Tukumbushane: Hivi Diamond alimpiga bao wapi Belle 9? Kwani wote walitoka kipindi kimoja!

Mkuu Diamond alianza kuonekana ana nyota ya kukubalika zaidi kuliko belle 9 wakati waliposhindana kwenye tuzo za kili music awards....ikumbukwe kuwa wakati huo 2010 wote hao walikuwa ni underground na hawakuwa na beef na media au wadau wakubwa wa bongofleva...hivyo ni wazi kuwa wote walikuwa wanategemea nguvu ya mashabiki...pia ikumbukwe kipindi hicho diamond hata hizo skendo alikuwa hana kbs yani bado kinda.

Sasa nashangaa unaposema belle 9 alikuwa juu zaidi ya diamond wakati wanaanza kutoka,na ilhali mashabiki waliamua kwenye tuzo za kili kwa kumtunukia diamond tuzo 3 kwa mpigo...baada ya hapo ndipo dogo akaanza kuinyoosha bongofleva maana kama chura ndo keshapigwa teke.

Wimbo wa mbagala huwezi kuufananisha na ngoma yeyote ambayo ilitoka kwa wakati ule...yaani kipindi cha mbagala kulikuwa hakuna takataka unaweza ilinganisha hapo...hii ngoma ilibamba mpk kero tena kwa rika na jinsia zote.

Belle 9 alikuwa mkali kwa kiasi chake lakini hakuwahi kumfikia diamond na hata kwa popularity ya ngoma zao hakuna ngoma hata moja ya belle ambayo ilikuwa most popular kushinda ya diamond kidoooogo kwenye masogange alikaza ila nyengine hazikuwa za kutisha sana ukilinganisha na pini za mondi....ukikaa na kuvuta picha kwa makini sana utaungana na mimi katika hili.

Ngoma kama, mbagala, nalia na mengi ft chidi benz, moyo wangu, mawazo ilikuwa ni misumari ya hatari kwa taifa aise...
 
Diamond ajaanza na belle 9 .
Mondi alikuwa na pacha wake anaitwa shetta sasa ndo ujiulize kwann Mondi kampiga gepu shetta ?

Belle 9 so talented boy bt mfumo wa watu wa ghorofani pale mlalakua ulimu underrate Sana . Jiulize yule demu Ruby yupo wapi ? Clouds imewapotezea wengi sana future.
 
Hapo ni kijana wa mkoa vs kijana wa dar lazima wa dar ashinde tu
 
Kwa wenzetu mamtoni hili liko wazi ila kwa bongo hawataki kulikubali ila ndio fact utake usi take, ili uwe famous and rich lazima uwe chamani.

Huu ndio ukweli mchungu kwa hiyo mnaposhangilia mafanikio yake mkubali pia kumeza huu ukweli mchungu.
 
Jiulize tna n hii alikiba alitoka pamoja na z anto ila z yupo wapi nbka leo.....
Alikiba hajatoka na Z Anto, Alikiba alitoka na Marlaw tena walikuwa na kaupinzani enzi hizo, kipindi Alikiba anatamba na Cinderella Marlaw alikuwa anakimbiza na Bembeleza. Mtoa mada ukiweza andika makala jinsi Alikiba alivyompiga gap Marlaw baada ya kumuoa Besta[emoji1], kipindi kile Alikiba alikuwa anaumizwa kichwa na Marlaw, maana hata tuzo za Kili alikuwa anazizoa mbele yake
 
kwa kweli shida ilianzia hapa, kwa kipindi hicho ilikuwa ni tukio la ajabu msanii kuchukua tuzo 3 kwa mpigo, wakina Lady Jaydee waliwahi kuchukua tuzo 2 ila sio 3, so ilimpa attention kubwa Diamond kwa kipindi hicho ukifungulia redio story ni yeye na tuzo 3, na dogo aliitumia hiyo nafasi vizuri kutoboa kwa hiyo tumsifu kwa hilo. Kina 20% walipata attention kwa tuzo 5 lakini hawakufanya lolote la maana baada ya hapo
 
Mi nakumbuka twenty percent aliwahi chukua tuzo tano kill music awards "
 
