Tukumbuke Zamani: Historia ya Taifa letu katika picha

Kisa cha Mwalimu kuacha kwenda uwanja wa Taifa kuangalia mpira ni siku ilipotokea fujo uwanjani.Wachezaji wa nchi ya kigeni,sikumbuki kama ni Sudan au wapi,walifanya fujo na matokeo yake FFU waliingia uwanjani na kuanza kuwashughulikia,kuna mchezaji alipigwa na kukimbia mpaka pale chini ya jukwaa la viongozi akiwa kama anamuomba Mwalimu awasaidie.Baada ya hapo Mwalimu hakwenda mpirani tena
 


si arusha jazz...ni ..KURUGENZI JAZZ BAND ...wana .."SUMU YA MAMBA"
 
Kuna habari zinasema SIkinde kabla ya kuchukuliwa na DDC ilikuwa inamilikiwa na na UwT na ndio maana Volvo nyingi zilikuwa zinajaa pale DDC Mlimani Park..

Senti zangu hamsini.

...GOTEE you are right UWT walikuwa wana influence kubwa kwenye ile bendi ...kama sehemu yao ya kupatia dataz...enzi hizo...pia walikuwa na mradi wa afrique h....

...taarifa nyingine niliyokuwa nayo ni kuwa kipindi MILTON OBOTE alipopinduliwa alipewa SIKINDE ili iwe kama mradi wake kwa muda apate pesa ya kula au ku m keep busy....hii sijapata kuingia kwa undani lakini najua members ie FMES....anaweza kuwa na details zaidi....
 

Mkuu Abel Baltazari, kama ninakumbuka vizuri,

Alianzia Msondo Afya, alipotoka yeye na Marijani Rajabu "Mwana-manyema", Chidumule, Beno, Chris Kazinduki, Gama, na wengineo walianzisha Dar International "Super Bomboka",

Marijani alikua na tabia ngumu sana kuelewana na wenziwe, ndipo Abel Baltazari, Cosmas Chidumule, King Enock michael (Msondo afya), na Hamis "Kumbakisa" wakaenda kuanzisha Mlimani Park, na jina Sikinde lililetwa na Chidumule kutoka Songea, unakumbuka ule wimbo "...usitumie pesa kama fimbo"

Baadaye naye Gurumo, Bitchuka nao wakaenda huko na ndio kwa mara ya kwanza wakaifanya Sikinde kuwa on the top, na later on Dede naye akaenda huko, sasa Bitchuka akarudi tena Msondo Afya, na kuungana kwa mara ya kwanza na Mkulu William Moshi TX (RIP).

ila uko sawa kabisa kuwa huyu alikuwa gwiji wa solo, na aliimba sauti ya kuongoza kwenye wimbo wa 'Magreti Mama" akiwa na Dar International.
 
GOTTEE
Unanikumbusha mbali sana kuhusu huyu shaaban dede
Mmanyema huyu pamoja na ukorofi wake mwingi maranyingi huwa hataki kuwa chini ya mtu ukubwa ana upenda na ni mwingi saaana wa mambo ya ndumba huyu jamaa
Napia niniulizia mpigasolo ambaye nilikuwa ninampenda sana joseph Mulenga ameishia wapi huyu mkulu?kama katika ile nyimbo ya nginde NALALA KWA TABUMIYE WALISEMAWATU LISEMWALO KAMA HALIPO LAJA
 
Wakuu wote heshima mbele sana, ninaomba kuwafahamisha kuwa tuko mbioni kukamilisha mipango ya kuihamimishia hii thread kwenye kumbu kumbu ya kitabu hivi karibuni sana, kwa hiyo ni ombi tu kwa wananchi wote tunaojumuika hapa kuwa kama wananchi wana picha zaidi wazibandike, na pia historia zaidi,

Thread bado ndio kwanza imeanza, na tunatoa respect na salute kwa wakuu wote wanaoshiriki hapa, maana as far as a simple and brief history goes, ambayo haikuandikwa na those in power, meaning kwamba ni unbiased, sidhani kama uanweza kupata fresh na straight to the point zaidi ya hii, halafu wakuu tunaomba historia ya upinzani nchini maana ina-miss sana so far!

