Tukumbushane enzi hizo Wasanii wanazindua Albamu zao!!

Greatest Of All Time

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2017
Posts
23,620
Reaction score
52,790
Zamani wasanii wa bongofleva na muziki wa dansi walikuwa wanautaratibu wa kuzindua albamu zao ukumbini.

Wote ni mashahidi, nani asiyejua kumbi maarufu kama Diamond Jubilee ambazo ili uweze kuujaza ilihitaji uwe katika kariba ya akina Juma nature na wengineo.

Je unakumbuka nini enzi zile wasanii wanazindua albamu zao ukumbini? Albamu zipi zilikuvutia? Visa na matukio katika uzinduzi wa albamu hizo.

Karibuni...
 
Umenikumbusha Ali Choki na kisa cha Farasi pale Diamond Jubilee.

Ali Choki akiwa katika ubora wa pekee katika dansi alizindua albamu yake siikumbuki jina, sasa akamua kuingia na farasi jukwaani.

Akatokea " mwehu " mmoja akaenda kumtekenya yule farasi aliyepanda Ali Choki.

Basi kilichofuata hapo ni Ali Choki kuanguka chini na toka siku hiyo akaanza kujulikana kwa jina la " Mzee wa Farasi ".

Nje ya mada:
Wangapi mnakumbuka vile viatu ( open shoes ) vilivyokuwa vinaitwa ali choki?
 
Hahahah huyo jamaa ana hatari sana.. muigizaji wa superman christopher reeve alipooza kisa haohao farasi
 
Baadaye akaona isiwe tabu, akaingia ukumbini na tingatinga...

Banza Stone akampa kijembe "Nyumba ya sterehe Kijiko kimefikaje?"
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
ha ha viatu vya choki vilisumbua sana...kuna mwingine aliingia na kijiko sijui nani ila Banza alidiss kwenye moja ya nyimbo za TOT BAND...."Kwenye starehe kijiko kimefikaje "
 
Pia kuna mwaka fulani Mr. Nice enzi hizo akiwa hakamatiki wala kushikika akaenda kuzindua Albamu yake ghafla bin vuu, Dudu Baya huyu hapa!!

Alikula vitasa vya kutosha kutoka kwa Dudu Baya!!
Mpaka leo sijuagi ugomvi wao ulikuwa nini?
 
Mi nakumbuka jinsi Solo Thang alivyoshindwa kuzindua album yake baada ya kutekwa na kikosi...sasa sijui alitekwa kweli ama zilikuwa kiki tu.
Album ilijulikana kama KIMA CHA CHINI (KCC)
Ni moja ya Album bora kuwahi kutokea katika Bongo Fleva.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…