Umenikumbusha kitu kingine katika kutumia fursa...ndo maana hata baada ya kuvunja record ya 20% kwa kuchukua tuzo 7 kwa pamoja (bado haijavunjwa hii rekodi) mondi hakujibweteka alizidi kukaza sana mpk hapa alipofikia leo...tutake tusitake dogo anajua hlf mjanja sana
 
Usizunguke mbuyu Diamond skendo ndo zilimuweka juu + tuzo 3 za kili awards akaanza kuwacheza shele bongo muvi hapo akawini udaku wote

huu ni ukweli mtupu. skendo zinasaidia sana kukupa attention kwenye vichwa vya watu, belle 9 enzi hizo skendo aliyoipata ni moja tu ya kutoka na aggy masogange ila diamond kachepuka kwa mastar wenzie na data zake zilikuwa rahisi kupatikana kwa mapaparazi. sometimes unaweza ukakaa na celebrity wa kike hata kama sio demu wako you have to do something kwa mapaparazi kesho uwe kwenye "fent ford" na ndicho alichokifanya diamond. Muangalie harmorapa kuimba hajui ila angalia vituko vyake kwa celebrities wenzie mbele ya mapaparazi vilivyomfanya akapata Fame yakutosha kuliko hata mziki wake. na ilimsaidia hata "kiboko ya mabishoo" kusikilizwa na kutazamwa. Unapopunguza kuonekana kwenye medias ndipo watu wanapokupotezea taratibu na kukuona wa kawaida. mfano kama umechaguliwa kuwania tuzo flani wiki ijayo basi do something for the sake of makachero wiki yote uwe on air tu alafu uone kama hujashinda tuzo.
 
Ndio hapo, Diamond baada ya kuchukua tuzo 3 kwa mpigo, akafuatia na ngoma baada ya ngoma na zote kali. Watu wakaanza kumvesha masikio marefu Ali Kiba, na yeye akalinunua bifu bila sababu, akasema nimekuja kufuta vumbi kiti changu. Ndio akatoa wimbo wa Kimasomaso Mwanangu Usimuone.
 
sijaisoma makala yako yote
ila mimi nitajibu swali lako tokana na mujibu wa heading yako

nihivi katika maisha wote mnaweza mkawa mnafanya jambo moja lakini mkawa mnatofautiana vision ..mimi nimebahatika kuwa karibu na belle mnooo
belle alikuwa anahang na watu wakawaida ambao hawakuwa na malengo makubwa dhidi ya future yao ifahamike kuwa diamond hakufika pale alipo kwa bahati mbaya but alikuwa nimtu anayetembea huku akiwa namchoro wenye pictr kubwa unaomfnya atamani kufika pahala flani kwenye mafanikio aliyoyalenga ...
wakati diamond alikuwa anapambana kutafuta network mbalimbali zakumfikisha pale alipo Leo ...belle9 alirudi morogoro huku akawa anaendesha Nazi zake zamziki huko nawakati anafnya huvyo alikiwa ndio yupo juu mnoo
so akachagua kurudi Moro sehemu ambayo inaufinyu wa fursa za music so alitegemea nani wakumfuata huko nakumpa michongo...then alikuwa anafnya kazi kienyeji hkuwa kuwa na manager ..alikuwa na washkaji tu kina monagangster watu ambao sio wazoefu kiasi hcho katk tasnia ya music ...alipokuja kushtuka nakurudi dar...akakuta wenzake wapo mbali mnoo
sasa hivi amepitwa mpka nakina youngkiller
 
mkuu umechambua vizuri, aiseeh

sasa weka uchambuzi wa Diamond kumzidi Ally K

[emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16] [emoji16]

nataka ona K aliteleza wapi?

alafu uje uchambue kwa nn mr Blue yuko palepale hashuki wala hapotei,

pia uje uchambue muelekeo wa P Funk
 
Nakumbuka siku ya kwanza "nenda kamwambie" inatambulishwa Kama ngoma mpya mida ya jioni......siku hyo brother angu alinambia "huyu msanii anaimba vzuri Sana atafika mbali"" mi nikaona Kama ananipigia kelele Tu hata sikumjibu kitu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…