Ahsante wakuu na tuendelee na vitu vya uhakika, lakini itakapofikia time ya kuanza kwenda kwenye kitabu tutawafahamisha, heshima kwako mkuu Mwanzage, kwa juhudi zako zote za kujaribu kufanikishwa kwa shughuli hii, ni Mungu tu ndiye anayeweza kukulipa.

Ahsante Wakuu wote na heshima mbele zaidi kama sio sana.
 
vilevile tusisahau kulikuwa na disco PARLIAMENT,waasisi wa wireless mike tanzania - DJ muasisi wa hii chama,JOE amefariki mwezi uliopita kwa ajali ya gari,mbuyuni,oysterbay(RIP)

Mkuu Son Of Alaska,

Huyu mkulu alikuwa na mwenzake DJ Eddy, vipi naye yuko wapi unajua long time sana, maana hawa mara mwisho niliwaona wakipiga nyumbani kwa aliyekuwa mwenyekiti wa simba enzi hizo Mzee Joakim Kimwaga, since then sijawahi kuwasikia tena vipi waliendelea au?

Duh! DJ Joe amefariki! habari ya kusikitisha hiyo mkuu, maana hawa wakulu walikuwa ni mabaharia wa nchi kavu, na walikuwa wakila pamba kama Cool and the Gang, kama uko karibu na familia ya mkuu fikisha salaam,

Salute!
 
... 'Unalewa bila kipimo hata watoto huwakumbuki' ...

"nguo zimekwisha na wewe hujali hata" "hujali hataaa"

mkuu gottee, umenikumbusha mbali saaana.
shukurani kwa hamsini zako
 
Last edited:

jamaa si ndio alitoa ile singo yenye maneno
dada-kachote maji ernesti, enersti
frank- na nini?
dada- na mtungi, ernesti, ernesti, na mtungi, enesti,enesti
frank- una shimo
dada- kazibe enesti, enesti...

kibao hiki kilipewa tafsiri tata mtaani lol

kuna wimbo nadhani wa dar jazz ulipigwa marufuku ulikuwa unasema
"chenyewee kimejibanza..."
 
Kafara,

Hii ya "Mukaka Yako" ni kali nilikuwa sijawahi kuisikia, sishangai Gurumo alipokuwa Sikinde alirushiwa mavi na jamaa wa Msondo!

kuna washkaji wangu walikwenda amana kufika huko bahati mbaya
hawakuwa na "mukaka yao" basi wakati wanacheza akawazukia
mbabe mmoja na kuwaambia " vijana hapa tunacheza kwa kuweka
mguu mmoja mbele na kukita chini na mukono mumoja umekuja
kama bawa la ndege anataka kuruka" halafu akatoa demo na
kuwaamrisha washikaji wafuate anavyocheza!!
 

Mkulu Shaaban Dede si mmanyema ni mhaya
 
Asante masatu [kisiki]
kumbu mzee ni kingulungulu
nikumbushe kidogo unaweza ukanimalizia...........Mama aeae mandonaee mtoto wa kwetuee mandonae naomba imalizie kigowakuu nafikiria hiyo ni kamanyola bila jasho
 

Sawa sawa mkuu, siku hizi mkulu Fresh Jumbe ana bendi yake binafsi, ingawa sometimes hurudi na kujumuika na Msondo Ngoma, lakini yeye ana-base Japan na hata youtube yuko sana.
 

