Tukumbushane 1,2,3 za udereva wa magari makubwa na Thomas B. MWAMFUPE

Tukumbushane 1,2,3 za udereva wa magari makubwa na Thomas B. MWAMFUPE

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
76,107
Reaction score
160,001
Chunguza upepo wa gari yako

#Roadlife.Tuendelee kukumbushana kuwa dereva ukiendesha lori lako jitahidi kuangalia geji zako zote mara kwa mara,tofauti yake ni kuwa madereva tunaangalia saana geji ya mafuta,geji ziko nyingi na kila moja ina umuhimu wake, ipo geji ya
Mafuta
Upepo kwenye mitungi
Temperecha
Oil presha ni,
Sasa basi ukiachia mbali geji ya mafuta hizi nyingine ukiona inashuka tafuta mahali salama paki gari yako ichunguze uangalie ni kwanini inashuka
KUFELI KWA BREKI.

Chunga sana geji ya upepo ukiona inapungupungua simamisha gari uone kama kuna likeji kwa kawaida kuna kiwango cha chini cha geji yako ya upepo na kiwango cha juu,upepo ukizidi au ukijaa sana gari itatema nnnnshhaaaaa lakini itaendelea kuwa juu kwa kipindi kirefu,ukiona geji yako inashuka mara kwa mara stuka,inawezekana gari yako haiko sawa,simama uichunguze na kama dashbodi yako nzuri basi taa itawaka au itapiga alamu tiiiiiiiiii,ujue hapo sio poa.Sasa hizo ndio baadhi tu ya dalili za awali kuwa gari yako inaweza KUFELI BREKI wakati wowote.

Upepo ukivuja utasababisha BREKI kuwa za mashaka na upepo unaweza ukawa unavuja sehemu ambayo sio rahisi kusikia au kuona,kwa uzoefu wangu upepo ukivuja kwenye breki chemba inasumbua sana kugundua hasa gari ikitembea,na kuvuja au kupotea kwa upepo ina maana upepo unaozalishwa na kompresa haukai kwenye mitungi,kawaida gari haitakiwi ivuje hata kidogo Lakini nikukumbushe tena kuwa gari inafua au kuzalisha upepo mwingi ikiwa kwenye gia kubwa ,na baadaye tutaangalia gia kubwa ni zipi.

Sasa kijiswali kidogo kwenye hiyo picha upepo unatosha au hautoshi

1661293328067.jpg
 
Back
Top Bottom