobi, ukitaka kufika usiku unakuja nao moja kwa moja toka Amsterdam. Watalii wameongezeka sana mkuu, KLM inasomba mpaka inakuwa kama daladala ila wengi wanashuka Kilimanjaro.
 
Hivi, nani walikuwa lead musicians wa Cicko Kids? naona tumewasahau hawa.

Halafu kulikuwa na jamaa anaitwa Frank na dada zake!

Nadhani kuwa Kiko Kids ilikuwa inaongozwa na Salum Zahoro. Mara ya mwisho nilipoondoka pale Dar alikuwa mmoja wa nguzo za Shikamoo na alikuwa akiziimba zile nyimbo za Umeniacha Mpenzi, na Wamtetea Bure kwa ustadi sana.

Frank alikuwa jamaa mmoja aliyezaliwa na baba mzungu na mama mchagga wakati huo wa ukoloni; jina lake kamili lilikuwa ni Frank Humplick. Frank alikuwa mwimbaji na mpiga gitaa maarufu sana wakati ule. Alikuwa akipiga muziki wake akishirikiana na dada zake wawili Maria Regina na Tecla Humplink. Mzee Frank alifariki 25 August 2007 huko Lushoto. Nilisoma na binti yake pale UDSM, alikuwa Civil Engineering; dada huyu alikuwa na akili sana, ndiye aliyekuwa mwanamke wa kwanza kupasua na kubakishwa kufundisha pale engineering. Nadhani ni alikuwa kachukua kwa babu yake ambaye alikuwa ni Civil Engineer pia. Baada ya kwenda kuchukua Masters yake huko MIT hakurudi Tanzania tena, nasikia siku hizi nadhani anafanya Umoja wa Mataifa.

Baadhi ya picha za mzee Frank za miaka ya karibuni ni kama hizi zifuatazo.



 

Attachments


Umepatia kila kitu; ilikuwa ni mwaka 1974.
 

Wakati nikiwa Tambaza kila alhamisi mchana British Airways lilikuwa linatua wakati huo ikiitwa BOAC kutoka London. Schedule yake ni kama ilikuwa imepandikizwa kichwani.
 
Safarilands.org

To this day in Majita there is a place called Iramba. Kitundu and Magembe are Bajita names.
Rev. Kishoka upo hapo?
There are more of us who came from Burundi than we realize.

Jasusi unaniangusha aisee, Wajita hawasemi Iramba; wanasema KWIRAMBA.
 
Wakati nikiwa Tambaza kila alhamisi mchana British Airways lilikuwa linatua wakati huo ikiitwa BOAC kutoka London. Schedule yake ni kama ilikuwa imepandikizwa kichwani.

Du! hii itakuwa zamani sana, mwaka gani huo?. Mimi British Airways ninayoikumbuka ni ile ilikuwa na kofia ya malkia, halafu ilikuwa Boing 747. Ilikuwa inafika saa 12 alfajiri, ikiwa inatua ilikuwa na madoido ya jinsi yake hivi tofauti na ndege nyingine. Ilikuwa raha kweli kiitazama, nakumbuka siku nilipopata bahati ya kuipanda ilikuwa kama nimeokota nyota ya jaha vile, kila mtu alinihusudu.
 

Ahhh sasa Jasusi mbona unaleta Utani mbele ya hadhara bwana? Unataka Mpaka Mwalimu Kichuguu naye ajue kuwa ni "mujukuu" wetu?

By the way alieandika ni Baba Mdogo!
 
msondo kulikuwa ndio maskani ya wababe. nakumbuka mtu ukiingia unaweza ulizwa "kijana umekuja mupweke au na mukaka yako?" kisha mtu unajibu "na mukaka wangu" halafu unapandisha t-shirt yako kidogo kumuonyesha muuliza swali nanga/kisu ulichobeba lol

Kafara,

Hii ya "Mukaka Yako" ni kali nilikuwa sijawahi kuisikia, sishangai Gurumo alipokuwa Sikinde alirushiwa mavi na jamaa wa Msondo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…