Saafi sana mkuu, na heshima mbele habari nzito na iko sawa inaonyesha ulikuwepo, unajua habari ya kusoma na kuhadithiwa na kuiona huwa zinajisema zenyewe, hii yako mkuu ni clear kuwa ulikuwepo, ubarikiwe mkuu!
 
ongezea stc/biashara jazz band

Ni kweli mkuu, hii bendi nayo ilikuwa ni ya zamani sana, na ilikuwemo pia kwenye list wakati mmoja, ikiongozwa na Juma Ubao, aliyekuwa akipiga solo na kuimba pia, kwa mtindo wa "Kumbakisa Imejipa", hawa nao walitoa vibao vingi sana safi, kama "Kasome Paule" na "Opresheni Maduka", aliziimba akishirikiana na Hamisi Kumbakisa, aliyehamia Sikinde, na Roy aliyekuwa kiongozi wa Bima Lee na kutoka baada ya Dede, kuingia Bima Lee yeye alirudi Biashara Jazz.

Kuhusu Sikinde na uwt, ninajua kuwa once uwt ni forever uwt kwa hiyo basi Sikinde bado ni uwt hiyo DDC ni kanyaboya, au?
 
"nguo zimekwisha na wewe hujalita" "hujali hataaa"

mkuu gottee, umenikumbusha mbali saaana.
shukurani kwa hamsini zako

Mkuu pia kumbuka ngoma zingine za William Moshi TX, akiwa Police kama "Mayasa" na "Msafiri Kafiri", halafu unajua jina hasa la Moshi lilikuwa ni Khamis Kishiwa, lakini somehow he became Moshi William TX, huyu atakumbukwa sana na tena daima maana ndiye mmoja wa Old school aliyebaki ambaye alikuwa bado anawika sana,

pamoja na hii mibongo flavor yaani mtu mmoja tu anakwenda studio anapiga muziki peke yake, siku moja pale Dodoma mjini kwenye Cafe moja ya nje nilikutana na mwanamuziki mmoja wa zamani kwa jina Kassim Mapili, ninakumbuka alivyoniambia kwa uchungu sana kuwa siku hizi hawa watoto wanaingia studio na kupiga mziki bila ya vyombo na wanatengeneza millions, sisi tuliohangaika usiku na mchana tuko hohehahe, ni kweli kabisa,

Lakini umesikia siku hizi hata hawa kina Bongo Flavor, inabidi wapige dansi na vyombo ili wananchi wengi waje, yale mambo ya kupiga na DJ tu siku hzizi wananchi wamewashitukia, Banana Zoro, mtoto wa Zahiri Ally Zoro, aliyekuwa nyoia wa bendi ya JKT B stationed @ Mafinga, yaani Kimuli Muli Ngoma, inasemakna ndiye anyeoongoza sana kwa mapato ya kibiashara baada ya kuwa wa kwanza kuelewa hili na kutafuta bendi kamili kwenye kupiga dansi.
 

mkuu unanikumbusha zahir ally na wimbo wake wa "christina (sina hakika kama ndio ilikuwa title ya wimbo). wimbo wenyewe chorus unamaneno yafuatayo;

"kitu mapenzi kilianza samani tokea enzi za mababu zetu, na hata wao
mapenzi waliyakuta tokea enzi za adamu na eva. yalianza zamani nasi
tuliyakutaa"

banana zorro ana bendi yake inaitwa b-band. na hata j-dee
naye anayo yake inaitwa machozi.
 
pia tusiwasahau wana michezo ya nguvu.
namkumbuka power mabula. mheshimiwa huyu
alikuwa anaweza vuta gari kwa meno. kali ilikuwa
anapokunywa chupa nzima ya orange squash
kisha ndio anakunywa maji ili vikachanganyike tumboni.
 


...kuna kipindi akionekana Ngakakuona, watu wazima wenye heshima na akili zao wanakesha usiku kucha wanampigia ngoma mnyama huyo, kisha katika pembe nne wanamwekea silaha, upande mwingine nafaka, kisha pande zilizosalia maji na mwisho sikumbuki... upande ataoelekea kamnyama haka ndio 'utabiri' wa mwaka huo

mnh ama waweza mnyang'anya mtu mali zake zote ila Imani , mnnhhh!!!




...Mwalimu na Madiba
 
Last edited by a moderator:
kafara, you made my day,yaani power mabula anakunywa orange squash,alaafu ndio anakunywa maji yakifika tumboni,yafanye kazi ya ku dilute hiyo orange squash!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…